Mtu kama huyu nimchukulie hatua gani kisheria?

Kwamba hujui hatua za kumchukulia! Toa hela watu wampoteze kabisa chini ya Ardhi..
 
nipe mbinu mkuu
Kashakuroga tayari....kwani haujui nyendo zake? Je una ushaidi wa namna ulivyompa iyo pesa? Bati na mbao unaacha kwenda kununua mwenyewe unampa fundi hela yote,we mgeni wa mambo ya ujenzi mkuu...
 
Huna chakufanya kwa sasa wewe fanya plan ufunike hapo juu kama mbao zipo maana fremu zitapinda na jua
 

Unadeka Sana...Yaani Matirio Ya Kwenda Kununua Mwenyewe Unampa Fundi Pesa Nyingi Kiasi Hicho Akakununulie..??Ulimwengu Wa Sasa...​
 
Una potezaea tu , pia ni namna ya kujifunza
Mmh hii ngumu kumeza labda kama una mzigo wa kutosha ndani.

Kuna fundi mmoja alipewa milioni 18 ya kazi kutengeneza vitanda na makabati ya mkongo akapita nayo.

Mwenyewe ni don(fisadi)wa serikalini kapotezea tu.

Fundi katumia pesa zote kamaliza karudi kijiweni hana mbele wala nyuma.
 
makaveli10 mwanetu mwingine wa faida huyu, hakuna kuremba kwenye chetu.

niliwahi mpiga kabali dereva wangu wa bajaji, ali niletea u superstar yeye ana nenepa, mi nakonda mpaka leo akiniona ana piga salute.

Beside hela ya urithi tamu bana 😂😅
 
Usinikumbushe balaa nililolifanya pale kati, tuchekeane kwenye mengine sio kwenye mali zetu.

Naunga mkojo, ahh mkono, hela ya urithi ni tamu 😂
 
Usinikumbushe balaa nililolifanya pale kati, tuchekeane kwenye mengine sio kwenye mali zetu.

Naunga mkojo, ahh mkono, hela ya urithi ni tamu 😂
Unajua kila niki Kumbuka nacheka kishenzi, naona wana vimba akati tuna makali.

Kaka hela ya urithi ni tamu, balaa ikianza kukatika 😂😂
 
Pole sana mkuu, hii Dunia hivi sasa siyo ya kuamini kila mtu, mchukulie hatua za kisheria kwa kumpeleka mahakamani haraka
 
Nenda kwenye vyombo ya kisheria ila ikitokea mahakama imekubali akulipe buku kila baada ya mwezi usishngae ni kutokana na uwezo wake mkuu
Hapa ndio utatamani zile mahakama za mtaani "gachacha" au kwenda kilingeni kupata mawaidha.
 
Mafundi wa Kibongo 95% ni wahuni tu, solution ni kuwapa tenda Wachina tu. Fundi akishakuzoea anakuchukulia kama zoba, I've learnt this the hard way.
 
Malizana naye kihuni, nenda kwenye kampuni ya simu anayo tumia toa kidogo wata mtrack.

kisha wasake wazee wa kazi, wata malizana nae kihuni arudishe hela na hasara..

Halafu unampaje hela ya bati fundi, badala ya kununua mwenyewe?!
Akikujibu nitag mkuu.

Topic zingine Jf ni kama kupeana home work, lakini kiuhalisia mambo yanayoongelewa yanakuwa hayapo.

Mabati 1000 (ya kawaida), mabati 500('msauzi') yanayoweza kupaua nyumba kubwa kubwa 10!

Huyo mtu alikuwa akijenga nini kikubwa namna hiyo bila kutumia contractor wenye mikataba ya kueleweka kisheria na badala yake ampatie fundi kishoka pesa cash badala ya vifaa?

Mi naona hainiingii akilini hii topic
 
Huko uliko ni wapi? Hamna hata panga wala shoka?
Nauliza tu. Nahitaji kununua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…