Mtu wako wa karibu anakwambia nini katika hatua kama hii?

Mtu wako wa karibu anakwambia nini katika hatua kama hii?

Me sio mjuzi; na mimi najifunza tu kama wengine. Nitarudi na jibu lako
yap, nakusubiri mama angu, nashangaa wenzako wananitolea mapovu as if nimewauliza wao,sasa nashangaa sijui ni utahira au kutokujielewa,maana wewe niliekuuliza umenijibu vizuri kabisa
 
Ulimwengu tunaoishi unaongozwa na kanuni. Moja ya kanuni kubwa ni kanuni ya KUPANDA na KUVUNA. Utavuna ulichopanda; na utavuna mema kama ulipanda mema; na ukipanda mabaya basi jiandae kuvuna mabaya. Na katika kupanda mema au mabaya; sio lazima uje uvune kwa mtu yule yule ulikopanda; wakati mwingine utavuna kwa third party; Au usivune wewe wakavuna kizazi chako.

Unfortunately; Wengi wetu hatujali nini tunapanda; bali tunatarajia sana mavuno mema tena hata ambako hatukupanda. Unaishi na mwenzi wako; humjali, unamnyanyasa, kumdhalilisha, unamnenea maneno mabaya etc; then siku ya uhitaji wako unatarajia uvune huruma na loyalty yake; je kwake ulipanda huruma na loyalty?

Huku kwetu most of times mke ukikamatwa unachepuka ni hakuna maelezo talaka 3; la kumnyanyasa me ni kwa ke wachache na wanalimudu hilo effectively. Ila mume kuchepuka eti ni nature; so mke utavumilia tu; ukinyanyaswa; ukipigwa, ukiletewa watoto vumilia tu.You have a face to save to the society; maana utaambiwa mwanamke mjinga huvunja ndoa yake blah blah. Bado wengi wetu ni tegemezi; unawaza ntaanzaje maisha on my own; what about my kids etc. So pamoja na manyanyaso yote bado utaendelea kudumu ndoani. Unfortunately katika manyanyaso haya; wanawake wengi huwa wanaishia kubeba uchungu moyoni. Uchungu ambao unaweza ukawa unamtafuna yeye mwenyewe; mwingine uchungu anamalizia kwa watoto; yani ni mkali kwa watoto na watadundwa hao bila hata kosa la msingi. Wachache huwa wanaomba rehema juu ya waume zao; hadi kufikia hatua ya kuwasamehe; ilhali bado wanawaumiza

Wale wenye uchungu; siku yako ya tabu ndo siku ya yeye kutoa uchungu wake; aisee utasuffer (sio kama unakukomoa; ile mimba ya uchungu ndo inatoka; so vumilia tu). Unfortunately tunaishiaga kulaani tu hawa wanaotoa uchungu wao; bila kujiuliza ndani yao kulipandwa nini. Do you expect anything good to come out of a bitter person? Hata neno la Mungu linasema "Moyo uliochangamka ni dawa nzuri"; so moyo wa mkeo uliojikunja juu yako huo, utakuwa ni ugonjwa kwako. Msamaha ni kwa wachache walio na neema; hawa watakusaidia despite maumivu yote uliyowapa. Uchungu zaidi unakuja pale ambapo mnarudigi kwa wake zenu mkishakuwa total liabilities kwao; either umefulia kabisa au ndo unaumwaaa. Mke lazima uchungu uzidi; lazima akumbuke ulivyomtosa wakati things were ok for you; sasa hivi umebaki kushney karonga ndo unamuona mwema? Umegundua wema wake, ukajuta ndo ukamrudia au umerudi kwa sababu huna option? Thats hurts so so much. Afu msamaha haulazimishwi; it is earned slowly. Make some efforts hadi mkeo ajue huyu kweli amejuta.

Kukosea sawa; ila rejeeni kwa wake zenu wakati hali bado ni shwari. Na wao waexperience "katika raha"; sio wao kila siku ni katika shida tu; raha na wengine eeeeh. "UNAPANDA NINI"?
Kiukweli umesema vema sana, uliyo yasema ni kweli kabisa na ndivo wengi wanavyofanyiwa.


Silazimishi msamaha, lakini kuna njia nyingine ya kurekebisha hilo, zaidi ya kusamehe?

Unadhani ukiutumia wakati wa hali ngumu kujipoza hayo machungu kwa kumdharau mumeo, kumdhihaki na kumkatisha tamaa na kumkomoa ndio itakuwa njia nzuri ya kumfunza na kumaliza machungu ulio nayo?? akiweka chuki zaidi kwasababu ya hayo unayo yafanya unadhani kutakuwa na suluhu tena hapo??

Tatizo linamalizwa kwa kutengeneza tatizo lingine?? au na wewe umeamua kukubaliana naye kwa kuunga mkono ujinga wake kwa njia ya wewe kuanzisha visasi??

Moyo we furaha ni dawa nzuri maandiko ni kweli yamesema, lakini nadhani umesahau kuwa njia pekee ya kurudisha furaha ya moyo ni kusamehe.

Kusamehe sio lazima ila ni lazima kama unania ya kujenga upya uhusiano ulio yumba, ila kama huna lengo hilo basi lipiza visasi na mwisho wa visasi nadhani unauja.
 
Haya chezeni ila msizime taa, watoto hawachezi gizani watajigonga kwenye viti waumie bure
🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣

πŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈ
 
yap, nakusubiri mama angu, nashangaa wenzako wananitolea mapovu as if nimewauliza wao,sasa nashangaa sijui ni utahira au kutokujielewa,maana wewe niliekuuliza umenijibu vizuri kabisa
Kumbe limekukaba eeeh!! Sukumia na maji.
 
Back
Top Bottom