Mtu mwenye akili timamu Maandiko yake ni mafupi

Mama Edina

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2022
Posts
850
Reaction score
2,019
JamiiForums habarini.

Niandike kwa kifupi Sana. Katika somasoma yangu. Nimeona na kutafakari maandiko mbalimbali watu tunayoyaandika, MTU unayeandika maneno meeengi, Kwa kawaida unarudiarudia yaleyale.

Ukiwa unauwezo wa kuandika sentence chache ambazo hazimchukui msomaji dakika moja na nusu, yaani sekunde tisini, na akaelewa maneno na dhumuni lako, aka akapata ujumbe uliokisudiwa basi wewe Upo kwenye kundi la wenye akili timamu.

Screenshot_20230211-090029.jpg

Nakaribisha comment fupi fupi na huu ndio ukweli wenyewe.
 
Sio kweli mama Edina, kuna watu wana content kubwa sana kichwani akichangia mada fulani basi atajikuta data nyingi zinakuja kichwani so atataka kuziweka zote hili kufanya hoja zake kuvutia na kuleta kitu kipya kwenye mada thus why anajikuta anaandika sentensi au paragraph kubwa zaidi.

Lakini hapa cha kuzingatia hili kujua kama huyu mtu ni timamu au vipi angalia hoja zake je zina mashiko!? Kama zina mashiko bila kurudiarudia content huyo ni timamu hapa kidogo ndio nakubaliana na wewe,lakini kama ulivyosema anarudiarudia content basi ujue sio smart sana kichwani.

Hata hapa jukwaani kuna member utakuta kuna swali dogo tu linalohitaji majibu mafupi lakini utaona jinsi anavyokuja na data nyingi kuchangia hiyo mada na ukiangalia kwa umakini point zake nyingi zina mashiko mtu huyu huwezi kumuita hana akili timamu.
 
Anaweza kuandika kwa ufupi akaeleweka bana.
 
Hapana... Kwa sababu wengi hua wana tatizo fulani la kisaikolojia ambalo hufanya iwe huvyo. Kutokana na watanzania hatuna uelewa na sakolojia hasa kwa watoto wetu basi hua tunaenda moja kwa moja kua huyu ni chizi. Mimi ni muhanga wa hiki kitu. Nikiandika kitu ha siwezi kufupisha coz hua naona sieleweki so I have to write a lot of words.

Kichwani hua nina Mambo mengi yamenyooka ila nikifungua mdomo tu maneno yanatoka machache naanza kukosea hivyo inabidi nirudie tena kusoma kitu... Ndio maana mimi siwezi mfundisha mtu akanielewa au kumuhadithia mtu kitu. Ila nikiandika inakua rahisi japo lazima liwe gazeti la 1000 words.

Tatizo linalosababisha ni Dyslexia. Dyslexia ni tatizo ambapo muhusika mwenye tatizo hili anakua inamuwea vigumu kuandika na kusoma ajili kushindwa kutambua sauti za matamshi, Wernickes’s area ni sehemu inayopaktikana kwenye posterior superior temporal lobe ambayo ipo kwenye ubongo wa mbele. Katika eneo hilo ndio kunahusika na kuchakata matamshi kama yameandikwa au yametamkwa, hivyo basi Dyslexia hushambulia eneo hili linalohuika na kuchakata lugha.

Kwakawaida dalili za huu ugonjwa hua ni ngumu kuugundua kabla ya mtoto kuanza shule lakini kuna baadhi ya viashiria ukiviona kwa mtoto basi vitakuashiria kwamba mwanao pindi akifianza shule anaweza kua na tatizo hili. Zifuatazo ni dalili za ugonjwa huu

Kabla ya kuanza shule

Hivi ni viashiaria amabavyo mwanao anaweza kuvionyesha kabla ya kuanza shule ambavyo vitakuashiria kwamba mwanao akianza shule atakua na dyslexia.
Kuchelewa kuanza kuongea
Kujifunza maneno mapya taratibu
Kushindwa kukumbuka kwamba hii ni namba ngapi au herufi gani, kushindwa kutambua rangi
Kushindwa kuunda maneno kwa usahihi pindi anapotamka au kuchanganya maneno ambayo yanafanana katika matamshi

Nitarudi
 
Anaweza kuandika kwa ufupi akaeleweka bana.
Sio rahisi kwa mtu mwenye content kichwani..let say wewe msanii umeanzisha mada umeuliza "kwanini muziki wa bongo hauendelei?" Kuandika tu maneno manne umaskini na ulimbukeni wa wasanii,support ndogo kutoka kwa serikali n.k haiwezi kuprove kwamba aliyejibu hivyo ana akili timamu maana hana mifano dhahiri na huwa haivutii kabisa kwenye mijadala ya kwenye forum labda tu kwa sms za simu

mfano unasema umaskini na ulimbukeni hapa mtu mwenye content ataanza kutrace back kuanzia enzi za kina Mr nice ilikuwaje,aje aelezee kwa data za kutosha mpaka kwa kina Diamond huyu mtu kama hatarudia maneno atakuwa ameprovide kitu kipya kwa watu wa forum tofaut na yule aliyeishia kuongea kwa ufupi tu..na hii ndio maana ya forum discussion
 
JamiiForums habarini.

Niandike kwa kifupi Sana. Katika somasoma yangu. Nimeona na kutafakari maandiko mbalimbali watu tunayoyaandika, MTU unayeandika maneno meeengi, Kwa kawaida unarudiarudia yaleyale.

Ukiwa unauwezo wa kuandika sentence chache ambazo hazimchukui msomaji dakika moja na nusu, yaani sekunde tisini, na akaelewa maneno na dhumuni lako, aka akapata ujumbe uliokisudiwa basi wewe Upo kwenye kundi la wenye akili timamu.

View attachment 2513344

Nakaribisha comment fupi fupi na huu ndio ukweli wenyewe.
Hiki ni aina gani ya kipimo cha utimamu wa akili?
 
Mbuzi ana mkia mfupi unaoelekea juu na kuacha sehemu yote ya siri ionekane wazi na ng'ombe ana mkia mrefu kuelekea chini angalau unafunika sehemu ndogo ya siri, hii yote ni mikia ila afadhali mkia mrefu wa ng'ombe.
 
Ndo nini sasa? Fasihi zingine bwana.
Ebu andika mengi labda utaeleweka hizi fupi fupi huwezi Mkuu.
 
Ina maana terms za mitandao ya kijamii inavyoandikwa kwa urefu unasoma mpaka unachoka, unaamua kukimbilia mwishoni ku agree ni wajinga na wanadharaulika? Hawa wenye kuandika kwa ufupi huwa hawaeleki kiufasaha na ni wavivu kuandika na kusoma
 
Sio rahisi kwa mtu mwenye content kichwani..let say wewe msanii umeanzisha mada umeuliza "kwanini muziki wa bongo hauendelei?" Kuandika tu maneno manne umaskini na ulimbukeni wa wasanii,support ndogo kutoka kwa serikali n.k haiwezi kuprove kwamba aliyejibu hivyo ana akili timamu maana hana mifano dhahiri na huwa haivutii kabisa kwenye mijadala ya kwenye forum labda tu kwa sms za simu

mfano unasema umaskini na ulimbukeni hapa mtu mwenye content ataanza kutrace back kuanzia enzi za kina Mr nice ilikuwaje,aje aelezee kwa data za kutosha mpaka kwa kina Diamond huyu mtu kama hatarudia maneno atakuwa ameprovide kitu kipya kwa watu wa forum tofaut na yule aliyeishia kuongea kwa ufupi tu..na hii ndio maana ya forum discussion
Mkuu ipo hivii
Kubali wanadamu wana uwezo tofauti kwa kila mmoja wao.

Mimi nikiandika jambo napenda kukusogeza kwenye uelewa bila kukuchosha na aya ndeefu.

Fuatilia Bungeni ulinganishe majibu ya Mwigulu na ya Prof Mkenda. Utagundua mtoa hoja hapo juu yupo sahihi
 
Back
Top Bottom