Ryzen
JF-Expert Member
- Dec 6, 2012
- 7,301
- 8,706
Tumsifu Yesu Kristu!
Mtu Mmoja Mzee alikuwa akiokota kuni mwituni mtu huyo mzee alionekana kuchoka sana na ugumu wa Maisha.. alilia na kumlaumu sana Mungu kwa ugumu wa Maisha yake, Hata Akatamani Kufa.. Mtu yule akazitupilia mbali kwa hasira Kuni zake alizoshikilia halafu..akapiga ukelele kwa sauti akisema KIFO UKO WAPI? SI UJE UNICHUKUE MATESO HAYA YANIISHIE.. Mara Ghafla likatokea Jitu kama Zimwi..La Kuogofya Likamwuliza Mtu Yule aliyatamani Kufa "CHAGUA KITU KIMOJA AMBACHO UNATAKA NIKUFANYIE" mzee yule kwa sauti ya Taratibu na Unyonge Akamjibu "NAOMBA NIKUSANYIE KUNI ZANGU HIZO"
Hakutaka Kufa tena, Kwa Maana Alikuja Kuona Kifo Kinatisha,Kinaogofya..
Ndugu Zangu Hakuna Mtu anayekipenda Kifo, Wala Kifo Hakizoeleki na Hakitazoeleka, Kifo Kitabaki Kuogopeka siku zote, Kama ilivyoandikwa Kila Nafsi Lazima ionje Mauti..Basi wote lazima tufe..Kwa Maana Hiyo huu wakati Ambao tu hai ni Wakati wetu sisi wa Kujiandaa kiroho kwa Ajili ya Kurudi Nyumbani Mwa Baba yetu..Tukiwa na Tumaini la Ufufuko..!
Tufe tukiwa katika urafiki na Mungu..Basi Pia Ndugu Zangu Tuchukue Nafasi Hii Kuwaombea Ndugu,Jamaa,Marafiki na watu wote wenye uhitaji wa Huruma ya Mungu..Aweze Kuwaangazia Huruma Yake..!