Mtu ni nini hasa? Ngoja nijibu kufuatana na fundisho/doctrine ya Biblia Takatifu,
Kitabu cha Mwanzo 2:7 (Genesis 2:7) ukisoma "New King James Version" inasema, " And the Lord God formed Man out of the dust of the ground, and breathed the breath of life into his nostrils". Ukisoma Biblia ya Kiswahili inasema " Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akapulizia pumzi ya uhai puani mwake mtu akawa nafsi hai".
Sasa basi, kufuatana na andiko hilo hapo juu, Mtu sio mwili, mtu sio nafsi bali mtu ni roho yenye nafsi inayokaa ndani ya nyumba na nyumba yenyewe inaitwa mwili. Kwa nini tunasema mtu ni roho? kwanza kabisa, mtu akifa, huwa tunasema "huu ni mwili wa marehemu Benard" basi kama huo ni mwili wa marehemu Benard,sasa tujiulize, huyo marehemu Benard yupo wapi hasa? kwa nini tuseme huu ni mwili wa marehemu Benard? Sasa kama ni mwili wake, yeye mwenyewe yupo wapi? imekuwaje auache mwili wake afu sisi tuseme hii ni maiti ya Benard?
Kimsingi, Benard ndio roho yenyewe, Mtu ni roho. Hivyo Mungu ambaye pia YEYE ni roho (Yohana 4:24) alipokuwa akiumba mtu, alifanya hivi, alichukua udongo(mwili), YEYE Mungu, kutoka kwenywe mapafu yake apulizia PUMZI ya UHAI ndani ya pua za udongo na mara mtu akawa nafsi hai. Neno nafsi maana yake ni "UTASHI" au ufahamu/Kujitambua/Kumbukumbu. Kwenye nafsi ndio kuna "MAWAZO", "HISIA", "MAAMUZI", "TABIA" kimsingi nafsi ya mtu imebeba kitu kinaitwa "PERSONALITY". Personality kwa kiswahili ni "UTU". Kwa mfano tabia za mtu zinatokana na amewaza nini, mawazo yake yatapelekea maamuzi, kitendo cha kufanya maamuzi kitadhihirika kwa mtu kufanya matendo kupitia viungo vya mwilini. Kwa mfano, Mtu ambaye ni roho, anaweza akawaza kufanya kitendo kizuri au kibaya, mathalani, mtu anayewaza kuiba au mtu anayewaza kununua shamba. Maamuzi yake yatatokana na Nafsi yake imeamuaje.
Nafsi inakuwa na options (machaguo mawili) ama kuiba au kutokuiba, ama kununua shamba au kutokununua. Maamuzi hayo yanafanyika ndani ya nafsi ya mtu, na mara zote nafsi hufanya hivyo ili mwili uchukue hatua na roho inufaike au ipate hasara. Nafsi ya mtu ikiamua kuiba kwa mfano, faida ni kuwa roho ya mtu itapata kuridhika(satisfaction) lakini endapo asipofanikiwa kuiba roho yake haitaridhika. Kutokuridhika ama kuridhika kutapelekea mtu huyo kuendelea na mchezo wa wizi na hatimaye itakuwa ni TABIA inayokaa ndani ya nafsi kwa kuwa huko ndiko maamuzi yanakofanyika.
Mavumbi ya ardhi (Mwili)+ Pumzi ya uhai (roho+yenye nafsi) kuwa na nafsi ni matokeo ya roho kuingia ndani ya mavumbi ya ardhi (mwili). Nafsi haipo mbaka roho iingie ndani ya mwili, hivyo basi mtu akifa hafi yeye isipokuwa mwili wake ndio unakufa. Uhai ukimtoka mtu, mtu huyo ndio anaitwa Ameaga dunia/amekufa/amefariki. Ukifa maana yake ni kuwa mwili wako umeamua kutengana na roho. Kama mwili ukitengana na roho basi roho+yenye package ya nafsi ndani yake inaondoka.
Kimsingi, roho ya mtu ina umbo la mwili. Ni kama hivi, ukichukua chupa ya maji mfano ile ya Kilimanjaro au ya Uhai, yale maji yanakuwa hayana shape/umbo, hivyo yatachukua shape/umbo la chupa, sasa ndivyo ilivyo kwa roho inapoingia ndani ya mwili. Roho ikiingia mwilini inachukua shape/umbo la mwili. Hivyo roho ikitoka ndani ya mwili inakuwa na umbo la mwili lakini haiwezi kuonekana kwa macho ya nyama(naked eyes) wala kushikika.
Mtu akifa, mwili unazikwa makaburini(utaratibu mzuri wa kibinadamu kutunza mazingira, kwa kuwa uzipozikwa ukaoza utatoa harufu na nchi/mji/mtaa/kijiji pakakuwa hapakaliki, hivyo njia salama ya usafi ni kuufukia ardhini). Ndio maana Biblia katika kitabu cha Mwanzo inasema, "Uu mavumbi wewe na mavumbini utarudi", anayeambiwa hapo sio roho bali ni mwili. Mwili unatokana na udongo(kwa kiebrania na tafsiri ya kingereza wanasema, "humarusman" yaani "udongo" bali roho ikitoka ndani ya mwili ama inaenda Paradiso,(mahali katika ulimwengu wa roho ambapo watakatifu wanasubiria parapanda, hukumu ili wapelekwe mbinguni) au wanapelekwa kuzimu (sehemu katika ulimwengu wa roho ambayo wasiowatatifu/wadhambi hupelekwa kusubiria parapanda/hukumu ili watupwe(roho zao) katika ziwa liwakalo moto) Hapa ukumbuke pia kuwa kuzimu nayo itatupwa motoni. Pia mauti/kifo ambayo nayo ni roho kamili zitatupwa zote katika ziwa liwakalo moto kwa mujibu wa Biblia. Hili nalo ni somo la siku nyingine kuhusu kifo, kifo sio tukio kifo ni roho kamili/mauti ni roho kamili inayotenda kazi, inaweza kumwingia mtu na kuutoa uhai wake nje.
Utajuaje kuwa mtu ni roho? Soma Luka 16:19 ambapo YESU anaelezea, kumbuka hapo hakuwa anasema mfano la hasha alikuwa akizungumzia habari ya jambo lililotokea, akaanza kwa kusema " Palikuwa na mtu mmoja tajiri, aliyevaa nguo za zambarau na kitani safi, na masikini mmoja jina lake Lazaro ambaye alikuwa akisubiri kujishibisha kwa makombo kutoka katika meza ya jule tajiri" Biblia inaendelea kwa kusema, "Ikawa yule masikini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani mwa Ibrahimu, yule tajiri naye akafa, akazikwa, kule kuzimu akayainua macho yake.........." inaendelea hapo. Sasa swali la kujiuliza ni kuwa kama tajiri alikufa, akazikwa, na alionekana kuzimu akiyainua macho yake sasa aliyekufa ni nani na aliyekuzimu ni nani? Jibu ni rahisi kuwa aliyekufa sio tajiri aliyekufa ni mwili wa Tajiri na tajiri mwenyewe ambaye ni roho amekwenda kuzimu, na upande mwingine ni kuwa yule masikini Lazaro yeye mwili wake ulizikwa ndio, ila roho yake ipo Paradiso kule alikopelekwa na malaika mpaka kifuani mwa baba Ibrahimu.(Kumbuka huyu Ibrahimu ndio baba wa imani, ibrahimu baba wa wayahudi wote (christians) na baba wa waarabu wote (Muslims). Ambaye kimsingi naye yupo paradiso, akisubiria kuingia katika mji mpya wa Jerusalemu, mji utakaoshuka toka mbinguni.
Nimalizie kwa kusema hivi, mbingu ipo, roho ikitoka mwilini ndio tunasema umekufa.Na roho yako inautambuzi inaweza kutambua kila kitu kwa kuwa imeambatana na nafsi (mind) ama wengine hupenda kuiita soul. Soul na spirit ni vitu viwili tofauti. Soul(nafsi), Spirit(roho) flesh (mwili). Kikubwa zaidi ni kuhakikisha kuwa unaacha dhambi,unampokea YESU kuwa Bwana na Mokozi wa maisha yako(roho) ili roho yako ambayo ndio wewe ikitoka katika mwili iende paradiso mahali salama na sio kuzima, kwa shetani na malaika zake. Kumpa Yesu maisha ni rahisi, ukiamini kwa moyo na ukakiri kwa kinywa kuwa Yesu alikufa,na siku ya tatu akafufuka, ukatubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, utakuwa umeokoka. Tafuta kanisa linalohubiri habari njema za wokovu, sikiliza neno la Mungu, lielewe, amini ndani ya moyo wako na ukiri kwa kinywa.
Asanteni kwa leo wana JF.