BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Hassan Banda anayedaiwa kukutwa na Bangi mwaka 2016, ameiomba Mahakama ya Kisutu imrudishe Mahabusu za Polisi kwa sababu mpaka sasa amewekwa Gerezani bila hukumu kwa kile kinachodaiwa ni "Upelelezi Haujakamilika".
Banda amesema, licha ya Rais Samia kuagiza kufutwa kwa kesi zisizokuwa na msingi, kesi yake imeshafutwa mara 5 lakini amekuwa akifunguliwa mashtaka upya, pia alishaandika barua ya kuingia makubaliano ya 'Plea Bargain' lakini hajapata majibu.
Mahakama imekubaliana na hoja za Banda na kuueleza upande wa Mashtaka kama hautakuwa na jibu la kuridhisha itamwachia huru mtuhumiwa huyo. Kesi itarejea tena Februari 21, 2023.
================
MSHITAKIWA Hassan Banda anayedaiwa kukutwa na bangi, ameiomba mahakama arudishwe katika kituo cha polisi hadi pale upelelezi utakapokamilika, kwa sababu mpaka sasa yuko gerezani kwa kile kinachodaiwa upelelezi haujakamilika.
Aidha, amedai kuwa hivi karibuni, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan alitaka kesi zisizokuwa na msingi zifutwe kwa sababu kesi yake hadi sasa imefutwa mara tano na kufunguliwa upya kwa madai kwamba upelelezi bado.
Banda alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Evodia Kyaruzi, wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa. Wakili wa Serikali, Monica Ndakidemi, alidai kuwa upelelezi haujakamilika.
Alidai kuwa faili bado liko kituo cha polisi na kwamba limerudishwa kwa ajili ya marekebisho ya kiupelelezi, hivyo akaomba tarehe ya kutajwa.
"Kesi yangu ina mwaka wa nane tangu Agosti, 2016 nilipokamatwa. Kila siku majibu ni yale yale ya upande wa mashtaka kuwa upelelezi bado haujakamilika.
"Nimekaa gerezani muda mrefu hadi naumwa mgongo, macho na pumu. Pia niliandika barua ya kuingia makubaliano 'plea bargaining' lakini sijapata. Nimechoka kukaa gerezani, naomba mahakama inirudishe polisi hadi upelelezi utakapokamilika ndiyo niletwe mahakamani," alidai.
Pia alidai kuwa kesi yake imeshafutwa mara tano na kufunguliwa upya kwa mashtaka yale yale huku familia na ndugu wakiwa wanamtegemea, hivyo akaomba aonane na kiongozi wa waendesha mashtaka mahakamani hapa, Grace Mwanga, ili amsaidie.
Baada ya mshtakiwa huyo kudai hayo, Hakimu Kyaruzi alisema hoja zilizotolewa ni za msingi kwa hiyo tarehe ijayo kama upande wa mashtaka hautakuwa na jibu la kuridhisha mahakama itamruhusu aonane na Mwanga.
Akijibu hoja za mshtakiwa, Wakili Ndakidemi alidai kuwa alichokidai ni cha kweli, kwa hiyo atajitahidi kuwasiliana na uongozi wa polisi ili kurudisha faili kesi iendelee.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 21 kwa ajili ya kutajwa na kuangalia hatua za faili zilipofikia.
Inadaiwa kuwa Agosti 25, 2016 mshtakiwa akiwa eneo la Mbezi Kibanda cha Mkaa wilayani Ubungo, alikutwa na bangi.
NIPASHE