Mtu kuficha "last seen info" kwenye Whatsapp... Swali...

Mtu kuficha "last seen info" kwenye Whatsapp... Swali...

Hatupendi tu mambo yetu yalikane. Mimi sio tu nimeficha last seen bali nimeficha hata Status na Profile Picture ambapo kama sijasevu namba yako hivyo vitu huvioni.

hahha kumbe ndo mana nilikuwa sikusomi lol
 
Hii whatsap naona iko popular sana dunia ya tatu. Sijui kwa nini tu.
 
hahaha! kweli besti ila anaekutaftia choko choko hashindwi kukuvizia aone kama upo online maana last seen utaficha ila ukiwa online unaonekana.

online ni muda wote ninakuwa online bestiiiiii......... labda internet ikate.
 
Toa boliti jichoni mwako ndio useme kibanzi cha mwenzio... Unaangaliwa tu

Kibanzi gani mkuu, kila mtu anamfumo wake wa maisha so siwezi kukulazimisha wewe uishi maisha ninayoishi mimi. U can leave your life.
 
Nimepata jibu...

Kumbe watu wengi wanajificha wasijulikane mda gani wapo online kwa kuogopa kuulizwa na wenzi wao.
But kama mtu unakuwa online kwa "nia njema" ukiulizwa si unajibu tu...

hiyo ni mojawapo ya misuse ya last seen......

mahusiano yanapogeuka kila siku ya kuulizana maswali na kujibu maswali , hapo uhuru na furaha hukosekana.
 
kuepusha maswali ya mara kwa mara na lawama zisizonatija.

Kama hufanyi ambayo hutakiwi kufanya sioni kwa nini uone shida kujibu maswali hata yawe ya mara kwa mara.

Na kama hufanyi lolote ambalo hutakiwi kufanya basi sioni kwa nini ulaumiwe pasi na sababu.

Kuficha ficha mambo ni dalili ya utovu wa uaminifu. Hilo hata mtoto mdogo wa miaka miwili analielewa.

Tatizo watu huwa hawataki tu kukubali kuwa sisi binadamu tuko inherently dishonest.
 
hiyo ni mojawapo ya misuse ya last seen......

mahusiano yanapogeuka kila siku ya kuulizana maswali na kujibu maswali , hapo uhuru na furaha hukosekana.

Kama hufanyi lolote baya kwa nini uone tabu kuulizwa maswali na mwenzio? Manake kama kweli hufanyi ambayo hutakiwi kufanya basi hata majibu ya maswali uulizwayo yatakuwa consistent, utayajibu kwa kujiamini, hutakuwa defensive, na hutatafuta lame excuses.

As simple as ABC or 1,2,3.....
 
Back
Top Bottom