Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 3,189
- 6,140
Kwa miaka mingi sana hiki chama kimevuna na kukandamiza mno vyama vingine vya siasa, Kimenufaika kwa unyonge na udhaifu wa vyama vingine vya upinzani. Unyonge na umasikini wa vyama vingi vya upinzani vimewafanya watumike katika kuinyanyua CCM na kukandamiza demokrasia ya kweli.
Hakuna maendeleo au mambo ya maana yaliyofanywa na CCM kwa miaka zaidi ya 60 kukifanya kisalie madarakani kwa miaka yote hiyo! Ni ubabe na kujimilikisha dola na kukandamiza demokrasia ya kweli kumeifanya kuendelea kusalia hapo! CCM wametumia ujinga wa watanzania waliousababisha wao kwa miaka mingi kuwafanya waamini amani ni kuwa mnyonge na kukaa kimya! HAPANA! HII HAIKUBALIKI kwa miaka mingi wamepandikiza hofu miongoni mwa watanzania kwa manufaa yao binafsi kwa kichaka cha 'tuilinde amani yetu' amani bila haki?
Si bure nchi tunazoziita hazina amani kama Kenya zimetuacha mbali mno kiuchumi, huku sisi tukibaki na ardhi yetu kubwa, mito, maziwa, na rasilimali za kila aina zisizo na tija wala manufaa kwa watanzania walio wengi huku zaidi ya 50% ya watanzania wakiendelea kuteseka katika lindi la umasikini wa kutupwa! Kwa zaidi ya miaka 60 sasa!
Kwa kifupi
NO REFORMS NO ELECTION