Mtu anayetumia ARV kwa muda mrefu virusi huwa havionekani kwenye vipimo vidogo?

Mtu anayetumia ARV kwa muda mrefu virusi huwa havionekani kwenye vipimo vidogo?

Watu mnapenda kudanganyana sana yaani.

By the way muuza duka la dawa wengi hawana taaluma ya maana kuhusu clinical medicine-wengi wao wamefunzwa kugawa tu dawa.

Ila kwa kuwa story za vijiweni ndiyo huwa tamu ,basi na story ziendeleee
 
Ahsante kwa taarifa, mtaangamia kwa kukosa maarifa...
 
Ninachoweza kusema
Mnadanganywa sana kuhusu haya maswala ya UKIMWI na virusi vyake
Comment zote nlizozisoma asilimia 95 Ni uongo

Elimu ! Elimu !Elimu
Kama jamii forum kwa magreat thinkers uelewa ndo huu huko vijijini na mitaani sijui kukoje

#elimu ya UKIMWI na virusi inahitajika
 
Ninachoweza kusema
Mnadanganywa sana kuhusu haya maswala ya UKIMWI na virusi vyake
Comment zote nlizozisoma asilimia 95 Ni uongo

Elimu ! Elimu !Elimu
Kama jamii forum kwa magreat thinkers uelewa ndo huu huko vijijini na mitaani sijui kukoje

#elimu ya UKIMWI na virusi inahitajika
Toa Elimu sahihi Sasa tujue lipi ni lipi
 
Kwa manufaa ya tusiojua na wanaojuwa watuhakikishie zaidi.7

Iko hivi hapa kazini kwangu jirani kuna duka la madawa,hivyo dada muuza dawa huwa tunapiga story za hapa na pale kiasi. katika story tukajikuta tunaongelea maambukizi ya UKIMWI. ndio nikamuuliza inawezekana kuna watu wanaleta dawa za ARV dukani kwako ili wasingudulike majumbani.. akasema ana watu wa hivyo kama watatu na wanampa pesa nzuri sana na nikiwaona siwezi jua kama tayari wanao.

Katika story akanitahadharisha juu ya watu fulani majirani mmoja ni dakitari ila cha pombe ambaya na huwa anakuja na mdada pale yule dada ana nata sana.. nikijua ni mke wake kumbe naye ni hawara yake tu. ndio akaniambia kuwa huyo jamaa tayari anao na kwa vile ni dakitari yeye anajua namna ya kujihudumia.. na mwanzo hakutaka waende na huyo dada bila kinga maana hataki maambukizi mapywa kwa usalama wake. lakini dada alikomaa wapime...

Kwa jamaa mwanzo aligoma ila akakumbuka kwa vile anatumia dawa na ni Muda mrefu anao na hataki maambukizi mapya wakakubaliana kupima kwa vile kipimo kidogo kwa maana ya kipimo cha kwenye kidole huwa hakisomi mwathirika anayetumia dawa vizuri.. dada na jamaa wamepima na wote wameonekana wako sawa..jamaa akamwambia nesi huyo dada anataka show ya kibabe hivyo kwa sasa jamaa ananunua dawa za kuongeza nguvu za kiume zile za bei ambazo zinakaa mwilini hata wiki mbili na sio za kumeza kila siku.

USHAURI TU. KAMA UNAAMUA KUPIMA PIMA KIPIMO KIKUBWA NA SIO HIKI CHA KIDOLE MAANA MTU HUENDA ANATUMIA DAWA NA ANAJUA FIKA KIPIMO HAKITA SOMA HIVYO KUPIMA KWAKE SIO TATIZO.

NB.. UKIWMI SIO MWISHO WA MAISHA WALA SIO MWISHO WA NDOTO ZAKO.. MAISHA NI YALE YALE TU
Habari!

Ili kuelewa haya mambo ni muhimu ukiwa na taarifa sahihi juu ya:

1: HIV virus na maisha yake
2: Ufanyaji kazi wa ARV
3: Ufanyaji kazi wa vipimo vya HIV

1: Kifupi: Virusi vya HIV huweza kuishi na kushambulia CD4 seli peke yake mwilini. Hii hutokana na CD4 seli kuwa na receptors/ milango ambazo hutumika kuingia kwenye seli husika. Kumbuka CD4 pia zina muda wake wa kuishi na kufa.
Hivyo, unaweza kuvifungia ndani ya seli husika au kufanya visishambulie seli mpya za CD4 na seli inapokufa itaondoka na virusi husika. Hapa ndo lilipozaliwa wazo la post exposure prophylaxis(PEP).

2: ARV: Hufanya kazi kwenye maeneo tofauti yanayohusisha: kuzuia HIV virusi asiingie kwenye seli mpya ya CD4 au asiendelee kuzaliana/kujigawanya ndani ya seli za CD4.

Hii huleta matokeo ya HIV kubaki ndani ya seli za CD4 ilizokwisha vamia au asiendelee na kuzaliana ndani ya seli husika.

3: Vipimo vya HIV:
A: Kuna vinavyopima antibodies(ambayo ni mfumo wa kemikali wa mwili unaozalishwa na mwili ili kujikinga au kupambana na kirusi husika). Kiasi cha antibodies hutegemeana na kiasi cha idadi ya virusi husika. Kadri virusi vinavyopungua, antibodies pia hupunguza taratibu. Kipimo kinachopima antibodies pia huweza kutoa majibu kulingana na kiasi cha antibodies. Kama kiasi ni kidogo sana basi reaction ya kuwezesha majibu kuwa chanya haitatoshereza kuleta majibu halisi/positive.

B: Kuna vinavyopima uwepo wa kirusi (DNA vs RNA). Hii huweza kupata majibu chanya kwani uwepo wa chembechembe hizi za urithi za kurudi husika huweza kusomwa/kutambuliwa na machine.

Hapa ndo ukweli au uongo ulipo.
 
Ninachoweza kusema
Mnadanganywa sana kuhusu haya maswala ya UKIMWI na virusi vyake
Comment zote nlizozisoma asilimia 95 Ni uongo

Elimu ! Elimu !Elimu
Kama jamii forum kwa magreat thinkers uelewa ndo huu huko vijijini na mitaani sijui kukoje

#elimu ya UKIMWI na virusi inahitajika

Kivipi Mkuu
 
America did, America is doing and America will do
 
Na baada ya kupima Kama NI maombi Basi ushuhuda Ni kwamba Mwamposa anaponya hata wenye UKIMWI kumbe kampima alotumia dawa muda mrefu
 
Na baada ya kupima Kama NI maombi Basi ushuhuda Ni kwamba Mwamposa anaponya hata wenye UKIMWI kumbe kampima alotumia dawa muda mrefu
Hii kadhia imempeleka dada yangu mmoja kaburini! ..kaaminishwa kapona kwa maombi.. ..baada ya mwaka vimekuja juu..
 
Back
Top Bottom