Mtu yeyote kwa manufaa ya umma anaweza kufichua maovu yaliyotendeka kwa Mamlaka

Mtu yeyote kwa manufaa ya umma anaweza kufichua maovu yaliyotendeka kwa Mamlaka

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mwaka 2022 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha sheria ya kuwalinda watoa taarifa (whistleblowers) na mashahidi (witnesses)

Watoa taarifa (Whistleblower) wanabeba jukumu muhimu katika kutengeneza Dunia yenye usawa. Utoaji wa taarifa husaidia kulinda Fedha za Umma, kuchochea Uwazi na Uwajibikaji pamoja na kuimarisha Huduma za Kijamii

Mtu yeyote kwa manufaa ya umma anaweza kufichua maovu yaliyotendeka kwa Mamlaka husika ikiwa mtu huyu anaamini kwamba:
(a) jinai imefanyika au inaelekea kufanyika au inataka kufanyika;
(b) mtu mwingine hajatimiza matakwa ya sheria au yupo katika hatua za kuvunja sheria au anaweza kuvunja sheria inayompa jukumu fulani mtu huyo;
(c) afya na usalama wa mtu au jamii utakuwa hatarini, au ipo hatarini au inaelekea kuwekwa hatarini;
(d) katika taasisi ya umma kumekuwa au kunaelekea kuwepo ubadhirifu, utapanyaji wa mali au matumizi mabaya ya mali ya umma au matumizi mabaya ya madaraka;
(e) mazingira yameharibiwa au yanaelekea kuhairbiwa au yanaharibiwa kwa wakati huo

Bila ulinzi sahihi, Watu wanaotoa taarifa kuhusu kashfa mbalimbali wanaweza kukutana na mashambulizi au Vitisho kwa kusema ukweli ikiwemo kufukuzwa Kazi, kushushwa Vyeo, kufunguliwa Mashtaka na wengine huuawa

Watu wengi kwenye Jamii wanaweza kuogopa kutoa taarifa ikiwa hatari za kuripoti taarifa hizo zinaonekana kuwa kubwa, au ikiwa wanahofia kwamba hawatapewa uzito unaostahili.
 
Back
Top Bottom