Mkuu Mzizimkavu na wenzako,fahamuni kwamba Mungu aliyeweza kufanya ''NABII MUSA ALIONA,FIMBO KAVU YA HARUNI IMECHIPUKA NA KUTOA MACHIPUKIZI;NA KUCHANUA MAUA;NA KUZAA MATUNDA YA MALOZI MABIVU,SIKU YA PILI YAKE KATIKA HEMA YA MUNGU;ILI KUKOMESHA MANENO YA WATU ![BIBLIA KITABU CHA HESABU 17:5-10].Kabla ya Bwana Yesu,miujiza ilitendeka na baada Kristo miujiza imeendelea kutendeka kila mahali ulimwenguni.Sikubaliani kamwe na msemo wa samaki mmoja akioza basi tenga zima limeoza;na kusema kuwepo wachunaji matapeli,basi wote ni wachungaji wasanii au wajasilimari.Nyakati zetu,wapo watumishi wa Mungu waaminifu wengi duniani,na Mungu anawatumia kuponya magonjwa yote kama UKIMWI na kila namna ya udhaifu kwa ishara,maajabu na miujiza kama nyakati za mitume na manabii wa Biblia Takatifu!!! Mwisho,nimepeleleza kwa muda haya,katika makanisa na huduma mbalimbali !
Mkuu
BAOBAO Usifananishe Miujiza Ya Nabii Musa aliyopewa
na Mwenyeezi Mungu kwa Firauni ukafafanisha na Miujiza ya Wachungaji hicho kitu sikubaliani nacho kabisa Nabii musa
alikuwa ni mtume wa Mwenyeezi Mungu Wachungaji wengi wao ni waongo wazinzi,wezi, wadanganyifu itakuwaje wawe
na miujiza? Ni uongo wa hali ya juu Hakuna miujiza ya kutibu Ukimwi hicho kitu sahau kabisa. Miujiza alifanya Bwana
YESU na wale Mitume wake 12 watu waliobakia ni matapeli wanafanya uganga pamoja na uongo wachungaji wengi
wanatumia uganga wa kienyeji kuwaongopea Waumini Eti wana miujiza kumbe ni amambo ya uganga wakienyeji na uongo ndani yake. mii pia ninaweza kufanya miujiza kama wanavyofanya wachungaji.
nadhani hujanielewa nilichoandika. MUNGU HUYU ninamwaabudu mimi ndiye huyo huyo anaendeleza uuambaji wake, wengine watasema kuwa tumesikia akitenda miujiza na wengine watasema nikiini macho, mimi daima mimi nitasema ni BWANA amefanya maana yeye amesema JINA LANGU LIATAKAPO TAJWA KWA AJILI YA KuTENDA JAMBO BASI MIMI NITASIMAMA UPANDE WANGU na KUTENDA kile ambacho neno limetumwa kutenda. SISI wengine ndugu yangu tumemuona YESU akitenda jambo katika maisha yetu, NIMEMUOMBA ANIVUSHE AMENIVUSHA MPAKA SASA NAAMINI NI YEYE AMETENDA, kumbuka mpaka leo yeye bado ni MUNGU ANAYETENDA KWAKE YEYE AAMINIYE.
Lakini hata hivyo nisikubishie sana, kwa sababu kuamini neno imani zinatofautiana ktk ukuaji wake (sorry kama nimeongea lugha usioijua hapo). Manabii wa uwongo pia wapo. Tatu mimi sijui wewe unamuabudu MUNGU yupi, naomba nikuulize Je, unaamini ktk MUNGU BABA, MWANA na ROHO MT.? MUNGU nimwaminiye mimi ni yule anayejitambulishe kwa jina la MIMI NIKO, AMBAYE NIKO- kama ndiye huyo nawe wamwamini amini kuwa anaponya
Mkuu
mwakaboko Mungu ninaye muamini mimi ni yule Mwenyeezi Mungu aliyeziumba mbingu na Ardhi na vilivyomo ndani yake wanyama ,Miti, wadudu,na banadamu . Na Mungu ninayemuabudu mimi ndiye yule
Mwenyeezi Mungu aliyewatuma Manabii na Mitume wake Ibrahim,Isaaka ,Yakubu,Mfalme Daudi,mfalme Suleyman,Nabii
Musa Bwana YESU,Na Mtume Muhammad rehema za mwenyeezi mungu ziwe juu yake na amani.Simuamini mi Mungu
katika nafsi 3 yaani Mungu Baba,Mungu Mwana,na mungu roho takatifu mungu watatu katika nafsi moja Mungu huyo
kwangu mimi anakuwa ni mungu feki kazi kwako na imani yako.