Mtoto wangu jamani

allina

Member
Joined
Mar 7, 2014
Posts
76
Reaction score
13
Natanguliza shukrani kwenu..ninamtoto wangu wadau,alipofikisha mwaka mmoja na miezi miwili aliugua ghafla nakulazwa rufaa mbeya,alipokuwa hapo alipumulia mashine kwa siku 26.

Na mwezi wa nne mwaka huu anatimiza miaka miwili nimeenda nae muhimbili kumfanyia CTC scan na picha tunayo lakini hakuna tulichojibiwa cha kitaalamu..tunae nyumbani kwa sasa.

shida hatua haziendi,hata kukaa pekeyake hawezi..

Nisaidieni mawazo jamani..akili yangu mpaka sasa imesimama.
 
Alipolazwa uliambiwa ana tatizo gani ?Tuanzie hapo kwanza,hatuwezi kukusaidia kama hatujui mtoto anasumbuliwa na nini!!

hawakutueleza kwakwel ila wao walidian ameangushwa na kusababisha mtikisiko wa ubongo..lakn kiukweli hakuangushwa..ha TCT scan wanaday hakuna shida..asa hatujui kama hapakuwepo wasomaji wa ile picha,mana walituambia tuende MOI.nako wakasema hamna shida.
 
tulimfanyia CTC scan wakasema hamna shida..ila mgongo wake laini sana..
 
Pole sana, Mungu atamponya...mshirikishe Mungu pia kwa kufanya maombi.
 
Pole sn dada hapo ni maombi tu,huyo ni shetan anataka kumuharibu mtoto..mtegemee Mungu atakusaidia tu.
 
Pole mwaya.

Endelea kuhangaika kwa wataalam mpaka upate majibu ya kueleweka. Pia usiache kumshirikisha Mungu.
 
1. Kama we ni mkristo funga na kuomba sana maana kwa mtoto imani yake inapitia kwa mama!! Mama akiamini naye ataponywa.. Na kama wewe ni muislam pia omba kwa imani yako na umpeleke kwa wanaouhusika...
2. Mpeleke kwa madaktari bingwa wa watoto ingia gharama tu muone specialist amuangalie aone tatzo hasa ni nini maana inashangaza unampeleka hospital na hawakuambii tatzo ni nini!!! Ni mara elfu wangekuambia hawaoni tatzo lolote kabsa !! Hapo tungeenda kukazania option ya kwanza....
Pole sana na Mungu ampe uzima malaika huyo...
 

Yasiyowezekana kwa wanadamu, kwa Mungu yote yanawezekana.
 
nashukuruni sana nduguzangu,pia samahani kwakuchelewa kuwajibu,nilikuwa kibaruani..Muombeni kwa kweli..Mungu ndie pekee..Mungu awabariki..vipi nipo nae hapa namfanyia wazoezi.
 
Kuna rafiki yangu mwanae aliugua ghafla after 3 months akaparalyse alikuwa na mwaka na nusu alimpeleka Nairobi akafanyiwa 2 operations. Moja ni ya spinal cord na nyiangine ya kichwa. Walimpima na kipimo kinaitwa MRI kwa sasa ni mzima na yuko class 1. Ila usimsahau Mungu
 
nashukuru ndugu yangu..unaweza ukampata na akakwambia ilimghalim kiasi gani lau nijaribu kujipanga pia..nisaidie kwa hlo bibi.com.ntanshukuru.
 
chaajabu ananguvu sana mwilini mwake..yan dah.hata sielewi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…