Mtoto wetu anatulazimisha kupata mdogo wake, atoa masharti ya ajabu

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Wakuu,

kwakweli Tunashindwa kuelewa tumsaidiaje.

Siku za hivi karibuni mtoto wetu wa miaka 5 amekuwa akitusisitiza sana kuhusu kupata mdogo wake. Anatuambia kwa sauti ya kusononeka, “Nataka mdogo wangu... Nahitaji mdogo wangu kwa sababu hakuna mtu hapa nyumbani wa kucheza naye!”

1793169663466.png
Kiuhalisia, kama familia hatujapanga kuongeza mtoto wa pili kwa sasa, kwani tuna muda tuliopanga kuongeza mtoto. Lakini kijana wetu hataki kabisa kuelewa. Tukijaribu kumweleza kuwa mama bado hajawa tayari, yeye anasema kwa kujiamini, “Tunaweza! Kwani mama si ana maziwa tele!” Akatupa na masharti kabisa kuwa anataka mdogo wake awe wa saizi yake na mwenye sura kama yake, wala asiwe mtoto mchanga!

Hawa watoto wa siku hizi, acha tu! Yaani, anafikiria kupata mdogo wake ni rahisi kama kwenda dukani na kuchagua kile unachotaka! Eti ameona familia ya jirani ikiwa na watoto watatu, hivyo anataka na sisi tuwe kama jirani zetu.
 
Wakuu siku za hivi karibuni mtoto wetu wa miaka 4 amekuwa akitusisitiza sana kuhusu kupata mdogo wake. Anatuambia kwa sauti ya kusononeka, "Nataka mdogo wangu... Nahitaji mdogo wangu kwa sababu hakuna mtu hapa nyumbani wa kucheza naye!"

Kiuhalisia kama familia hatujapanga kuongeza mtoto wa pili kwani kuna muda tuliojipangia kuongeza mtoto, lakini kijana wetu hataki kabisa kuelewa. Tukijaribu kumweleza kuwa mama bado hajawa tayari, yeye anasema kwa kujiamini, "Tunaweza! Kwani mama si ana maziwa tele!" Akatupa na masharti kabisa kuwa anataka mdogo wake awe wa saizi yake na mwenye sura kama yake, na wala asiwe mtoto mchanga!

Hawa watoto wa siku hizi hawa acha tu! yaani anafikiria kupata mdogo wake ni rahisi kama kwenda dukani na kuchagua kile unachotaka!

Hapo unaomba msaada watu wakusaidie hilo tatizo? Changamoto kubwa miaka hii ni
1. Watoto wadogo kuoana
2. Wanawake kuoana

Mwanaume asingekuja andika upupu kama huu.
 
Wakuu siku za hivi karibuni mtoto wetu wa miaka 4 amekuwa akitusisitiza sana kuhusu kupata mdogo wake. Anatuambia kwa sauti ya kusononeka, "Nataka mdogo wangu... Nahitaji mdogo wangu kwa sababu hakuna mtu hapa nyumbani wa kucheza naye!"

Kiuhalisia kama familia hatujapanga kuongeza mtoto wa pili kwani kuna muda tuliojipangia kuongeza mtoto, lakini kijana wetu hataki kabisa kuelewa. Tukijaribu kumweleza kuwa mama bado hajawa tayari, yeye anasema kwa kujiamini, "Tunaweza! Kwani mama si ana maziwa tele!" Akatupa na masharti kabisa kuwa anataka mdogo wake awe wa saizi yake na mwenye sura kama yake, na wala asiwe mtoto mchanga!

Hawa watoto wa siku hizi hawa acha tu! yaani anafikiria kupata mdogo wake ni rahisi kama kwenda dukani na kuchagua kile unachotaka!
Naona hapa hakuna MTU, yaani hamna tofauti na huyu!
 
Attachments

  • downloadfile-8.jpg
    downloadfile-8.jpg
    81.3 KB · Views: 6
Wakuu siku za hivi karibuni mtoto wetu wa miaka 4 amekuwa akitusisitiza sana kuhusu kupata mdogo wake. Anatuambia kwa sauti ya kusononeka, "Nataka mdogo wangu... Nahitaji mdogo wangu kwa sababu hakuna mtu hapa nyumbani wa kucheza naye!"

Kiuhalisia kama familia hatujapanga kuongeza mtoto wa pili kwani kuna muda tuliojipangia kuongeza mtoto, lakini kijana wetu hataki kabisa kuelewa. Tukijaribu kumweleza kuwa mama bado hajawa tayari, yeye anasema kwa kujiamini, "Tunaweza! Kwani mama si ana maziwa tele!" Akatupa na masharti kabisa kuwa anataka mdogo wake awe wa saizi yake na mwenye sura kama yake, na wala asiwe mtoto mchanga!

Hawa watoto wa siku hizi hawa acha tu! yaani anafikiria kupata mdogo wake ni rahisi kama kwenda dukani na kuchagua kile unachotaka!
Pumbavu
 
mchaneni ukweli hamtaki mdogowake azaliwe avae sare za st.kayumba mnajipanga upya kwake mlikurupuka
 
Wazazi ni wazembe mpaka mtoto anawakumbusha wajibu wenu
 
Kwa akili zako hizi,hata huyo mtoto uliye nae,kama inawezekana kumrudisha tumboni,mrudishe haraka sana,
Hujui malezi ya jinsi ya kulea mtoto.
 
Mtoto hajataka kuwa mnafiki, kaweka wazi matakwa yake.

Sasa ni ni wazazi kufanya maamuzi yao.
 
Kama wazazi ndio myie mnaombwa wadogo mnakuja kuanzisha thread humu basi taifa limekwisha. Ndio mana watoto skuizi wanaropoka tu
 
Back
Top Bottom