Mtoto wangu wa kike miaka 5 , anapitia changamoto ya mikono kutoka jasho na kutoka vipele

Mtoto wangu wa kike miaka 5 , anapitia changamoto ya mikono kutoka jasho na kutoka vipele

Pelly

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2013
Posts
287
Reaction score
370
Habari zenu,

Mtoto wangu wa kike miaka 5 darasa la kwanza, anapitia changamoto ya mikono kutoka jasho na kutoka vipele kama picha ninavyonekana, hali hii inasababisha kushindwa kuandika vizuri maana analalamika mikono kuwasha na kulowana kwa jasho, kwa nayejua jua dawa au maarifa naomba msaada wako.
Asante

IMG-20260818-WA0081.jpg
IMG-20260818-WA0079.jpg
 
Attachments

  • IMG-20260818-WA0081.jpg
    IMG-20260818-WA0081.jpg
    96.2 KB · Views: 11
Nilimpeleka ilipoanza tu akashauri tufanye alargy test ila alimpa dawa ya kupaka
 
Nilimpeleka ilipoanza tu akashauri tufanye alargy test ila alimpa dawa ya kupaka
Umechunguza aina ya mafuta anayojipaka na sabuni ya kuogea anayotumia? Inaweza kuwa hapatani navyo hasa sabuni na mafuta yenye kemikali kwa wingi na manukato makali...

Tafuta mafuta na sabuni nzuri ya watoto ya kuogea ambazo ni maalumu kwa ngozi ambazo ni sensitive...
 
Mafuta ya nazi parachut labda sabuni pia au chakula inabidi kuanza kubadili kimojakimoja, nashukuru sana wacha nifanye hivyo
 
  • IMG-20260818-WA0096.jpg
    IMG-20260818-WA0096.jpg
    122.3 KB · Views: 12
Mafuta ya nazi parachut labda sabuni pia au chakula inabidi kuanza kubadili kimojakimoja, nashukuru sana wacha nifanye hivyo
Maji yenye uvuguvugu na chumvi kiasi ni msaada pia kukausha vipele na kupunguza muwasho, unaacha anaweka mikono kwenye bakuli lenye maji vuguvugu na chumvi kiasi isiwe nyingi.. itamsaidia kupunguza muwasho na kukausha vipele... analoweka mikono kwenye bakuli dkk 10.. akimaliza unamkausha mikono kwa kitambaa kwa kugusa sio kama unafuta..
 
Pole
Nimerudia kusoma kumbe ni mikono tu, na inatoa jasho na kutoka ngozi
Hio ni hyperhidrosis

cc DR Mambo Jambo atakupa muongozo
 
keratolysis exfoliativa
Hakikisha mikono ya mtoto inakuwa na unyevu unyevu especially wakati wa usiku

Tumia gricelin kupaka kwenye mikono ya mtoto kisha mvalishe gloves kwaajili ya kulinda upotevu wa unyevu huo... Fanya hivyo kila siku kwa muda siku 14-21

Pole na uponyaji mwema
 
Maji yenye uvuguvugu na chumvi kiasi ni msaada pia kukausha vipele na kupunguza muwasho, unaacha anaweka mikono kwenye bakuli lenye maji vuguvugu na chumvi kiasi isiwe nyingi.. itamsaidia kupunguza muwasho na kukausha vipele... analoweka mikono kwenye bakuli dkk 10.. akimaliza unamkausha mikono kwa kitambaa kwa kugusa sio kama unafuta..
Asante nitafanya hivyo
 
Mikono kutoa jasho jingi na kutoka vipele au malengelenge madogo mara nyingi husababishwa na ugonjwa wa ngozi unaoitwa Dyshidrotic Eczema, msongo wa mawazo, au kutokwa na jasho kupita kiasi (Hyperhidrosis) kunakowasha ngozi. Vipele hivi huweza kuleta muwasho mkubwa na kukauka vibaya.Sababu KubwaDyshidrotic Eczema: Huleta vipele au malengelenge madogo yenye maji viganjani na kuwasha sana.Jasho Jingi (Hyperhidrosis): Hufanya mikono kuwa nyevu kila wakati, jambo linaloweza kuwasha na kuharibu ngozi.Msongo wa Mawazo: Wasiwasi na hofu huchochea mishipa ya fahamu kutoa jasho jingi na kuchochea vipele.Mzio (Allergy): Kugusa kemikali kali, sabuni, au vyuma kama nikel kunaweza kusababisha hali hii.Njia za Kujikinga na Kupunguza TatizoWeka mikono mikavu: Kausha mikono mara kwa mara na kitambaa safi.Epuka kemikali: Tumia glavu wakati wa kufanya usafi au kuosha vyombo.Tumia mafuta maalumu: Paka mafuta ya kulainisha ngozi (moisturizer) ili kuzuia ngozi kupasuka.Punguza mawazo: Pumzika na uepuke hali zinazokupa hofu au msongo.Je, vipele hivyo vina maji ndani yake au vinawasha sana? Naomba niambie ili nikupe ushauri mzuri zaidi.
 
Back
Top Bottom