Singida ndio home
JF-Expert Member
- Feb 23, 2012
- 3,188
- 3,370
Tumekua timu kituko kwa sababu ni kituko kukusanya michango kwenye vikapu vinavyoptishwa pindi mechi inapoendelea.
Binafsi ni mshabiki damu damu wa Timu ya Yanga na wala haitokuja kutokea nimechangia wale wanaozungusa vikapu uwanjani, Unajua Kwanini? Sina imani kabisa na wale wanaozungusha mikapu na huwa nafikiria ni wapigaji tu waliovalia jezi za yanga ili kucheza na ushabiki wetu damu damu kwa manufaa ya matumbo yao.
Licha yah hio style iliyopitwa na wakati ambayo inatuchafua mashabiki wa yanga kuna hii system mpya ya kuchangia kwa M-PESA na Tigo pesa, Huu utaratibu ulipokuja nikajua hapa wametatua kila kitu ila nilivyotaka kuchangia kwa M-PESA nafsi ilisita na sijawai kutuma hata shilingi mia hadi leo, Je wajua Kwanini?
Huu utaratibu haunithamini mchangiaji kwa asilimia 99.9- Hata kwenye kwenye kipindi cha majonzi kama misiba au kwenye kipindi cha furaha kama sherehe kuna daftari la michango linaloonyesha jina la mchangiaji, kiasi cha mchangiaji, tarehe aliyochangia, muda aliochangia, na vidokezo. Hili daftari sio tu kwamba ni kutunza kumbukumbu ila linaonyesha uzito wa umuhimu wa wachangiaji, Ili hata siku chapisho linapobandikwa la wachangiaji basi huwa ni faraja kwa wachangiaji kujiona majina yao yamo katika listi ya watu waliofanikisha shughuli kufanyika.
Sasa hawa wenzetu imekuwa kinyume kabisa, Yani hii michango imekuwa kama unatupia sadaka kwenye msitu mnene, Hakuna ukweli na uwazi kitu kinachonifanya niamini kwamba hii michango huwa haifikii katika kutekeleza malengo ya timu bali kuna majamba wanazitafuna.
Nikiwa kama mwanayanga ambaye hali yangu ya kiuchumi ni ya kawaida sana nipo tayari kuichangia timu yangu hata elfu 10 kila mwezi kwa hiari bila kulazimishwa kwa sababu nina mapenzi ya dhati kabisa na timu yangu ya Yanga, Sifurahii hata kidogo wachezaji wanapodai dai mishahara na wengine kuona ni heri waanze kuuza mchele, sifurahii hata kidogo timu yangu inapokua katika sinto fahamu aidha watakwenda na basi au ndege pindi wanapokuwa na mechi na mbeya city au alliance, sifurahii hata kidogo tunapokwama kusajili wachezaji hodari kwasababu ya ukata wa pesa, na mambo kadha na kadha yanayojitokeza kwa sababu ya ukata wa fedha.
Oneni wenzetu samba, Walikuwa na hali mbaya sana miaka michache iliyopita ila ona sasa muujiza uliotokea, Sio hata muujiza bali ni Nguvu ya pesa na hata sasa mashabiki wao wanajiamini na kujaza uwanja kwa sababu pesa zimeifanya timu iwe imara ukiachana na mchezaji wa 13 ambae ni mashabiki.
PENDEKEZO:
Nikiwa kama mwana yanga mwenye hali ya uchumi ya kawaida mno nawahakikishia mkiyanya haya nitakua tayari kuchangia wekundu wangu kila mwezi na hata zaidi maendeleo yakizidi.
Ni hayo tu niliyonayo kwa viongozi wa yanga, hakuna kitu kinachoshindikana endapo tukitia nia, Nawakumbusheni tu ya kwamba yanga ni timu yenye mamilioni ya wafuasi ambao wanapenda kuiona timu yao ipo juu kwa gharama yoyote ile wanayoweza kuichangia, KAZI KWENU

- Andaeni utaratibu wa kutoa ripoti ya michango ya MPESA NA TIGO PESA kila wiki na mwezi inayoonyesha michango ya mpesa, katika ripoti hii kuwe kuna namba ya muamala, jina la mchangiaji, muda / tarehe aliyochangia, na data za ziada, Kwa kufanya hili binafsi kama mchangiaji ntajua mchangi wangu unathaminiwa, michango ipo wazi, naweza kuhakiki mchango wangu kwa kuangalia tarehe nilituma na muamala, nendeni huko Vodacom na tigo muwaambie mnahitaji hii huduma, kiufupi UKWELI NA UWAZI
- Kuanzishwe huduma za kuwatambua wachangiaji, mfano mtu mwenye juhudi za kuchangia apate jezi au apate tiketi ya bure, n.k
- Kuwe na ripoti za hesabu za mapato na matumizi ili tujue hizi fedha zinatumikaje, Hapa nashauri muajiri wahasibu wanaotambulika na bodi ya wakaguzi na wahasibu wa Tanzania, hawa ndio wale tunaowaita C.P.A, inatupasa tujue tunachochangia kikiongezwa na vyanzo vingine vya mapato kama viinglio hizi hela zinatumikaje, Pia hata madeni (liabilities) inabidi yawekwe wazi tujue kabisa kitu gani kinatukwamisha kupata mzunguko wa fedha uliotulia. Faida za kuweka haya mabo ni nyingi sana kuliko hasara.