Wakuu hii imekaaje maana nimeenda kupima urefu juzi nakuta urefu wangu ni kama umepungua hii imakaaje kitaalamu.
- Tunachokijua
- Kadri mtu anavyozidi ndivyo anavyozidi kupitia mabadiliko mbalimbali kwenye mwili wake ikiwemo uoni, usikiaji, kumbukumbu pamoja na nywele lakini pia anaweza kupoteza sehemu ya urefu wake.
Tafiti na machapisho ya afya yanabainisha kuwa binadamu anaweza kupungua urefu wake kadri anavyozeeka kutokana na mabadiliko mbalimbali yanayotokea kwenye mwili wake ikiwemo ya mifupa, misuli na viungo ambapo baadhi ya mabadiliko hayo yanaweza kufanya urefu wako upungue kidogo.
Makala ya cleverland clinic inabainisha kuwa hali huwapata zaidi haswa watu wanaoanzia miaka 40, lakini makala ya kituo cha afya cha UAM inaongezea kuwa kati ya miaka 30 hadi 70 mwanaume anaweza kupoteza hadi nusu Inch na mwanamke anaweza kupoteza Inch nzima.
Kwa kawaida kiwango cha urefu unaopaswa kupungua huwa ni mdogo sana yaani kati ya nusu Inch (sentimeta 1.27) hadi Inchi moja (Sentimeta 2.54).
Hivyo ikiwa utapitia mabadiliko makubwa ya kupungua urefu ni vema kuwaona wataalamu wa afya kwani inaweza kuwa dalili ya changamoto nyingine za kiafya kama vile magonjwa ya moyo ama uti wa mgongo.
Ingawa uzee hauzuiliki lakini inashauriwakupunguza baadhi ya vitu ikiwemo unywaji wa pombe, kutokuvuta sigara, kufanya mazoezi ya viungo kwa wingi pamoja na kula vyakula vyenye wingi wa ‘Calcium’ ili kupunguza uwezekano wa kupungua urefu.