KWELI Mtu anaweza kujihisi amelewa bila kuwa amekunywa pombe

KWELI Mtu anaweza kujihisi amelewa bila kuwa amekunywa pombe

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Wakuu,

Kumekuwa na nadharia nyingi huku mtaani kuhusu ulevi bila kuonja kileo, sasa ndo wengine tunajiuliza inawezekanaje mtu akalewa bila kunywa pombe?
1785764452918.png
 
Tunachokijua
Mara nyingi imezoeleka kuwa watu wanaolewa na wale wa kunywa pombe. Lakini katika nyakati chache na za nadra mtu anaweza kujihisi amelewa bila kutumia kilevi.

Hali hii kitaalamu inajulikana kama auto-brewery syndrome, hutokea pale ambapo vijidudu vilivyopo kwenye mfumo wa chakula, hasa tumboni, vinapochachusha sukari kutoka kwenye vyakula na kuzalisha ethanol (pombe), kana kwamba kuna kiwanda kidogo cha pombe kinachofanya kazi ndani ya tumbo la mtu.

Watu wenye changamoto kwenye mfumo wa chakula wana wana uwezekano mkubwa zaidi ya kupata hali hii. Tovuti ya medical brief inafafanua kuwa watu wenye changamoto hiyo wamekuwa wakidai kukumbwa na hali hiyo baada ya kutumia vyakula vyenye sukari na wanga mwingi.

Dalili

Mara nyingi dalili zinazoweza kumpata mtu mwenye changamoto hiyo ni zinafanana kabisa na dalili za mtu aliyekunywa pombe. Dalili zinazotajwa ni kama vile kuzungumza kwa shida, pumzi kunukia kama matunda, kuyumba na kutembea, kutapika degedege, Kuchanganyikiwa au kushindwa kutambua mazingira vizuri (disorientation).

Dalili nyingine zinaweza kuwa maumivu ya tumbo, kupoteza fahamu, kuvimba tumbo na gesi nyingi, uchovu, kubagua baadhi ya vyakula, mafua, kikohozi pamoja na mabadiliko ya mfumo wa haja kubwa na ndogo.

Nini cha kufanya kuzuia uwezekano wa kutokea hali hii?

Ikiwa una moja au zaidi ya sababu za hatari zinazoweza kuongeza uwezekano wa kupata Auto-Brewery Syndrome (ABS), ni muhimu kuzingatia zaidi afya ya mfumo wako wa chakula ili kusaidia kuzuia kutokuwiana kwa vijidudu tumboni (dysbiosis).

Unaweza kuanza kwa kula aina mbalimbali za vyakula vya mimea na vyakula visivyosindikwa sana (whole foods), pamoja na kupunguza ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi na wanga mwingi.
Back
Top Bottom