Mtu na maisha

SPYnoCODE

Senior Member
Joined
Jun 3, 2022
Posts
151
Reaction score
273
Ukweli halisi ni kwamba Kila mtu anaiona dunia kwa namna yake,kulingana na akili yake, ama katika kuwaza jinsi maisha yanafananaje kinamna ya yeye !

Nikiwa katika hali ya utulivu mwingi, ndani ya ulimwengu wangu wa kufikiri...

Nilijikuta nikianza kutathmini kwa namna ambavyo binadam wote tunaishi, kwa kujishughulisha na kukutana na mambo mengi ambayo tunayaona ni kama mapya kwetu, na kwa namna yalivyo yakisasa katika ulimwengu wetu

Lakini ukweli ni kwamba yalishafanyika ama kuwepo hapo awali....


Yes! Ni nyakati ambazo hatukuzipitia na wala kumbukumbu zetu hazikuwepo wala hakuna yeyote wa nyakati hizo aliyejua chochote kutuhusu.

Waliishi kwa kujitambua na kufanya mambo ambayo sisi tunayafanya yatokee kwa usasa.

Kitu pekee ninachokiamini kuwa Msingi wa maisha wa binadam yeyote ni AKILI.
Na Katika kuyaishi ni lazima tuanze na Akili katika kuyawaza."

-Hii inatufanya tuwe tunaanza kuunda taswira ya wapi pa kwenda/namna ya kufanya.
Yaani;
"Ukishafikia namna ya kujitambua/utuuzima basi uumbaji wako wa kiAkili hutangulia mbele ya uumbaji wa kimwili.
Ndio ile hatua mtu anafikia anawaza mbele sana kuifikia kesho yake, kisha mwili unaonyesha muitikio/respond.

nayaona maisha yamemfunga mtu kwa mambo 10 ambayo ili kuyaepuka itakubidi ufe kwamaana hayatakuwa na maana tena kwako ndani ya hii sayari
1. PESA - money
2. FAMILIA -family
3. KUMILIKI - possession
4. KAZI - work
5. FURAHA - pleasure
6. RAFIKI - friend
7. ADUI - enemy
8. DINI - religious group
9. BINAFSI - self
10. MWENZI -spouse

Katika vitu vyote hivyo, vinafanya maisha yawe na balance kwa binadam yoyote kwa kiwango chake na namna yake katika kuyaishi.

Mwisho itoshe kusema - Kama kutakuwa na maisha mengine ambayo nitakuwepo nikiwa najitambua hivi yaan hivi live, (kama sasa hivi) ...... sijui yatakuwa na muonekano gani, na sijui tutayaishi kwa namna ipi..
NAYATAMANI ili nijifunze kupitia kwayo. Asante.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…