Mtu wa kwanza kunywa pombe

soweto85

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2016
Posts
301
Reaction score
247
Wakuu, nimejaribu ku trace mawazo ya huyu jamaa wa kwanza alipo kunywa pombe akalewa, na bila shaka alipoteza network. Pia nahisi alivyoamka alikua hoi na pia nahisi aliliendeleza siku zilivyozidi.

Sasa najiuliza:

1. Hakuogopa na kuachana nayo ?

2. Au zamani hazikua ngangari kama za sasa ?

3. Au jamaa aliyegundua alikua mbishi dhidi ya mazingira yanayomzunguka?

Naomba mawazo yenu wakuu!!
 
kwa nini umewaza pombe tu? bangi je?,dawa kwa mfano unaweza kuumwa na mdudu, kuumwa tumbo,kuumia na ukaambiwa jani flani ni dawa ilikuwaje mwanzo mpaka ikaja kufahamika ivyo! niliwahi kuwaza hivyo na mengine mengi mengi mengiii
 
kwa nini umewaza pombe tu? bangi je?,dawa kwa mfano unaweza kuumwa na mdudu, kuumwa tumbo,kuumia na ukaambiwa jani flani ni dawa ilikuwaje mwanzo mpaka ikaja kufahamika ivyo! niliwahi kuwaza hivyo na mengine mengi mengi mengiii
shukran mkuu, kwa kuongezea na mengine. pia ni mtiririko unaohitaji tafakari ya undani...!!
 
siku ya kwanza hakujua kama amelewa,may be alidhan amepata homa ya gafla akawa amepoteza kumbukumbuku.hapo hakuwa na wazo hata chembe kwamba alichokunywa ndio kimemfanya awe hvo.hvo baada ya kuwa strong ikawa pengne anaendelea ku2mia hiyo pombe(kwa muda huo tuseme ni kinywaji\chakula) siku za mbele baada ya kutokewa na hali hiyo,akagundua kuwa hali hiyo inatokea kila akila/kunywa hiyo kinywaji.

hayo ni mawazo yangu tu
 
Huyo jamaa aliitwa mlenda fuka aliishi migori zamani kweli
 
Kwani ukinywa pombe unapoteza kumbukumbu?
Na hiyo pombe aliitengenezaje bila kujua kitu anachokitengeneza I mean dhamira yake ilikuwa nini mpaka ikatokea pombe?
 
Kwani ukinywa pombe unapoteza kumbukumbu?
Na hiyo pombe aliitengenezaje bila kujua kitu anachokitengeneza I mean dhamira yake ilikuwa nini mpaka ikatokea pombe?

sio lazima atengeneze,chukulia mfano alikuwa muwindaji na kila siku polini, kiu imembana afu maji hayapo jirani,gafla anaona mti unatoa maji maji kama ile miti ya ulanzi,akaamua kutupia bila kujua kama ni kilevi.so dhamira yake ilikuwa kukata kiu ya maji but kumbe amekunywa kinywaji ambacho baadae amekuja kugundua kimemletea hali fulani mwilini.hapo ndo akaimba dear gambe
 
Mkuu hata ule mti wa ulanzi ukiukata na kunywa majimaji yake muda ule ule hulewi, mpaka yalale yachachuke then ndio yawe na ukakasi wa kilevi. Nothing can be termed alcohol without going fermentation process upo hapo mkuu? Hata hizo spirits, grants, wisky matunda yalichachushwa kwanza ndipo distillation ikafanyika kuvipata.
You haven't yet knocked my head....
 
Pombe kilikuwa kiburudisho ila sisi wa sasa ndo tumeamua kutengeneza Kali zaidi
 
Asilimia kubwa ya wabunifu wa zamani walifanya vitu kimakosa ndipo kukagundukika kitu kipya mfano tuchukulie ugali watu zamani walikuwa wanakula nafaka kwa kutafuna ila siku moja dogo kaona kuliko nitafune pora nipondeponde nibwie tu jumla hapo wakagundua unga siku nyingine dogo kashindwa kubwia unga akaona bora aweke maji ili anywe kwa wingi hapo ukagundulika msukulu au unga uliowekwa maji siku nyingine kwenye baridi kali maji hayanyweki ule uji mbichi haunyweki pia,dogo akaona auweke jikoni upate moto ili anywe ukapatikana uji siku nyingine wazazi wapo shamba dogo kaambiwa apike uji akazidisha unga kupeleka shamba kala fimbo za kutosha lakini walikula kwa shida baadae wakazoea ukatokea ugali huu mfano ndivyo pombe nayo ilivyogunduliwa hawakujua ninini lakini kama ni matunda yalichumwa leo wakala yakabaki yakachachuka kesho walivyokula wakaona mbona yapo hivi ni fikra zangu tu
 
Mimi najua mtu wa kwanza kunywa pombe ni nuhu....
Haujaulizwa Mtu wa Kwanza aliyetajwa kwenye Biblia.... na kama Nuhu alikunywa basi akili za kutengeneza hakuzianzia nje tu baada ya kutoka kwenye Safina it means either aliipakiza ndani ya Safina au nae alikuta watu wa enzi zake walishaigundua na ilikuwa inatumika kama vinjwaji vya kawaida na haikuwa haram
 
huyo jamaa aligundua pombe alikuwa ni alchemist aliyejulikana kama Mohammed ibin raz miaka hiyo na tunavyojua scientists wengi wanapenda kile kinywaji kama kinafungua akili hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…