mimiamadiwenani
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 5,718
- 7,784
Aug 26th, 024
Dar es Salaam, Tanzania
Saa 5:27 asubuhi
-------------------------------
Habarini madada, makaka, na wazee wenzangu!
Leo nivunje ukimya niongelee suala nyeti kidogo.
Umewahi kusaidiwa katika point ya maisha yako, na aliyekusaidia akataka uwe mtumwa wake?
Hiki kitu ni kansa mbaya sana.
Nilipomaliza chuo kikuu, mambo yangu fulani fulani hayakukaa sawa. Hivyo nilihitaji msaada fulani.
Nilisaidika lakini changamoto ikawa ni mimi kutawaliwa kimawazo na kifikra. Nikawa sina maamuzi.
Nikasita kufanya vitu vingi nikihofu 'atakwazika'. Nikashindwa kuishi maisha ya uhuru. Nikawa mfungwa aliye uraiani.
Ilikuwa ni ngumu lakini nilifanikiwa kuchukua maamuzi magumu. Nililazimika kuanza kubadilika.
Hapo nikaona rangi halisi za watu. Nikatambua watu ni nani!
Ukweli huu kuhusu watu uliniumiza sana.
Watu! Watu! Watu!
Kwako wewe, ulijinasua vipi na nyavu hii 'hatari'?
Ulifanya nini baada ya kugundua msaada ulioupata unakufanya uwe mfungwa? Uliona aibu?
Ulikabiliana vipi na maneno kama vile "binadamu hawana shukrani", " ila nilikusaidia wewe", "watu hawasaidiki" na mengine mengi ya kunyong'onyesha?