LOTH HEMA
JF-Expert Member
- Dec 6, 2015
- 18,611
- 27,615
Imekuwa kawainda mtu fulani kuitwa jina la kabila lake au sehemu anayotoka na jina hilo kumkaa na kukubalika katika jamii anamoishi ugenini kufanya shughuli zake. Majina ambayo yamekuwa maarufu sana utasikia mtu akiitwa muha, mchaga na mpemba, akiwa na duka panaitwa kwa muha, kwa mchaga na kwa mpemba. Tanzania ina makabila mengi lakini ni hayo tu ndiyo yanayosikika watu wake wakienda kufanya biashara mbali na kwao. Labda wengine nao wanaitwa wanapokwenda ugenini kwa shughuli zao.