Mtu aliyewasumbua majasusi wa Mossad kwa miaka zaidi ya 20 kufanikiwa kumuua

Shukrani mkuu, we must learn to live together as brothers and sisters to flourish or as a FOOLS to perish.
 
Nyingine inaitwa

Kill him silently (episode one na Two) ya Aljazeera hii ni shida

nyingine inaitwa What killed Arafat

Nyingine AGENTS OF ISRAEL


utajua Mossad wanavyohusika na matukio mazito middel east ili waendelee kuexist
Yeeaaahhh, hao jamaa ni MAGAIDI kuliko hao wanaoitwa hivyo, ila good people wapo silent
 
iko youtube! tafuta Mossad the world's most killing machine

Wale jamaa hawafai walimuua huyo weita Mbele ya mke wake Mjamzito kwenye mlango wa nyumba yao kumbe wamemananisha

Na hawakuomba msahama wala samahani....

Nafikiri uliona yule scientist alivyokufa aliyebuni SUPER GUN aliitwa Gerrard Bull ambayo hiyo super gun alikuwa anamtengenezea Saddam Hussein wakamvamia kwenye apartment yake huko Ubeligiji mji wa brussels na kumpiga risasi 5 za kichwa na kutoweka

na kesho yake vyombo vyote vya israel vikasambaza habari kuwa kauliwa na Agents wa Iran...

siasa za Middle east ni balaa
 

hawa jamaa mossad nimewavulia kofia mkuu
 
Kafiri namba moja ni marehemu mwamedi.

Sasa mmeanza kuchafua thread, humu tuzungumzie mambo black and white bila sentiments za kiimani ili kila mtu ayaelewe mambo bila chenga. Kila mtu ana misimamo yake, tukianza kuyazungumzia hayo, wengine tutakosa la kuchangia.
 

Precisely. I have always been thinking of writing something like this ila kwa upana ili watu waache kupigizana kelele humu kwa sababu ya watu wanaotafuta ugali wa watoto wao.
Kifupi, kuna vitu vikuu vinavyoongoza dunia na kikubwa ni pesa.
 

Hongera kwa post nzuri.....daah...kama vile na ww ni mdau vile wa ndani wa haya mashirika ya kijasusiiii!
Hiz excerpts ni kutoka kitabu au movie gani umezipata?
 
Hongera kwa post nzuri.....daah...kama vile na ww ni mdau vile wa ndani wa haya mashirika ya kijasusiiii!
Hiz excerpts ni kutoka kitabu au movie gani umezipata?

Hapana mkuu mimi sio mdau ndugu yangu, mimi raia tu wa kawaida sema napenda kufatilia na kujua vitu vingi, vitabu vinavyoelezea vitu hivi viko vingi sana, huwa napenda kusoma vile ambavyo vya uhalisia, sio finction. Mfano ni kitabu hicho nilichokitaja hapo cha Spies against armageddon , kingine kinaitwa Gideon's spies,kingine by way of deception, hivi vya middle east sana sana Israel, A spy'revenge cha waingereza, na The Quest for C and foundation of secret service kinaelezea jinsi shirika la ujasusi la MI6 au SIS ilivyoanzishwa na mambo mengi.Na kuna kingine nimeagizia kinaitwa Duet in Beirut kinaelezea assassination unit ya KIDON, kwa hapa bongo kuna jamaa anaitwa Godwin Chilewa aliandika kitabu kinaitwa IJUE IDARA YA USALAMA WA TAIFA nilisoma makala zake aliandika vichache ila akatengeza kitabu kinapatikana Amazon nilijaribu kununua online ila ikashindikana japo yeye haelezei matukio yeyote, Vitabu hivi vinakupa uhalisia wenyewe na matukio yaliyotokea, Movie na TV series pia unaweza jifunza mambo fulani kwa sababu movie zingine zime base kwenye vitabu lakini zingine zinakuwa ni finction hazina ukweli. movie ziko nyingi saaana, wewe search tu google spy film. Tv series inayofundisha mambo mengi ni Burn Notice, zingine ni the americans, homeland, covert affairs, n.k wadau watakuongezea. Mengine najifunza humu humu, pia tafuta documentaries youtube utazipata. Vitabu vya spies against armageddon na gideons spies nimewahi apload humu, kuna thread inazungumzia KIDON mwisho wa makala niliweka vitabu hivyo, vingine wadau watakupatia ukiomba. Elimu ipo wazi tu
 
mngony tuwekee mambo hadharani juu ya hili.

ushiriki wao hauelezwi vizuri mkuu, japo jasusi wao hodari na nguli barani Afrika alikuwepo Zanzibar wakari wa mapinduzi. Tufatilie wote kisha tuje tujadili
 

Umeelezea vizuri sana ile sumu ni nusu kaputi unalala unapitilza hukuhuko na kifo kinakukuta na ndio ilikua objective jamaa akutwe kafa kwenye gari akiwa kalala usingizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…