Mtu anayetumia ARV kwa muda mrefu virusi huwa havionekani kwenye vipimo vidogo?

Watu mnapenda kudanganyana sana yaani.

By the way muuza duka la dawa wengi hawana taaluma ya maana kuhusu clinical medicine-wengi wao wamefunzwa kugawa tu dawa.

Ila kwa kuwa story za vijiweni ndiyo huwa tamu ,basi na story ziendeleee
 
Ahsante kwa taarifa, mtaangamia kwa kukosa maarifa...
 
Ninachoweza kusema
Mnadanganywa sana kuhusu haya maswala ya UKIMWI na virusi vyake
Comment zote nlizozisoma asilimia 95 Ni uongo

Elimu ! Elimu !Elimu
Kama jamii forum kwa magreat thinkers uelewa ndo huu huko vijijini na mitaani sijui kukoje

#elimu ya UKIMWI na virusi inahitajika
 
Toa Elimu sahihi Sasa tujue lipi ni lipi
 
Habari!

Ili kuelewa haya mambo ni muhimu ukiwa na taarifa sahihi juu ya:

1: HIV virus na maisha yake
2: Ufanyaji kazi wa ARV
3: Ufanyaji kazi wa vipimo vya HIV

1: Kifupi: Virusi vya HIV huweza kuishi na kushambulia CD4 seli peke yake mwilini. Hii hutokana na CD4 seli kuwa na receptors/ milango ambazo hutumika kuingia kwenye seli husika. Kumbuka CD4 pia zina muda wake wa kuishi na kufa.
Hivyo, unaweza kuvifungia ndani ya seli husika au kufanya visishambulie seli mpya za CD4 na seli inapokufa itaondoka na virusi husika. Hapa ndo lilipozaliwa wazo la post exposure prophylaxis(PEP).

2: ARV: Hufanya kazi kwenye maeneo tofauti yanayohusisha: kuzuia HIV virusi asiingie kwenye seli mpya ya CD4 au asiendelee kuzaliana/kujigawanya ndani ya seli za CD4.

Hii huleta matokeo ya HIV kubaki ndani ya seli za CD4 ilizokwisha vamia au asiendelee na kuzaliana ndani ya seli husika.

3: Vipimo vya HIV:
A: Kuna vinavyopima antibodies(ambayo ni mfumo wa kemikali wa mwili unaozalishwa na mwili ili kujikinga au kupambana na kirusi husika). Kiasi cha antibodies hutegemeana na kiasi cha idadi ya virusi husika. Kadri virusi vinavyopungua, antibodies pia hupunguza taratibu. Kipimo kinachopima antibodies pia huweza kutoa majibu kulingana na kiasi cha antibodies. Kama kiasi ni kidogo sana basi reaction ya kuwezesha majibu kuwa chanya haitatoshereza kuleta majibu halisi/positive.

B: Kuna vinavyopima uwepo wa kirusi (DNA vs RNA). Hii huweza kupata majibu chanya kwani uwepo wa chembechembe hizi za urithi za kurudi husika huweza kusomwa/kutambuliwa na machine.

Hapa ndo ukweli au uongo ulipo.
 

Kivipi Mkuu
 
America did, America is doing and America will do
 
Na baada ya kupima Kama NI maombi Basi ushuhuda Ni kwamba Mwamposa anaponya hata wenye UKIMWI kumbe kampima alotumia dawa muda mrefu
 
Na baada ya kupima Kama NI maombi Basi ushuhuda Ni kwamba Mwamposa anaponya hata wenye UKIMWI kumbe kampima alotumia dawa muda mrefu
Hii kadhia imempeleka dada yangu mmoja kaburini! ..kaaminishwa kapona kwa maombi.. ..baada ya mwaka vimekuja juu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…