Comrade Ally Maftah
Member
- Nov 6, 2016
- 77
- 271
MTU AKICHAGUA KUWA ADUI, USIMFANYE KUWA RAFIKI
Na Comrade Ally Maftah
JITU LA MIRABA
Katika maisha kuna watu wanatabia za chuki wanazaliwa nazo na wengine wanaziendekeza, unaweza kukuta mtu analazimisha kuwa na uadui na wewe, anaweza kutumia muda wake mwingi sana kuchambua chambua mapungufu yako na hatayakosa, kwani upungufu wa mwanadamu ndio ukamilifu wake.
Watu wa aina hii ukitenda mema anatamani lisuonekane, na ukitenda baya basi furaha kubwa anaipata. na wakati mwingine mtu wa hivi huparangana kuingilia uhuru wako, huja kama mtoa ushauri ili umwambie ushauri wako siupojei ageuze kibao kwamba unamtukana.
Mathalan Comrade Ally Maftah ameamua kuweka mitindo ya nywele kwenye kichwa chake, kwa gharama zake na mipango yake, anajitokeza mtu na vichuki vyake nikamwambia sitaki ushauri wako, mimi ninao washauri wangu wewe kashauri ndugu zako, akaanza kuleta ugomvi, na kaja mwenyewe, watu bwana, nikamuongezea wewe kama unaweza kushtaki tukutane mahakamani,. ni chuki tu.
Hoja ni kwamba mtu akichagua kuwa adui kamwe usimfanye kuwa rafiki, mweke kwenye kundi lake lile la Iron Friends, chukua tahadhari kubwa sana unapomkaribia, na ikiwezekana usimkaribie, akae mbali kabisa, akose ugomvi wa kudhihirika, atabaki akisononeka kukosa mivutano na wewe.
Ndimi
Comrade Ally Maftah
JITU LA MIRABA
CHALINENEE