Halafu nilitoa wazo la kuwapunguzia usumbufu walipa kodi wenu kuja kupanga foleni kila baada ya miezi 3, kwa ajili ya malipo ya kodi! Mtaanza lini kutumia mfumo kama ule wa wenzenu wa Idara nyingine za Serikali?
Mfano kuna Idara moja ya maji ambayo mimi ni mteja wao! Kila bill inapotoka, wananitumia control number kupitia ujumbe mfupi (sms) kwenye simu yangu, then nalipia!
Ila nyinyi mpaka mlipa kodi aje ofisini kwenu, halafu apange foleni! Ndiyo mumtolee hiyo cotrol number! Hivi inaleta mantiki kweli!! Yaani hela ni ya kwangu, bado mnaninyanyasa!!
Aisee mjitahidi kubadilika. Lakini pia muende na wakati.