Mtu wako wa karibu anakwambia nini katika hatua kama hii?

Kwani mimi naitafsiri vipi na wewe unaitafsiri vipi? Hebu naomba nifafanulie.
Kwa ufupi tu, mara nyingi nimekuiona ukiitafsiri katika dhana ya 60-40. Yaani mwanaume akusaidie zile home errands kama kupika,kupiga deki,kuosha mazagazaga,kuandaa watoto kwa mitoko,kusafisha bustan n.k halafu hapo hapo huyo huyo mwanaume atekeleze yale majukumu yake makuu kiasili(providing all the basic needs). Yaani sio tu unataka fifty-fifty bali unataka favor kwenye majukumu.
 
Uamuzi upi sasa hebu nisaidie? Siwezi kuchukua uamuzi wowote kwa sababu kwa wakati huo anakuwa hana matatizo hivyo anakuwa hahitaji msaada wangu ila namsubiri siku akipata matatizo na kuhitaji msaada wangu ndipo nitamuomba aende kwa huo mchepuko wake ukampe msaada
Wakati mwanaume anakunyanyasa pengine sababu ya visent vyake na wewe upo tu unavumilia manyanyaso hayo hii inatafsiri kwamba manyanyaso hayo hayana athari zozote kwako na haupaswi kulalamika kwa vyovyote vile. Sababu kama kweli haufurahii kuwa sehemu ya mateso/manyanyaso ni lazima uchukue maamuzi sahihi haraka sana ambayo ni kuachana kabisa na mwanaume huyo pasipo hata kumsubiri sijui mpaka haingie matatizo ya kifedha(ambazo obvious ndio zinazokufanya uvumilie mateso).

Kitendo cha wewe kuvumilia manyanyaso/mateso kwenye mahusiano sababu ya maslahi fulani unayoyapata kinaonesha kuwa mwili na nafsi yako havina thamani yoyote kabisa kulinganisha na hayo maslahi unayoyapata(fedha), hata kama baadae huyo mnyanyasaji wako akiingia matatizoni na wewe kulipiza kwa kumfanyia visanga haiwezi ikakuponya wewe kwa 100% maana akilini mwake atakuwa anajua tu 'huyu mwanamke anajitia kiburi sababu nimefulia, siku mambo yakirudi kwenye right track lazima atakuwa mpole na nitaendelea kumnyanyasa kama kawaida". Kosa/tatizo huwa alitibiwi kwa kufanya kosa, hivyo wewe ukijikuta kwenye situation kama hiyo huna haja ya kumsubiri apate matatizo ndio ulipize unavyojua chukua uamuzi mapema.
 
Mkuu umewahi kumsoma mara ngapi huyu bibie Madame S ??? Believe me humu kuna wanawake wako njema sana sana sana!
Mkuu sio mara kwa mara natembelea humu, huyo Madam S sionagi sana mabandiko yake kama ambavyo nnayaona ya Edelyn na washirika wake ambao nimewa taja kwenye comment yangu moja hapo nyuma. Lakini kwa alivyochangia hii mada kiasi fulani kanibadilisha mtazamo.
 
Tunapwaya wapi? Sema ile siku tumekupiga makombora hadi ukakimbia.[emoji23][emoji23][emoji23].
Tatizo lenu huwa hamkai hadi mjidhihirishe mmeshindwa, mnatafutaga visababu mnakimbia.
Duuh... halafu nyie wabishi kweli sijui ni mashabiki wa MAN U
 
Wacha we!! Ungetumention tu tuone mapema.

Sasa kwa taarifa yako hao ulotutaja hapo ndio wife material haijawahi tokea. Yaani ukitaka kuifaidi ndoa hao ndio wa kuoa.
Umewasahau na manengelo. Heaven Sent Khantwe Mother Confessor Sakayo
Ehee.. wacha weee!! basi kama ni hivyo ngoja nifanye mpango nijivutie mmoja kati yao. Maana naamini mwanaume yeyote anaeweze kuwa handle hao effectively, he has to crown himself as noble man. Soon naanza kuwatembelea pm zao mmoja baada ya mwingine.
 
Ulimwengu tunaoishi unaongozwa na kanuni. Moja ya kanuni kubwa ni kanuni ya KUPANDA na KUVUNA. Utavuna ulichopanda; na utavuna mema kama ulipanda mema; na ukipanda mabaya basi jiandae kuvuna mabaya. Na katika kupanda mema au mabaya; sio lazima uje uvune kwa mtu yule yule ulikopanda; wakati mwingine utavuna kwa third party; Au usivune wewe wakavuna kizazi chako.

Unfortunately; Wengi wetu hatujali nini tunapanda; bali tunatarajia sana mavuno mema tena hata ambako hatukupanda. Unaishi na mwenzi wako; humjali, unamnyanyasa, kumdhalilisha, unamnenea maneno mabaya etc; then siku ya uhitaji wako unatarajia uvune huruma na loyalty yake; je kwake ulipanda huruma na loyalty?

Huku kwetu most of times mke ukikamatwa unachepuka ni hakuna maelezo talaka 3; la kumnyanyasa me ni kwa ke wachache na wanalimudu hilo effectively. Ila mume kuchepuka eti ni nature; so mke utavumilia tu; ukinyanyaswa; ukipigwa, ukiletewa watoto vumilia tu.You have a face to save to the society; maana utaambiwa mwanamke mjinga huvunja ndoa yake blah blah. Bado wengi wetu ni tegemezi; unawaza ntaanzaje maisha on my own; what about my kids etc. So pamoja na manyanyaso yote bado utaendelea kudumu ndoani. Unfortunately katika manyanyaso haya; wanawake wengi huwa wanaishia kubeba uchungu moyoni. Uchungu ambao unaweza ukawa unamtafuna yeye mwenyewe; mwingine uchungu anamalizia kwa watoto; yani ni mkali kwa watoto na watadundwa hao bila hata kosa la msingi. Wachache huwa wanaomba rehema juu ya waume zao; hadi kufikia hatua ya kuwasamehe; ilhali bado wanawaumiza

Wale wenye uchungu; siku yako ya tabu ndo siku ya yeye kutoa uchungu wake; aisee utasuffer (sio kama unakukomoa; ile mimba ya uchungu ndo inatoka; so vumilia tu). Unfortunately tunaishiaga kulaani tu hawa wanaotoa uchungu wao; bila kujiuliza ndani yao kulipandwa nini. Do you expect anything good to come out of a bitter person? Hata neno la Mungu linasema "Moyo uliochangamka ni dawa nzuri"; so moyo wa mkeo uliojikunja juu yako huo, utakuwa ni ugonjwa kwako. Msamaha ni kwa wachache walio na neema; hawa watakusaidia despite maumivu yote uliyowapa. Uchungu zaidi unakuja pale ambapo mnarudigi kwa wake zenu mkishakuwa total liabilities kwao; either umefulia kabisa au ndo unaumwaaa. Mke lazima uchungu uzidi; lazima akumbuke ulivyomtosa wakati things were ok for you; sasa hivi umebaki kushney karonga ndo unamuona mwema? Umegundua wema wake, ukajuta ndo ukamrudia au umerudi kwa sababu huna option? Thats hurts so so much. Afu msamaha haulazimishwi; it is earned slowly. Make some efforts hadi mkeo ajue huyu kweli amejuta.

Kukosea sawa; ila rejeeni kwa wake zenu wakati hali bado ni shwari. Na wao waexperience "katika raha"; sio wao kila siku ni katika shida tu; raha na wengine eeeeh. "UNAPANDA NINI"?
Asante kwa ufafanuzi yakinifu binadada, Nimeelewa sana hasa hapo kwenye kuvuna na kupanda we are all guilty of that at some points in life.

Kwanza kabisa ifahamike kokosea/kukengeuka ndani ya mahusiano inaweza kutokea kwa mtu yeyote yule iwe ni KE au ME, na ninavyoamini mimi na hata wahenga wanasema katika mahusiano/ndoa kila mmoja ni mlinzi wa mwenzake kwa mantiki ya kwamba linapotokea tatizo lolote ambalo chanzo ni mmoja wenu basi wewe ambaye umeona ni tatizo ndio unabeba jukumu la kuhakikisha kuwa tatizo hilo halikui na linaondoka mara moja kwa namna yoyote ile inavyowezekana. Ndio maana huwa tunapokabidhiwa kutoka kwa wazazi tunaambiwa kabisa mbali na kuwa mke/mume lakini huyu pia ni mwanao hivyo mlee.

Changamoto inakuja kwenye kuishi mitazamo/busara tulizoonesha kuzipokea kutoka kwa wazee kama nilivyoelezea hapo juu, je ni wangapi tuna ule moyo/juhudi za` ku deal na wenza wetu pale wanaponesha mabadiliko yasiofaa pasipo kukata tamaa haraka hili kumrudisha kwenye mstari mnyoofu?.. unamuona mwanaume mlevi, sio muaminifu, asiyejari familia na mgomvi umefanya nini hili kumfanya aachane na tabia hizo za ajabu? umekaa nae chini kwa njia ya mazungumzo imeshindikana sasa je, umejaribu kuwashirikisha mashee/wachungaji? wanafamilia au ndugu na jamaa? je umefanya hayo yote na kwa muda gani kama kweli una nia ya kumsaidia mwenza haondokane na tabia mbovu isiyokupendeza? Hii sio kwa mwanamke tu hata kwa mwanume pia(japo kwa mwanaume akipitia hizi njia zote ataonekana ni dhaifu mno).

Ni ukweli ulio wazi tulio wengi hasa kwa kiizazi cha sasa hatuweki efforts kubwa kiasi hicho kwa ajili ya kunusuru mahusiano pale mambo yanapokuwa sio mazuri na hasa ukizangati wewe huna kosa lolote liliofanya mwenzako kafanye madudu. Na hatuoni sababu ya kutumia efforts zote hizo sababu mahusiano tunayachukulia kirahisi rahisi sana na hivyo kutoa mwanya wa tatizo kuwa kubwa zaidi na kadri linavyozidi kuwa kubwa linaleta emotional separation, na kukishatokea tu mtengano wa kihisia chuki/mimba ya uchung lazima iwepo na uchungu/chuki ni mzigo unaokaa kifuani kwa muda mrefu mpaka pale utakapata mahala sahihi pakuutelea, na mahala sahihi penyewe ndio kama hapo yule mbwana anapoingia matatizoni na wewe ndio mtu uliyenaye karibu basi utamuoinesha visanga vya kila namna hili kumfanya ajutie yale yote aliyokuwa anayafanya na kukupa mateso uliyojitahidi kuyavumilia.

Kikubwa ninachokiona mimi kama mwanamke/mwanaume anaona mwenzake ameshapotea kiasi kwamba kwenye ubinadamu hayumo tena, kuliko kuanza kumsubiria huku unamuombea sala mbaya aingie matatizoni hili uyatumie matatizo yake kupata relief ni mara mia ukamuacha mara moja kabla hata hizo sala zako mbaya hazijajibiwa, zaidi ya hapo basi mvumilie na umfariji wakati wa matatizo. Maana hata kama ukishatimiza unachokusudia(kulipiza), baada ya matatizo kuisha kuna uwezekano mkubwa sana akarudi kwenye ile hali yake ya mwanzo ambayo ilikukosesha raha na amani na tena safari hii anaweza kuwa pasua kichwa zaidi sababu hata yeye atakuwa na uchungu uliotokana na namna ulivyokuwa una misbehave wakati yuko kwenye crisis.

Halafu hili suala la kuchepuka...... kuchepuka..... kuchepuka..... kuchepuka...!mbona mnapenda kuligusia sana? vipi mnatuonea wivu nini? the mother nature favors us a lot in this(kidding).
 
Muangalie fulani ana biashara nzuri, yule binti amewajengea wazazi wake nyumba, yule mliyesoma nae ana watoto wawili, kijana yule kawawekea wazazi wake mashine ya kusaga, wewe unakwama wapi? Hayo ndio maneno tunaambiana

🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Kwa ufupi tu, mara nyingi nimekuiona ukiitafsiri katika dhana ya 60-40. Yaani mwanaume akusaidie zile home errands kama kupika,kupiga deki,kuosha mazagazaga,kuandaa watoto kwa mitoko,kusafisha bustan n.k halafu hapo hapo huyo huyo mwanaume atekeleze yale majukumu yake makuu kiasili(providing all the basic needs). Yaani sio tu unataka fifty-fifty bali unataka favor kwenye majukumu.
Nope I've never said something like that mimi siku zote nasemaga kuwa mwanamke anayetakiwa kusaidiwa kazi za ndani ni yule ambaye anaprovide nusu kwa nusu na mume wake

Yaani mume akilipa kodi yeye analipa bili mume akilipa ada yeye ananunua mahitaji ya nyumbani au wale wanawake ambao wao ndo wanahudumia zaidi kuliko waume zao

Yaani yale majukumu ambayo alitakiwa afanye mwanaume kwa kiasi kubwa anayafanya mwanamke sasa wanawake wa aina hiyo ndo wanatakiwa kusaidiwa

Na siyo wale ambao wanahudumiwa na waume zao sasa bad enough ni kwamba hata wanaume wenye wanawake wa aina hiyo niliyoitaja hapo juu nao hawataki kuwasaidia wake zao majukumu yao and that is the problem
 
Wakati mwanaume anakunyanyasa pengine sababu ya visent vyake na wewe upo tu unavumilia manyanyaso hayo hii inatafsiri kwamba manyanyaso hayo hayana athari zozote kwako na haupaswi kulalamika kwa vyovyote vile. Sababu kama kweli haufurahii kuwa sehemu ya mateso/manyanyaso ni lazima uchukue maamuzi sahihi haraka sana ambayo ni kuachana kabisa na mwanaume huyo pasipo hata kumsubiri sijui mpaka haingie matatizo ya kifedha(ambazo obvious ndio zinazokufanya uvumilie mateso).

Kitendo cha wewe kuvumilia manyanyaso/mateso kwenye mahusiano sababu ya maslahi fulani unayoyapata kinaonesha kuwa mwili na nafsi yako havina thamani yoyote kabisa kulinganisha na hayo maslahi unayoyapata(fedha), hata kama baadae huyo mnyanyasaji wako akiingia matatizoni na wewe kulipiza kwa kumfanyia visanga haiwezi ikakuponya wewe kwa 100% maana akilini mwake atakuwa anajua tu 'huyu mwanamke anajitia kiburi sababu nimefulia, siku mambo yakirudi kwenye right track lazima atakuwa mpole na nitaendelea kumnyanyasa kama kawaida". Kosa/tatizo huwa alitibiwi kwa kufanya kosa, hivyo wewe ukijikuta kwenye situation kama hiyo huna haja ya kumsubiri apate matatizo ndio ulipize unavyojua chukua uamuzi mapema.
Yaani wanaume bwana kwahiyo suluhisho la maovu yenu ni wake zenu kuwaacha hivyo hivyo mlivyo ila siyo ninyi kubadilika hivi ni kazi sana wanaume kuacha maovu?
 
Ehee.. wacha weee!! basi kama ni hivyo ngoja nifanye mpango nijivutie mmoja kati yao. Maana naamini mwanaume yeyote anaeweze kuwa handle hao effectively, he has to crown himself as noble man. Soon naanza kuwatembelea pm zao mmoja baada ya mwingine.
Halafu wanawake wa aina yetu ndo wife material kama ulikuwa haujui yaani wanaume ogopeni sana wale wanawake wa kila kitu "ndiyo mume wangu" maana ndo mnaowataka hao
 
Duuh... halafu nyie wabishi kweli sijui ni mashabiki wa MAN U
Hahahaha hapa umenichekesha kwa kweli mimi siyo shabiki wa MAN U na pia siwapendi mashabiki wa MAN U maana wengi ni wabishi kweli halafu wana sifa za kijinga nimesema wengi siyo wote
 
Asante kwa ufafanuzi yakinifu binadada, Nimeelewa sana hasa hapo kwenye kuvuna na kupanda we are all guilty of that at some points in life.

Kwanza kabisa ifahamike kokosea/kukengeuka ndani ya mahusiano inaweza kutokea kwa mtu yeyote yule iwe ni KE au ME, na ninavyoamini mimi na hata wahenga wanasema katika mahusiano/ndoa kila mmoja ni mlinzi wa mwenzake kwa mantiki ya kwamba linapotokea tatizo lolote ambalo chanzo ni mmoja wenu basi wewe ambaye umeona ni tatizo ndio unabeba jukumu la kuhakikisha kuwa tatizo hilo halikui na linaondoka mara moja kwa namna yoyote ile inavyowezekana. Ndio maana huwa tunapokabidhiwa kutoka kwa wazazi tunaambiwa kabisa mbali na kuwa mke/mume lakini huyu pia ni mwanao hivyo mlee.

Changamoto inakuja kwenye kuishi mitazamo/busara tulizoonesha kuzipokea kutoka kwa wazee kama nilivyoelezea hapo juu, je ni wangapi tuna ule moyo/juhudi za` ku deal na wenza wetu pale wanaponesha mabadiliko yasiofaa pasipo kukata tamaa haraka hili kumrudisha kwenye mstari mnyoofu?.. unamuona mwanaume mlevi, sio muaminifu, asiyejari familia na mgomvi umefanya nini hili kumfanya aachane na tabia hizo za ajabu? umekaa nae chini kwa njia ya mazungumzo imeshindikana sasa je, umejaribu kuwashirikisha mashee/wachungaji? wanafamilia au ndugu na jamaa? je umefanya hayo yote na kwa muda gani kama kweli una nia ya kumsaidia mwenza haondokane na tabia mbovu isiyokupendeza? Hii sio kwa mwanamke tu hata kwa mwanume pia(japo kwa mwanaume akipitia hizi njia zote ataonekana ni dhaifu mno).

Ni ukweli ulio wazi tulio wengi hasa kwa kiizazi cha sasa hatuweki efforts kubwa kiasi hicho kwa ajili ya kunusuru mahusiano pale mambo yanapokuwa sio mazuri na hasa ukizangati wewe huna kosa lolote liliofanya mwenzako kafanye madudu. Na hatuoni sababu ya kutumia efforts zote hizo sababu mahusiano tunayachukulia kirahisi rahisi sana na hivyo kutoa mwanya wa tatizo kuwa kubwa zaidi na kadri linavyozidi kuwa kubwa linaleta emotional separation, na kukishatokea tu mtengano wa kihisia chuki/mimba ya uchung lazima iwepo na uchungu/chuki ni mzigo unaokaa kifuani kwa muda mrefu mpaka pale utakapata mahala sahihi pakuutelea, na mahala sahihi penyewe ndio kama hapo yule mbwana anapoingia matatizoni na wewe ndio mtu uliyenaye karibu basi utamuoinesha visanga vya kila namna hili kumfanya ajutie yale yote aliyokuwa anayafanya na kukupa mateso uliyojitahidi kuyavumilia.

Kikubwa ninachokiona mimi kama mwanamke/mwanaume anaona mwenzake ameshapotea kiasi kwamba kwenye ubinadamu hayumo tena, kuliko kuanza kumsubiria huku unamuombea sala mbaya aingie matatizoni hili uyatumie matatizo yake kupata relief ni mara mia ukamuacha mara moja kabla hata hizo sala zako mbaya hazijajibiwa, zaidi ya hapo basi mvumilie na umfariji wakati wa matatizo. Maana hata kama ukishatimiza unachokusudia(kulipiza), baada ya matatizo kuisha kuna uwezekano mkubwa sana akarudi kwenye ile hali yake ya mwanzo ambayo ilikukosesha raha na amani na tena safari hii anaweza kuwa pasua kichwa zaidi sababu hata yeye atakuwa na uchungu uliotokana na namna ulivyokuwa una misbehave wakati yuko kwenye crisis.

Halafu hili suala la kuchepuka...... kuchepuka..... kuchepuka..... kuchepuka...!mbona mnapenda kuligusia sana? vipi mnatuonea wivu nini? the mother nature favors us a lot in this(kidding).
Hilo neno kidding ungelitoa tu maana that is the truth na siyo kwamba tunawaonea wivu ila huko kwa michepuko kuna magonjwa kuna uchawi hili hamlioni kwa sababu mmeweka tamaa mbele wanaume ni viumbe wabinafsi sana laiti kama mngekuwa mnawafikiria na wake zenu msingethubutu hata kuwatongoza hao wanawake wengine huko nje achilia mbali kuwalala
 
Back
Top Bottom