Mtu mbinafsi mwenye kujipenda peke yake(narcissist)

Mtu mbinafsi mwenye kujipenda peke yake(narcissist)

Dogoli kinyamkela

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2024
Posts
618
Reaction score
1,440
MTU MBINAFSI MWENYE KUJIPENDA PEKEAKE(NARCISSIST)

Narcissist ni mtu ambaye ana tabia ya kujipenda kupita kiasi na kujiweka mbele ya wengine. Watu hawa mara nyingi wana mawazo ya juu kuhusu nafsi zao, wanahitaji kupewa sifa nyingi, na wanaweza kuwa na shida katika kuelewa hisia za wengine.

Katika saikolojia, narcissism inaweza kuwa na viwango tofauti, na kuna aina mbili kuu: 😷

1. Narcissism ya Kijamii: Hii inahusisha tabia za kujiweka mbele katika mazingira ya kijamii, kama vile kutafuta umaarufu au kutaka kuonekana bora kuliko wengine.😵😵

2. Narcissism ya Kliniki: Hii ni hali ya kiafya ambapo mtu anaweza kuwa na ugonjwa wa narcissistic personality disorder (NPD), ambao unajumuisha sifa kama kutokuwa na huruma, kudharau wengine, na kuwa na hisia za ukuu.

Ni muhimu kuelewa kwamba narcissism inaweza kuathiri mahusiano na watu wengine, kwani watu hawa mara nyingi hawana uwezo wa kuunda uhusiano wa kweli nao😎😎

Kuhusu Narcissus

Nilisoma katika story za Kigiriki,nikajifunza kwamba katika miaka ya nyuma sana kuna Bwana mdogo mmoja aliitwa Narcissus.

Siku moja aliiona taswira(reflection) yake,ndani ya maji ya kwenye kidimbwi.

Alipokwisha kujiona ndani ya yale maji,alikamatwa na kuvutiwa na jinsi alivyomzuri na wa kuvutia watu.😎😎
Aliendelea kujitazama kisha akapoteza uwiano(balance).

Kisha akatumbukia ndani ya hilo dimbwi...🥸

Nakuanza kuteseka kisha kufa maji🥺🥺🥺

Ila mahala pale alipofia palikauka🤪🥵

Nakisha pakaota ua zuri Kama Narcissus🥸

Likaitwa ua Narcissus (Narcissus flower)🤨

Ua hilo lilitambuliwa kua na lakuvutia na harufu nzuri🤬🥸

Lakini lilitengwa kwa kua ni ua lenye sumu kali.

Maana maua mengine yaliyoota kando yake yake yalipata shida katika ukuaji wake.

Yalipata tabu katika mionekano yao.

Mwishowe yalikufa kabisa...🧐😪😫

Kwahio tabia mbaya na isiyovutia wengine,tabia ya kujiona ilipatiwa jina
Narcissist kutokana na huyo bwana mdogo.😪

LEO HII

Tunaweza kua tumevutiwa na watu,hata kutamani kuingia nao katika
Mahusiano🙄
Lakini sio watu sahihi kwetu,hao ni sumu kali kwanini?
Wataua utu wako.
Wataua namna yako ya kujiamini🤐

Brother : kuna mwanamke uko nae kwenye mahusiano,wewe

Umempa hisia na upendo lakini hauoni,wala kuuthamini Bali

Atakachokifanya ni kujitazama yeye,😇😇

Anavaaje,

Anasifiwa vipi na wanaume wengine😯🤐 au anajiona ni jinsi gani wanawake wengine wanamwonea wivu kwa umbo na uzuri wake🤐😪😥

yaani taswira yake inamgandisha fikra zake,hatasogea hatua zozote zaidi ya kufia kwenye hilo dimbwi la kujiona yeye tu🤐😪

Ni mtu,asiyeogopa hata kukujibu,,kwamba anatongozwa na wanaume wengi...
Ili tu kuua ule utu na heshima yako binafsi...

Bro: kuendelea kua na mwanamke wa namna hio,ni kujiangamiza mwenyewe.😪

My SISTER

Kama uko na mwanaume ambaye,fikira zake ni jinsi ambavyo kilo chake kinamdanganya,

Kwamba yeye ni kijana mtanashati(handsome)😫

kwamba anaweza kua na mwanamke amtakaye😜 anapewa sifa nyingi,

AKipost na kujionyesha kwa jamii hana nia nyingine zaidi ya kuonekana yeye ni bora....😫😪

sista kaa mbali na hio kenge itakuua kwa presha..🤐😥

HITIMISHO.
Usiamshe hisia za kujiona ndani yako.
Maana hizo hisia za kujiona,zina rafiki yake anaitwa KIBURI
Huyo akishajitokeza tu,
Ndugu yangu
Anguko lako ujue limefikia tamati.
Ahsante.
#philosophyoflife #foryouシpage #KnowledgeIsPower

Content created by : Dogoli kinyamkela
 
Mmojawapo ni Rais wa Yanga.Anaiendesha Yanga kama kampuni yake binafsi ukipinga unatolewa.Hata kumuajiri msomali mwenzake Moalin kama Mkurugenzi wa Ufundi wa Yanga ni uamuzi wake mwenyewe. Wengine kwenye kamati ya utendaji ni rubber stamp tu.Hakuna anayeweza kupinga jambo.

Hivi Moalin ana utaalamu gani wa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi yaani Bosi wa jopo zima la makocha wa Yanga.?
Hiyo ni nepotism na hakuna anayeweza kufungua mdomo.
 
Tafiti za hivi karibuni zinasema "Narcissism" imeonekana kuwa common sana kwa wanawake wa kizazi cha sasa na ni rahisi sana kuidiagnose character hii kwa mwanamke kuliko mwanaume. Kwa maneno mengine ni kama kusema ukikusanya traffic officers 1,000 na wamafunzi 1,000 wa chuo, je ukitafuta watuhumiwa wa kula rushwa ni kundi lipi una uhakika wa kuwapata wengi?🤔

Mtu akiwa ana describe tabia za narcissist unaweza hisi anamzungumzia mwanamke au binti wa kisasa kwasababu wamezivaa sifa hizi kupita maelezo.

Anyways, Narcissism ni dosari ya kitabia na inaweza kurekebika kama muhusika ataamua kuchukua hatua kuangalia visababishi.

Watu huwa Narcissistic kwasababu mbali mbali ikiwamo malezi, historia mbaya ya kimaisha, kudekezwa sana, kuzaliwa mtoto wa pekee kwa wazazi, na kadhalika.

Kuishi na mtu mwenye character ya narcissist ni kutafuta msongo wa mawazo usio na mwisho sababu atakukausha furaha na utulivu wako wote ili yeye ajiskie vizuri.

Ikitokea umekutana na mtu mwenye hii character amua moja kuhakikisha anakwenda kupata tiba ya kiakili na tabia au kama hatokuwa tayari na kugoma then muachane kabla hajakuacha na trauma kwenye akili yako.
 
haya mambo ya kisaikolojia yapo kijumuishi sana, unaweza dhani kila mtu ni narcissist

hiyo maana ya narcissist ni pana sana, hizo tabia unaweza ziona kwa yeyote
 
Tangu mwaka uanze huu ndo Uzi ulionivutia sana kwa kuwa unaendana na falsafa ya mdogo wangu mmoja anayesemaga

"Wema ni wengi kuliko wabaya ila wabaya wanaonekana mara nyingi kwa kuwa wema wengi ni waoga"
 
Hiyo hali anayo MTU mweusi na hii imepelekea bara la Africa kuwa nyuma Kwa kila kitu.

Kuwaza kuhusu MTU mwingine na kumuwaza Kwa uchanya itakufanya kuwa creative, innovative na visionary ukiniuliza why most of people wame stumble they can't get ahead hilo ndo jibu.

Akili ya kukusanya (accumulation) inabidi kuwa sawa na kuzalisha na kusambaza.
 
ubinafsi unatokana na kulelewa na Mzazi au Mlezi mmoja Mara nyingi hiyo inaleta hathari kwa mtoto kwa sababu anashindwa kupata Combination ya Pande mbili
 
Back
Top Bottom