Kuna watu wanajificha kwenye ID zao hapa jf wakidhani hawajulikani.
Kuna mtu mmoja amekaribishwa kwenye timu ya utopolo lakini sasa anataka kuvuka mipaka na kuanza kutamani nafasi ya urais wa timu.
Amewafanya wasemaji wa zamani wa utopolo waonekane wasaliti na kila wakitajwa leo wanatajwa kwa jina la usaliti.Na wafuasi wa utopolo kama tujuavyo akili hawana wakaamini huo ujinga.
Sasa ni zamu yako rais jiandae maana tayari kuna uzi hapa unakuponda na aliyeanzisha kutaka kujikuza.Na huyu jamaa ni nyoka mmemkaribisha ndani mtajuta
Sasa wewe mbona Ndiye unaye weweseka kuliko Yanga wenyewe. Kwanza Kuna kitu hukifahamu Yanga ni nucleus katika Atom inayo itwa Simba, Yaani Yanga ni core (kiini)Cha Simba.
Hakuna kiumbe yoyote anaye weza kutokea nje ya Yanga kuisaliti Yanga.
Yanga ni Kitu kilicho kamilika yaani protons na neutrons na nucleus vyote vinaendana.
Atom ya Yanga iko very strong.
Tofauti iliyopo na Simba kiini Cha Simba (nucleus) ni Yanga Kwaiyo ata Simba wafanye namna gani katika mazingira ya Kawaida au uchawi au elimu ya unajimu kama Yanga watakuwa Serious hawezi kuihujumu au kuishinda Yanga.
Sababu ni ndogo tu ambayo wasio na macho yenye kina wataizarau ni Asili ya Simba, Pan Africa kuwa ni Yanga.
Pan Ilisha ondoka kwenye ushindani.
Yanga inaweza kusalitiwa na Yanga wenyewe tu kama ilivyotokea 1976 Tabu Mangara akaenda kuanzisha Pan Africa,uku Yanga ikifukuza Nyota wake wengi wakijiunga na Pan, wakafungwa na Simba goli 5.
Mwaka 1994 mgogoro wa Mpondela na Gulamali baadhi ya Wana Yanga wakahujumu timu ikafungwa 4 na Simba Yanga ikatimua karibu nyota wake wote wengi wakajiunga na Simba.
Mwaka 2012 Mgogoro wa Royd Nchunga na Wazee wa Yanga, wazee wakamsusia timu Nchunga kwenye Mechi na Simba na kumwambia asubiri aone kinacho fuatia na mechi ilikwisha Kwa Yanga kufungwa 5 Golikipa Yaw Beko Alisha tonywa yatakayo tokea na akajidai kaumia wakati mchezo ukiendelea na kuacha shughuli iliyo kusudiwa iendelee uku Simba akipewa penalty 3 na refa ambaye ni shabiki wa Yanga.
Hii mechi ya mwisho ya 4-0 ya mwisho aliyofungwa Yanga kwenye mashindano ya FA baadhi ya watu wanajua kilichotokea ila Kwa faida na mustakbali ya baadhi ya wachezaji na kiongozi atuta Sema Kwa Sasa.
Ninacho sisitiza ni kuwa Yanga kama Haina mgogoro wa ndani ni ngumu kusalitiwa au kupoteza mechi na Simba kirahisi. Yanga dhidi ya mpinzani wake wa jadi wako imara katika nyanja zote kwakua Asili Ina mpendelea.
Kwasasa Yanga iko macho kuliko macho ya Bundi.