Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Habari wakuu.
Nimekuja tena kuwatisha. Ipo hivi, watu wengi wanafikiri pombe huchochea utendaji wa akili, ukweli ni kuwa pombe hupunguza utendaji wa akili. kama ilivyo heroin. Ndiyo sababu mtu aliyekunywa pombe hawezi kufikiri wala kutenda mambo sawasawa. Inafanya hivyo kwa kuzuia sehemu ambayo vichocheo vya ubongo huenda kufanya kazi yake.
Kwa mtu ambaye ni mlevi kupita kiasi, ubongo wake hukabiliana na athari hizo za pombe kwa kutengeneza vichocheo vingi kupita kiasi. Ili walau uweze kufanya kazi. Sasa basi, siku mlevi huyu akiacha pombe ghafla, kwenye ubongo wake kutakuwa na vichocheo vingi sana na huku pombe iliyokuwa inavizuia kufnya kazi yake ikiwa haipo. Hapo shida ndipo huanza, ubongo unachochewa kufanya kazi isivyo kawaida. Hilo linaleta kuchanganyikiwa na hata kifo. Ni kitu cha hatari sana.
Mlevi sugu hatakiwi kuacha pombe ghafla.