Nashukuru sana kaka. umetupa mwanga angalau. sasa kuna mambo mengine kama wakati wa kula, au kusalimiana. ukimwacha kabisa si anaweza akajikuta anatumia mashoto, na hili tunajua watu wengi hawapendi.
Pili mashuleni huwa wanapata tabu sana wanapokuwa wanaandika darasani, hasa ukizingatia wengi wanatumia kulia. sababu wakati wanaandika darasani au wakati wa mitihani huwa wanapinda upande wa kulia na wale wanaoandikia kulia wanapinda kushoto. sasa hii huwa inawaleteaga tabu, wakati mwingine wanadhaniwa kama wanadesa. au kuhisi kwamba anamsumbua jirani yake anayetumia malia.