Mtu akiiba KURA ADHABU IWE NINI?

Mtu akiiba KURA ADHABU IWE NINI?

fikirikwanza

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Posts
7,452
Reaction score
3,071
Kura ni maisha yetu ya kila siku, mtu anashikwa ameiba kura, au anakura feki, mtu huyo apewe adhabu gani??? maana hali ya wizi wa kura sasa imekuwa kubwa, hizi kauli za kulinda kura ndo Upinzani ushinde tunatakiwa kujiandaa mapema ili tunapokamata kura feki au wizi wa kura kwa kubadilisha matokeo, tuwe tunajua tunapaswa kuwafanya nini wezi hawa?? Cha ajabu na cha kuzingatia wengi wa wezi hawa wanashirikiana na vyombo vyetu, je tuwafanye nini wezi wa kura.

Kuna clip moja ya kijana wa tarime, akiwa igunga na tisheti ya njano anasema mipango ya kuiba kura ipo na usalama somtimes pamoja na tume ndo wanakula njama hizo na chama fulani hapa TZ. Tuwafanye nini wezi hawa maana hilo ndo tatizo kubwa jamii inamchagua S anashinda K.

Nawasilisha
 
Kula yake wapewe magamba kwani watakuwa wanauzoefu nazo coz ni ka tabia kao ka kuchukua kula mfu na kuzipa uhai hewa.
 
Aliyeibiwa ndio anatakiwa kupewa adhabu kwa sababu amethibitisha uzembe wa hali ya juu!!!
 
Kura ni maisha yetu ya kila siku, mtu anashikwa ameiba kura, au anakura feki, mtu huyo apewe adhabu gani??? maana hali ya wizi wa kura sasa imekuwa kubwa, hizi kauli za kulinda kura ndo Upinzani ushinde tunatakiwa kujiandaa mapema ili tunapokamata kura feki au wizi wa kura kwa kubadilisha matokeo, tuwe tunajua tunapaswa kuwafanya nini wezi hawa?? Cha ajabu na cha kuzingatia wengi wa wezi hawa wanashirikiana na vyombo vyetu, je tuwafanye nini wezi wa kura.

Kuna clip moja ya kijana wa tarime, akiwa igunga na tisheti ya njano anasema mipango ya kuiba kura ipo na usalama somtimes pamoja na tume ndo wanakula njama hizo na chama fulani hapa TZ. Tuwafanye nini wezi hawa maana hilo ndo tatizo kubwa jamii inamchagua S anashinda K.

Nawasilisha

akiiba kura, afutwe kabisa katika orodha ya wagombea mana what kind of the leader l we going to have in the future? mwizi, mdanganyifu, mtu ambae yupo kwa maslahi yake binafsi n ol those negative behaviours. Na hao vibaraka wake wapewe adhabu ya kufungwa miaka isiyopungua 10 na watoe compasation kwa taifa zima (waweza toa pesa zitakazoongezwa kwenye pato la taifa) kwa muda waliopotezea watu na kucheza na akili za watu.
 
Chadema watunge hiyo sheria, CCM waibe kura halafu utegemee adhabu ifate mkondo wake? Thubutuuuuuuuuuuu
 
Ukiandiaka habari za mashaka ambazo inaonekana ni uchochezi, faini au jela, je mwanasiasa akiiba kura jela miaka mingapi??? Daktari akikosea jela miaka mingapi? Hakimu akikosea jela miaka mingapi??? Etc
 
Nafikiri ni wazo zuri sijapitia sana sheria ya uchaguzi kama inasemaje lakiki ni muhimu kuwa na kifungu kikali juu ya hilo ka sababu huyu anacheza na maamuzi ya watu kwa mstakabali wa maisha yao.
 
Kwa maoni yangu hakuna kosa kubwa kama wizi wa kura, watu hawa tuwafanyeje jamani??? kila nikiangalia hakuna kitu kibaya mtu anamtendea mwenzake kama kuiba kura, aliyepiga na aliyepikiwa wanaathrika pia jamii kwa wakati huo huo inaathirika, utitiri wa viongozi ambao hawatakiwi, ambao wanajua hawatakiwi hivyo kazi yao ya kwanza madarakani ni wizi na dili.
 
Back
Top Bottom