Mtoza Ushuru, Askari, Daktari Muuguzi na Mwalimu ni kazi za WITO. Siasa ni uasi wa shetani aliouasisi pale Bustani ya Eden

Mtoza Ushuru, Askari, Daktari Muuguzi na Mwalimu ni kazi za WITO. Siasa ni uasi wa shetani aliouasisi pale Bustani ya Eden

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kinacholisumbua taifa letu la Tanzania kwa sasa ni kwamba watu hawajakaa kwenye nafasi zao kama walivyojaaliwa na mwenyezi Mungu kwa karama walizopewa.

Kazi za Wito yaani kiutumishi kwa mujibu wa maandiko matakatifu wamewekwa watu wasio na karama nazo. Ndio unaona TRA, Polisi na Hospitali zimegeuka kuwa vijiwe vya wala rushwa badala ya kuwa baraka kwa taifa.

Watoza ushuru. Madaktari, Polisi Manesi na hata walimu hawana hofu ya Mungu kabisa.

Tukumbuke katika utendaji kazi wa Yesu alitupa Ulinzi wa Roho mtakatifu, Uponyaji wa maradhi, Mafundisho na yeye mwenyewe alilipa kodi kwa Kaisari.

Siasa ndio kimbilio la wengi kwa sababu hakuna karama ya siasa.

Siasa iliasisiwa na shetani mwenyewe pale katika bustani ya Edeni alipomshawishi Eva " kwa maneno matamu" ili aasi agizo la Mungu.

Tangu uasi wa Adam na Eva bustanini Siasa hazijawahi kumuacha mwanadamu salama kwani amekuwa ni mtu wa kudanganywa maisha yake yote.

Mungu wa mbinguni awabariki sana.

Jumaa kareem!
 
Halafu huo uasi/siasa inalipa
 
Back
Top Bottom