Nimesikia mtu akingatwa na mbwa mwenye kichaa anachombwa sindano saba kwenye kitovu, ikiwa ni njia ya kuzuia yeye asipate kichaa.
Je, Hii ni kweli?
Je, Hii ni kweli?
- Tunachokijua
- Kichaa cha Mbwa ni ugonjwa wa kuambukiza unaoathiri mfumo wa kati wa fahamu yaani ubongo na Ugwe mgongo na kupelekea kupooza, kupoteza fahamu au kifo. Ugonjwa huu ni hatari na husabishwa na virusi viitwavyo kitaalam kitaalam kama rabies virus.
Kichaa cha mbwa, hujulikana pia kama hydrophobia, ni maambukizi ya virusi hatari wanapatikana kwa wanyama. Ni ugonjwa wa kuambukiza unaoenezwa kupitia mate ya mnyama aliyeambukizwa baada ya kuuma au kukwaruza mnyama mwingine au binadamu.
Ugonjwa huu unaathiri ubongo na mfumo wa neva wa mtu aliyeathiriwa, lazima uzuiwe kwa wakati. Dalili za ugonjwa wa kichaa cha mbwa si mahususi katika hatua za mwanzo lakini huathiri zaidi mfumo wa upumuaji, mfumo wa utumbo na mfumo mkuu wa neva.
Mtu aking'atwa na mbwa anatakiwa kupatiwa chanjo ya kuzuia virusi wa kichaa cha mbwa ili asipate maambukizi ya kichaa cha mbwa iwapo mbwa aliyemng'ata alikuwa na maambukizi ya virusi wa kichaa cha mbwa.
Mtu akiwa ameng'atwa na mbwa mwenye kichaa atakiwa kupatiwa chanjo haraka sana, ile chanjo ya kichaa cha mbwa na hiyo inatakiwa apatiwe muda mfupi baada ya kuwa ameng'atwa siku ya kwanza(1) siku ya 3, siku ya 5, siku ya 14 na siku a 90, anapata chanjo ya kichaa kwa ajili ya kuzuia wale virusi wasiingie mwilini.
Cha pili, kuosha kidonda kwa maji na sabuni yanayotiririka, lakini atatakiwa kutia dawa pale na taratibu nyingine za kimatibabu kulingana na ushauri wa daktari.
Je, ni kweli sindano ya kuzuia kichaa cha mbwa huchomwa kitovuni?
JamiiCheck imezungumza na Dkt. Dkt. Jofrey Josia, Mtaalamu wa Mifugo Kutoka Goba, Veterinary clinic ili kubaini iwapo ni kweli chanjo ya kichaa huchomwa kitovuni kama ambavyo imekuwa ikidaiwa na baadhi ya watu.
Dkt Josia amebainisha kuwa si kweli kuwa chanjo ya kichaa cha mbwa huchomwa kitovuni bali huchomwa kwenye eneo lenye nyama kama begani na inaweza kuchomwa makalioni pia.
"Inachomwa sehemu yenye nyama, mara nyingi ni begani, pia inaweza kuchomwa kwenye makalio, haichomwi kwenye kitovu"