Mtu anayetumia mashoto au malia kitaamu nini kinasababisha!!!

Mtu anayetumia mashoto au malia kitaamu nini kinasababisha!!!

halafu naskia wanaotumia mashoto huwa ni noma kwa namba

Haahahahah..., unanikumbusha 2[SUP]x[/SUP]=4X, mbona itakuwa balaaa..., Nashukuru sana mkali wangu.
 
Nashukuru sana kaka. umetupa mwanga angalau. sasa kuna mambo mengine kama wakati wa kula, au kusalimiana. ukimwacha kabisa si anaweza akajikuta anatumia mashoto, na hili tunajua watu wengi hawapendi.

Pili mashuleni huwa wanapata tabu sana wanapokuwa wanaandika darasani, hasa ukizingatia wengi wanatumia kulia. sababu wakati wanaandika darasani au wakati wa mitihani huwa wanapinda upande wa kulia na wale wanaoandikia kulia wanapinda kushoto. sasa hii huwa inawaleteaga tabu, wakati mwingine wanadhaniwa kama wanadesa. au kuhisi kwamba anamsumbua jirani yake anayetumia malia.

Kula An kusalimiana hizo ni tabia.. Na tabia hujengwa na mazingira.. Mzoeshe kula na mkono wa kulia kama unapenda, na hiyo iwr pale atakapotumia kijiko pekee au umma pekee (lakini kwa matumizi ya kisu na umma anaruhusiwa kutumia mkono wake wa kushoto), kusalimiana mfundishe pia..
Mimi ni lefthanded, nikiwa mbele ya watu naweza kula kwa mkono wa kulia japo kwa tabu kidogo(nimejifunza kwa kuona watu. - mazingira.) lakini kusalimiana ni automaticcaly kulia, mama alinifunza sana.. So unaweza mfundisha hayo.. Lakini mengine mwachie mkono wake..

Narudia tena hiyo ni zawadi adimu umepewa, you should be proud of yo kid
 
Back
Top Bottom