Mtu mmoja ameuawa na wengine wakijeruhiwa kwa kukatwa mapanga Handeni

Mtu mmoja ameuawa na wengine wakijeruhiwa kwa kukatwa mapanga Handeni

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
1594633936047.png
Mtu mmoja ameuawa huku wengine wanne akiwemo mtoto wakijeruhiwa wilayani Handeni mkoani Tanga baada ya kukatwa mapanga huku wananchi wakijawa na hofu kuhusiana na tukio hilo.

Tukio hilo limetokea katika kitongoji cha Kwamagome kilichopo ndani ya halmashauri ya mji Handeni majira ya saa kumi na mbili jioni, huku Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Blasius Chatanda akithibisha kutokea kwa tukio hilo na kusema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio hilo.

Chanzo: ITV

=========



Akizungumza akiwa hospitali ya wilaya Handeni, baba mzazi wa mmoja wa majeruhi Waziri Mhina amesema tukio hilo limetokea jioni ambapo mtoto wake wa miaka sita Hossein Mhina, amekatwa sehemu ya uso na kuumia vibaya huku akivuja damu nyingi.

Aidha majeruhi wengine katika tukio ni Mwaliko Sadiki amekatwa mkono wa kushoto, Mgaza Waziri mkono wa kulia na Kabelwa Zuberi aliyekatwa maeneo ya tumboni, ambapo wote walifikishwa hospitali ila Yasin Athuman alifariki hapo hapo baada ya kukatwa mkono na mguu.

Mtuhumiwa wa tukio hilo Ramadhani Abdi naye alishambuliwa na wananchi wenye hasira kali na amelazwa hospitali akiwa chini ya ulinzi wa polisi.
 
Back
Top Bottom