Mtumba nchi gani unalipa?

Mtumba nchi gani unalipa?

Elisha

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2011
Posts
381
Reaction score
662
Habari za mchana wapendwa!

Moja kwa moja kwenye mada.

Kwa muda mrefu nimetamani sana kufanya biashara ya kuuza mitumba lakini sijui ni mtumba toka nchi gani unalipa. Naomba kwa yeyote anayefahamu soko la mtumba anijuze nipate kuanza! Nilitamani sana nipate balo la mtumba wa watoto na wanawake grade A!

Swali ni je, mtumba toka nchi gani unabamba? Marekani, Canada, China au Korea?

Bei ya balo moja grade A watoto ni sh ngapi? Duka gani lipo vizuri kwa kuuza mtumba safi siyo mafua?

Ahsanteni!
 
Huwezi kupata zote nzuri, maronyaronya lazima yawepo; ukichanganya na yale yanayochambuliwa na wabongo na kufungwa tena, ndipo tatizo linapoanza. Kuna dada mmoja wa kiarabu huwa nanunua mashati kwake, anashauri kama una hela bora ununue beli la zero, halina gredi, we waambie unataka beli la zero, ingawa inaweza enda mpaka milion 3
 
Kumbe huwa yanafunguliwa na kufungwa tena hapa bongo?
 
Kuna siku nilikuwa nafanya matembezi ya mkoa kwa mkoa, kwa ajili ya kujifunza vitu mbali mbali.

Nilipokuwa kwenye stendi moja ya mabasi; nilimuona kijana mmoja anabegi kubwa mgongoni, huku mikononi ameshika suruale nzuri sana za mtumba jamii ya kadeti.

Akawa anazinyoosha nyoosha ili watu wazione; haikuchukua muda, wale madereva wa mabasi, makonda, na baadhi ya abiria wakamfuata kwa wingi kwa ajili ya kununua. Mbaya zaidi walikuwa wanazigombania, kwa sababu mwingine anapenda achukue rangi fulani, ambayo mwingine alishaipenda.

Na kweli, siku hiyo aliuza.

Nashauri , kama unaweza kwenda kwenye mitumba na kuchagua zile nguo ambazo ziko ‘classic’, na ukazipeleka sehemu zenye mikusanyiko ya watu; utauza.
 
Hivi bado tunavaa mitumba?! Maana last time i checked maduka ya nguo brand new kwasasa ni 90% kuzidi ya mtumba plus za dukani ni cheap zaidi.
Kuna mitumba iko vizuri, hasa upande wa mashati; ukipata shati zuri, linakuwa ni la peke yako, na si sare sare kama ya dukani
 
Kuna siku nilikuwa nafanya matembezi ya mkoa kwa mkoa, kwa ajili ya kujifunza vitu mbali mbali.

Nilipokuwa kwenye stendi moja ya mabasi; nilimuona kijana mmoja anabegi kubwa mgongoni, huku mikononi ameshika suruale nzuri sana za mtumba jamii ya kadeti.

Akawa anazinyoosha nyoosha ili watu wazione; haikuchukua muda, wale madereva wa mabasi, makonda, na baadhi ya abiria wakamfuata kwa wingi kwa ajili ya kununua. Mbaya zaidi walikuwa wanazigombania, kwa sababu mwingine anapenda achukue rangi fulani, ambayo mwingine alishaipenda.

Na kweli, siku hiyo aliuza.

Nashauri , kama unaweza kwenda kwenye mitumba na kuchagua zile nguo ambazo ziko ‘classic’, na ukazipeleka sehemu zenye mikusanyiko ya watu; utauza.
kuna siku nilikuwaga nipo Dar,kuna maeneo nilielekezwa niende wanauza nguo za minada pale Ilala sokoni,nilieenjoi sana na bei zao zipo chini sana,nilikuwa kwenye upande wa mashati bei zao ni chini sana kuuliza uliza nikaambiwa kuna hadi wale majamaa wa boutique/shop zile kubwa wananunua pale kisha wanapeleka kwenye dry cleaner wanazipiga parfume kisha wanazitundika dukani kwao huwezi jua kama ni mtumba umetoka kugombaniwa pale ilala sokoni
 
Kuna mitumba iko vizuri, hasa upande wa mashati; ukipata shati zuri, linakuwa ni la peke yako, na si sare sare kama ya dukani
Kwahiyo unashauri nisichukue balo lilofungwa ambalo hujui kilichomo si ndivyo? Badala yake nikachague toka kwa wafungua mabalo!!?
 
kuna siku nilikuwaga nipo Dar,kuna maeneo nilielekezwa niende wanauza nguo za minada pale Ilala sokoni,nilieenjoi sana na bei zao zipo chini sana,nilikuwa kwenye upande wa mashati bei zao ni chini sana kuuliza uliza nikaambiwa kuna hadi wale majamaa wa boutique/shop zile kubwa wananunua pale kisha wanapeleka kwenye dry cleaner wanazipiga parfume kisha wanazitundika dukani kwao huwezi jua kama ni mtumba umetoka kugombaniwa pale ilala sokoni
Umenipa kitu kipya!!
 
Hyo ni wengi sana ata jamaa yang ana duka mwenge na sinza anachukuaga sana mashati ilala alaf anazipeleka shop kwake hapo bei usije ukagusa.
 
Back
Top Bottom