Mtu anaanzaje kumchukia ndugu yake?

Umeandika ukweli mkuu
Ubinafsi ni sifa ya nafsi kila nafsi yajitakia mema kwanza yenyewe
Ila kulijua hili na kuona utapambana nalo vipi ndio point amabayo tumetofautiana sana
Baadhi hawajui kabisa kuhusu hili hivyo upelekea nafsi zao kuwa hifadhi ya chuki na hasadi...na kwa kweli hamna maradhi mabaya kama maradhi ya hasadi.

Hasadi ni kutamani Baraka au neema ambazo mwenzio kazipata kutoka kwa mungu wake zimuondokee.

wengine ndio hivyo wanatamani hata wenzio wapate ajali au wapoteze na uhai kabisa...lakini chuki na hasadi kiuhalisia humchoma na kummaliza zaidi yule alievihifadhi
 
Hama yako umenunua bei gani,hongera kwa kumiliki ndinga kali
 
Ndugu lawama

Unashangaa mtu mwenye chuki kwenda kanisani?
Hata wachawi uwa wanaenda kusali kanisani..!
 
Jipende mwenyewe ndo ujifunze kumpenda mwingine...hii ndo falsafa yangu
 
Kumbe umeamua kuleta mambo ya familia yetu humu ndani? Kea kuwa umenunua gari aina ya nyundo ndiyo unipite bila kunisalimia?kwa hili sitokubali tutakutana jumamosi kwenye kikao cha familia
 
Ndugu wakweli siku hizi ni mke, watoto zako, baba&mama na washkaji. Mbali na hapo tegemea maumivu tu.

Mimi siongei na mdogo wangu na wajomba zangu chanzo mali zangu na kazi yangu. Wanatamani nifukuzwe kazi, nimepeleleza wanasema najisikia naringa nimekuwa sasa.
 
Kazi ipo
 
Kumbe umeamua kuleta mambo ya familia yetu humu ndani? Kea kuwa umenunua gari aina ya nyundo ndiyo unipite bila kunisalimia?kwa hili sitokubali tutakutana jumamosi kwenye kikao cha familia
Duh, jino kwa jino
 
Mkuu huyo ndugu yako anayekufokea hivyo una uhusiano gani naye??
Ni kaka, mjomba, shangazi au nani?

Hata baba yangu mzazi siwezi mruhusu anipande kichwani kiasi hicho aisee.
 

CHANZO CHA HIZI CHUKI ZOTE ZA NDUGU NI WIVU
Kasome visa vya hawa ndugu na wengine
1.Kaini alimuua Habili
2.Yusufu na ndugu zake
3.Rahel na Lea
4.Yakobo na Esau (mapacha)
 
Mh! mke ni ndugu siku hizi tayari ushatengenezwa wewe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…