Mtu anatekwa Stendi ya Magufuli huku watu wanaangalia? Wananchi tunatakiwa kujitafakari, imekuaje tumekuwa mazombi hivi?

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Mtu wa pili huyu anatekwa sehemu ambayo kuna watu na hakuna kitu raia tunafanya? Tunasubiri apotee ndio tuje mtandaoni kuanza kulaani na kulisema Jeshi la Polisi, Samia na Serikali yake?!

Pia soma: Breaking News: - Dar: Abdul Nondo amechukuliwa na Watu wasiojulika katika mazingira ya utatanishi Kituo cha Mabasi cha Magufuli

Wana Dar tuna nini? Ndio hatuna umoja kiasi hiki? Hili jambo lingetokea Chuga au sehemu nyingine wangekiwasha hadi kieleweke, na ijulikane hao watu ni akina nani. Walau hata kwa Bonge walijiongeza tukio likarekodiwa, huko watu wamekaa tu kama ndezi.

Wamejaribu kwa bonge wakaona jinsi watu hatuna umoja, leo wakaenda kwa chembamba wamprove kuwa wananchi tupo tupo tu!

Kwanini lakini tunakuwa mazombi hivi?
 
Dar unaibiwa watu wanakuangalia.

Dar unaporwa simu na vibaka Raia wanakuangalia

Dar unatekwa stand Raia wanakuangalia bila kuhoji

Dar mji wa wajanja,hakuna kama Dar Tanzania πŸ˜€πŸ˜
 
Tulia uelezee vizuri tukio lilikuaje, unavyoelezea ni kama vile na wewe ulikuepo eneo la tukio, umeshindwa kuchukua hata video au picha?
 
Dar hakuna wanaume mkuu! Yaani wapo wapo tu nawaangaliaaa! Mwanza kuna watu walitaka kumchukua mfanyabiashara kwa kisingizio eti wao ni Polisi, raia wakawaweka chini ya ulinzi wakitaka mpaka Mkuu wa Kituo cha Polisi Pamba aje kwenye tukio kuwathibitishia kwamba hao ni Polisi kweli! Dar jirekebisheni bwana!
 
SImba na Yanga
 
Dar unaibiwa watu wanakuangalia.

Dar unaporwa simu na vibaka Raia wanakuangalia

Dar unatekwa stand Raia wanakuangalia bila kuhoji

Dar mji wa wajanja,hakuna kama Dar Tanzania πŸ˜€πŸ˜
Na ndio kumejaa makanisa na misikiti watu wake ni watu wa Dini sana.
Unafiki mkubwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…