Mtume Muhammad: Jamii isipotoshwe; Jua huzama katika Chemchemu ya matope Meusi na Mazito

Status
Not open for further replies.
[emoji12] [emoji12]


Yesu alimuuliza Filipo vipi nimwonyeshe Mungu kwa wanafunzi, kitu ambacho hakiwezekani. Unatakiwa umwamini Mungu kwa kuheshimu Viumbe vyake: jua, mwezi, viumbe vyote, na Yesu, aliyeumbwa na Mungu. Yeye amesema katika Yohana 4:24 "Mungu ni Roho....." na Yohana 5:37 "... Sauti yake hamkuisikia wakati wowote, wala Sura yake hamkuiona."

Vipi utaweza kuona roho? Kile walichokiona kilikuwa ni Yesu, sio Mungu. Paulo amesema katika 1 Timotheo 6:16
"Ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uwezo una yeye hata milele. Amina."

Kwa hiyo kile ukionacho si Mungu.

Qurani inasema katika Sura 6:103 "Macho hayamfikii (kumwona), bali yeye anayafikia macho (kuyaona na kuwaona hao wenye macho). Naye ni Mwenye kujua yaliyofichikana na yaliyo dhahiri."
 
Endelea kuzunguka , hakuna mwanasayansi duniani atakae kuamini kuwa yesu aliuambia mti ukauke halafu ukakauka, kwasababu kisayansi haiwezekani mti ukauke kwa maneno ,hapo vip unawaamini wanasayansi kwenye hili la maneno hayakaushi mti?
Zipo sayansi hadi za kuhusiana na Ancient Alliens, UFOs. Pitia huko ujifunze mengi. Pia usiache kusoma kuhusu kitu wanaita Pseudo Science.

Ila hata mie siamini kama Mohammad aliupasua mwenzi akaugawa nusu.
 
Hujui vijiwe ni miratul rasul akawa anasikiliza stori za Wayahudi baadaye anawamwagia misukule wanameza [emoji12] hadi Wayahudi walimuita rainaa [emoji38] [emoji38]
Unaleta story za kwenye kahawa , Paulo kweli tapeli na kakuharibu
 
Zipo sayansi hadi za kuhusiana na Ancient Alliens, UFOs. Pitia huko ujifunze mengi. Pia usiache kusoma kuhusu kitu wanaita Pseudo Science.

Ila hata mie siamini kama Mohammad aliupasua mwenzi akaugawa nusu.
Mambo ya alliens ni porojo ambazo hakuna wa kuthibitisha , kiufupi wanasayansi sio wote wa kuaminika
 
Mtahangaika sana kabla ya kukamuliwa ngama [emoji12] YESU anaongea na nduguze Wayahudi walio mkataa! Tayari umesha chomeka huo utàbiri unahusu maarabu [emoji12] [emoji38] [emoji38] daah [emoji15] [emoji47] mwar

". Hapo kabla, Nabii Yeremia (As) aliwaonya watu juu ya ufisadi uliofanywa katika ufunuo na wale wanaofundisha dini ya Mungu. Anasema:

"Mwasemaje, Sisi tuna akili, na torati ya BWANA tunayo pamoja nasi? Lakini, tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo." Yeremia 8:8

Kwa kile kinachofungamana na ibada za uongo, Nabii Yesu (As) amerudia kutumia onyo lilotolowe na Nabii Isaya (As), lakini watu kwa hakika hawasikii. Anasema:

"Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami, nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu." Mathayo 15:8-9
 
Mambo ya alliens ni porojo ambazo hakuna wa kuthibitisha , kiufupi wanasayansi sio wote wa kuaminika
Shida yenu ni pale mkiona stories za alliens zinakubaliana na maelezo ya Quran. Mnakubaliana nao.
 
muhammad sio mtume wewe [emoji117] View attachment 858246 au hata allah humuamini [emoji47] [emoji12]




JE, YESU (AS) ANATHIBITISHA UFAHAMU WA ROHO MTAKATIFU?


Mungu kwa hekima na Rehema zake zisizo na kikomo, ameshatuma mitume mara kadhaa kusambaza UJUMBE Wake na kuwaita viumbe katika kufanya wema (yaani njia ya AMANI na UTIIFU kwa Mungu Mmoja wa Kweli). Huo Ujumbe unaitwa UISLAMU (kutii matakwa ya Mungu).

Ujumbe huu ulisambazwa kwa mataifa na makabila yote ulimwenguni kwa kufuatia mlolongo wa vizazi ukiwaita wanadamu kutii Matakwa ya Mungu. Hata hivyo, funuo zote za mwanzo zilibadilishwa na kupotoshwa na vizazi vilivyokuja baadaye, na mitume wakapuuzwa na kuteswa. Ufunuo safi wa Mungu umechafuliwa na maruweruwe, ushirikina, kuabudu masanamu na imani za kijinga. Kwa hiyo, dini ya Mungu ilipotezwa na kuingizwa katika mkondo wa ibada mbalimbali za uongo.

Historia ya nyendo za binadamu imekokotwa kati ya nuru na kiza. Mungu, kwa wingi wa Mapenzi na Rehema zake kwa wanadamu hajatuacha kizani tugundue njia ya haki kwa kujaribu na kukosea pekee. Amemtuma mjumbe wake wa mwisho, Mtume Muhammad (SAW) kuwaongoza binadamu katika kipindi kinachojulikana kuwa ni zama za kiza. Ufunuo, (yaani Quran Takatifu kwa kupitia malaika (Gabriel) Jibrilu) alioupokea Muhammad (SAW) unawakilisha chanzo cha msingi cha uongozi, chanzo chenye kukusanya mambo yote na cha maumbile ya dunia nzima. Mwongozo huu Mtakatifu unatoa muhtasari wa maarifa na hakika kuhusu Muumba Muweza, ulimwengu, lengo la kuumbwa kwetu na maisha yetu ya hapa duniani na Ahera. Ufunuo huo utawaongoza wanadamu kuelekea NJIA YA KWELI, WEMA na MAFANIKIO katika maisha haya na ya baadaye.

Kusema kuwa atakuja "mpatanishi /mshauri/ Mwombezi/ Roho wa kweli mwingine akiwa ni "mtume mwingine" kama vile Musa na Yesu (AS) ni sahihi kabisa. Ufahamu wa "Roho Mtakatifu" badala ya "mtume mwingine" umekanwa kikamilifu na Injili ya Yohana.

Ili kufahamu ujumbe wa Yesu (AS) juu ya maudhui hii, unatakiwa uanze na waraka wa kwanza wa (1 Yohana 2:1) Hapa, utamfahamu Yesu (AS) alikuwa ni "Mwombezi halisi", "Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,"

Yesu (AS) aliyekuwa "Mwombezi halisi" ameshatabiri kuja kwa "Mwombezi mwingine". Hata hivyo, ikirejewa Biblia kama ilivyotafsiri hilo neno "Mwombezi" kwa maneno mbalimbali ambayo msomaji anaweza kuyafikia kwa kutegemea nani aliyeandika Biblia, (yaani Msaidizi/ mpatanishi/ mshauri/ mwombezi/ Roho wa kweli/ Roho Mtakatifu).

Neno hilo hilo "Paraclete" linatumiwa katika Injili ya Yohana likiashiria utabiri wa Yesu (AS) kwa kuja kwa "Paraclete mwingine". Anasema: "Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;" (Yohana 14:16) Pia amewaambia wanafunzi wake kuwa huyo "msaidizi" atafundisha kila kitu na atawaletea kila kitu ili wakumbuke. Amesema katika (Yohana 15:26) "Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia."

Utaona katika mistari iliyopo hapo juu kuwa BIBLIA ya (RSV) imetumia neno "Counsellor" na neno hilo hilo limetajwa hapo juu (14:25) kuwa ni "Roho Mtakatifu". Lakini neno hilo hilo limebadilishwa katika (Yohana 15:26) hapo juu na kuwa ni "Roho wa kweli". Tena, katika aya zifuatazo hapa chini, imerejeshwa kwa "Counsellor" lakini utagundua baadaye kuwa neno hilo hilo kwa mara nyingine linarejeshwa kwa "Roho wa kweli" katika (Yohana 16:13).

(Yohana 16:7-8): "Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke; kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu, bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu. Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu." Hili limeshathibitishwa katika Quran pale Mungu alipomnyanyua Yesu (AS) na sio kusulubiwa kama ilivyodaiwa.

Katika aya ya hapo juu, (Yohana 16:7-8), kuja kwa "Counsellor" au "Paraclete" kunategemea kuondoka kwa Yesu (AS). Kando ya hayo, Yesu (AS) hajaashiria kuwa huyu "Mpatanishi" atakuja katika kipindi hiki. Katika (Yohana 16:12-15), Yesu (AS) ameendeleza utabiri wake wa kuja kwa huyu Mpatanishi mwingine aliyemwita kuwa ni "Roho wa kweli". Anasema: "Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahamili hivi sasa. Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hata nena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. Yeye atanitukuza mimi; kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari. Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari."

Aya ya hapo juu inavunja utata ulioundwa na neno Roho Mtakatifu [Holy Ghost] au Roho Mtakatifu [Holy Spirit] uliodaiwa na Wakristo kwa sababu, kwa mujibu wa Biblia katika (Mwanzo 1:2), huyu Roho Mtakatifu ameshakuwepo duniani tangu siku ya kuumbwa dunia. "Huyo-Roho Mtakatifu" vilevile alikuwepo kule mto Jordan wakati Yohana alipombatiza Yesu (AS). Kwa hiyo, vipi Yesu (AS) aseme: "bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu." (Yohana 16:7). Kile alichomaanisha Yesu (AS) ni kuwa "Msaidizi mwingine" au "Mtume mwingine" akiwa kama yeye atakuja kwa sababu kuletwa kwa Roho Mtakatifu kumeshafutiliwa mbali kabisa kwa kuwa huyo Roho Mtakatifu ameshakuwa hapa duniani tangu siku ya kuumbwa.

Zaidi, Roho Mtakatifu na Roho wa kweli hayo ni maneno mawili tofauti na kila moja linajitegemea kikamilifu. Hilo la mwisho limechukuwa kiwakilishi "he" nacho kinamaanisha yeye mwanamume, wakati ambapo ya kwanza (Roho Mtakatifu) inachukuwa kiwakilishi "it" nacho kinamaanisha hicho kitu. Yesu (AS) ametuambia kwa maneno ya sawasawa kuwa Counsellor au Roho wa kweli (paraclete) aliyemtabiri ni Mtu atakayetufundisha vitu vyote.

Viwakilishi vyote vya he vimerejea kwa "Roho wa kweli" jambo linalodhihirisha jinsi ya kiume ili liafikiane na neno "Counsellor" katika (Yohana 16:7). Hilo neno "Counsellor" ni neno kivumishi (descriptive - la kueleza sifa) linalotumika sehemu ya "Roho wa kweli", na kwa kisarufi (kigrama), kiwakilishi lazima kiafikiane kijinsia na jina linalofungamana nalo. Kwa hiyo, aya ya 13 na 15 ya Yohana 16 zinathibitisha kuwa Roho wa kweli si sehemu ya Utatu.[1]

Kando ya hayo, katika (Yohana 16:13) Yesu (AS) ametilia mkazo nukta inayomhusu huyu Roho wa kweli, kuwa ndiye mtume wa pekee atakayefundishwa cha kufanya kutoka kwa Aliye Juu: "Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hata nena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena," Kuwa ni mtume wa pekee (si Mungu wala Roho Mtakatifu), hatokuwa na mamlaka yake mwenyewe, bali atapewa ufunuo kutoka kwa Mungu huko Mbinguni.
Zaidi, utagundua kuwa katika (Yohana 16:14), Yesu (AS) anasema juu ya Roho wa kweli: "Yeye atanitukuza mimi; kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari." Quran, ambayo ni ujumbe wa Muhammad (SAW) umewatukuza wote wawili Yesu (AS) na mama yake Mariamu. Jina Isa [Yesu (AS)] limetajwa katika Quran Takatifu mara tano zaidi ya jina Muhammad. Na ukweli ni kuwa, sura kamili ya 19 ya Quran Takatifu bayana kabisa, imeitwa jina la mama yake Yesu ambaye ni Mariamu (yaani Surat Maryam), imethibitisha kiumbuji (utaalamu wa kueleza) hoja yetu kuwa, kwa hakika, Yesu (AS) ametukuzwa sana.
Kwa kuongezea, Yesu (AS), anasema: "Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia." Hiyo ndio sababu kuwa ujumbe wa Muhammad (SAW) ambao ni Quran Takatifu ni ujumbe uliokamilika, unaojumuisha ujumbe wa Yesu (AS) na ujumbe wote uliotangulia. Kwa hakika, Quran ni kithibitisho cha ujumbe wa Yesu (AS) na wale wote waliokuja kabla yake. Huo ni ujumbe mpana unaokusanya mitazamo yote ya juhudi za wanadamu, sawa ni za kibinafsi, kijamii, kisiasa, kiuchumi au mahusiano ya kimataifa. Unaitwa UISLAMU (dini ya kutii Matakwa ya Mungu Mmoja wa Kweli – Allah) hiyo ni sheria kamili ya maisha, na vilevile ni ujumbe wa dunia nzima ulioelekezwa kwa wanadamu wote unaomwongoza mwanadamu kusuluhisha nafsi yake na Mungu Ujumbe ambao unaweza kuuita, Matakwa ya Mungu, matunda ya Uokovu.
Pia, katika (1 Waraka wa Yohana 4:6) maneno mawili "Roho wa kweli" na "Roho mwovu" yametumika kwa ajili ya mwanadamu. Na, katika MSS, Codex Syriacus ya zamani imegunduliwa mwaka 1812 katika Mlima Sinai na Bibi Agnes S. Lewis na Bibi Bensley, andiko la (Yohana 14:26), linalosomeka: "Paraclete, the Spirit" na sio "Paraclete, the Holy Spirit". Hilo neno "Roho" imerejeshwa na MSS, ya zamani, kwa "Roho wa kweli" katika (Yohana 15:26) ya Biblia za kisasa.
Mwisho, akisi kile alichokisema Mtume Isa - Yesu (AS), katika (Mathayo 21:43): "Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake."
Zingatia kuwa, onyo la Yesu (AS) kwa wayahudi pale walipokuwa waasi kwa kuamini na kuabudu miungu mingine kinyume na Mungu Muweza wa asili katika (Mwanzo 49:10) na Mtume Yakobo (AS) ameonya kuhusu Yuda. Kwa kweli ilikuwa ni kukamilisha utabiri wa awali katika (Kumbukumbu la Torati. 32:21): Mungu anasema: "Wamenitia wivu kwa kisicho cha Mungu; Wamenikasirisha kwa ubatili wao; Nami nitawatia wivu kwa wasio watu, Nami nitawakasirisha kwa taifa lipumbaalo."
Warabu wa kabla ya Uislamu walikuwa wakielezwa na watu wa Magharibi kuwa ni taifa jinga. Mwandishi mmoja amewatolea taswira ya kuwa ni "wanyama wakiwa na ngozi ya mwanadamu", ndipo, pale walipoletewa Uislamu, wakawa ni kiigizo cha wanadamu. Mtume Muhammad (SAW) ameondosha aina zote za kuabudu masanamu na kuhubiri upweke wa Mungu – Muumba. Yeye peke yake ndiye Mungu, Mlezi na Mpaji wa ulimwengu wote Asiye na Mke, Mwenza, Mshirika, Familia, mtoto wala msaidizi. Taifa la Kiarabu kwa ujumla na mtume Muhammad (SAW) kwa kipekee walikuwa ni ukamilisho wa tabiri zote za hapo juu.



[1] Victor Paul Wierwille: "Jesus Christ is not God", American Christian Press, the Way International, New Knoxville, Ohio 45871, p. 143.
 
Usiondoke ubao wetu [emoji53] umetupa jukwaa swafi sana [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji106]

Swali:

Ikiwa dini tatu zote, Uyahudi, Ukristo na Uislamu, zinadai zinatokana kwa Mungu Mmoja na Muumba huyo huyo, kwa nini zitofautiane?

MAJIBU:

Mitume yote, tangu Adamu hadi Muhammad (SAW) waliletwa wakiwa na ujumbe huo huo: utiifu kikamilifu wa binadamu kwa Allah.
utiifu huu kwa Kiarabu unaitwa “Islamu,” pia unamaanisha, amani kati ya Muumba na na viumbe vyake. Kinyume na majina Uyahudi na Ukristo,

jina hili Uislamu limetolewa na Allah, Mwenyewe, kama ilivyotajwa katika Qurani Sura 5:3 "...Leo Nimekukamilishieni Dini yenu, na
kukutimizieni neema Yangu, na Nimekupendeleeni Uislamu uwe Dini yenu....." Si “Uyahudi” wala “Ukristo” unaopatikana katika Biblia au kamusi ya Biblia.

Hakuna Nabii wa Kiisraeli aliyesema neno “Uyahudi.”

Yesu kamwe hajadai kuuanzisha Ukristo na kamwe hajajiita Mkristo.

Neno “Ukristo” limetajwa mara tatu tu katika Agano Jipya mara ya kwanza lilitumiwa na Wapagani na Wayahudi wa Antokia, mnamo mwaka 43 AD., muda mrefu baada ya kuondoka kwa Yesu na kuiacha
dunia hii.

" Soma katika Matendo 11:26 “... Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo Antokia.”

Baadaye, litumiwa na mfalme Agripa wa pili kamweleza Paulo katika Matendo 26:28 "Agripa akamwambia Paulo,

Kwa maneno machache wadhani kunifanya mimi kuwa Mkristo."

Kwa hiyo jina Ukristo, kwanza kabisa lilitolewa na maadui wa Ukristo si marafiki. Na hatimaye lilitumiwa na Petro katika waraka wake wa kumfariji mwenye imani, katika 1 Petro 4:16 "Lakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya..."

Mwislamu wa kwanza duniani si Muhammad (SAW), bali ni Ibrahimu, aliyejisalimisha kikamilifu kwa Allah. Likini Uislamu ukiwa ni njia ya maisha umefunuliwa kwa Mitume mingine iliyomtan
gulia Ibrahimu, kama vile Adamu na Nuhu.

Kwa hiyo, Uislamu ndiyo njia ya maisha ya wanadamu wote.
 

hebu rejea swali la Filipo kwa Yesu [emoji117] View attachment 859845 Filipo anataka anyone nani?=MUNGU! YESU anamjibu ALIYE NIONA MIMI AMEMUONA MUNGU [emoji106] FILIPO ANAMUONA YESU [emoji106] HIVYO ANAYE MUONA FILIPO = NI MUNGU [emoji123] [emoji106]
 
[emoji12] [emoji12] [emoji12]
 

Paulo amesema katika 1 Timotheo 6:16

"Ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uwezo una yeye hata milele. Amina."

YESU ANASEMA :

Yohana 5:37 "Naye Baba aliyenipeleka amenishuhudia. Sauti yake hamkuisikia wakati wo wote, wala sura yake hamkuiona.”
 

Yesu mwenyewe amesema kuwa ametumwa kwa watu wa Israeli tu (Matayo 15:24) "Akajibu, Akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.

" Pia Matayo 1:21 "Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao."

Yesu pia amesema kuwa hakuja kubadilisha ila kukamilisha (Matayo 5:17-18) "Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie."

SWALI:

Lakini katika Marko 16:15 Yesu amesema, "Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe."

MAJIBU:

Hilo linapingana na kile kilichotajwa hapo juu katika matayo 15:24 na Matayo 1:21.

Pili, Marko 16:9-20 zimeondoshwa katika Biblia nyingi.

The New American Standard Bible imekiweka kipande hiki katika mabano na ikaweka maelezo yafuatayo:

"Baadhi ya miswada ya kale mno inaondosha kuanzia aya 9 hadi 20."

Biblia ya The New World Translation of the Holy Scriptures inayotumiwa na Mashahidi wa Yehova inakubali kuwa miswada maalumu ya kale inaongeza maelezo marefu au mafupi baada ya Marko 16:8 lakini baadhi ya miswada hiyo inaondosha aya hizo.

Na Biblia ya The Revised Standard version inachapisha chini ya ukurasa rejeo lifuatalo: "Baadhi ya mamlaka za kale zaidi inakileta hicho kitabu cha Marko na kukifunga mwishoni mwa aya ya 8..."

Hili linamaanisha kuwa ufufuo si kweli, kama ulivyoelezwa katika Marko 16:9.

SWALI:

Lakini Yesu amesema katika Matayo 28:19: "Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la
Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu."



MAJIBU

"Mataifa yote" lazima ifafanuliwe kuwa ni yale makabila kumi na mbili ya Israeli, vinginevyo itapingana na Matayo 15:25 na Matayo 1:21.

Katika Biblia ya The New American Standard Bible na ya The New World Translation of the Holy Scriptures, kifungu hicho hakitafsiriwi kuwa, ni "all nations – mataifa yote" lakini kinatafsiriwa "all the nations, - yale mataifa yote," inayomaanisha yale mataifa (makabila) kumi na mbili ya Israeli.
 
Mambo ya alliens ni porojo ambazo hakuna wa kuthibitisha , kiufupi wanasayansi sio wote wa kuaminika


NIMEWAMWAGIA UPUPU ; ILIYOBAKI TUSUBIRI UZI KUFUNGWA, JECHA STYLE , KAMA ULE UZI WA "WAKRISTO WAMEKOSEA " ULIOFUNGWA😀😀

KAZI KWAO KUSUKA AU KUNYOA
 
Kitman. tawriya na Taqiyyah. Umeungaunga vizuri kwenye kuelezea Dhehebu Jipya la Uislamu. Ila haujaweza kuweka sawa Kuhusu Roho Mtakatifu ni nani hasa?.na hii inaweza kua inachangiwa na kukosa Elimu ya Roho.


Let Suppose Roho wa kweli ni Mohammad.
Angalia alichokisema hapa uone jinsi Roho Mohammad alivyoeleza.


The Quran 10:47 says,
And for every people there is a Messenger.

[emoji115] [emoji115] Hizo ayah hapo juu alizoshushiwa Roho Muhammad, anasema wazi kua Kila Taifa wanaye Mesenja wake. Ikiwa na maana mayahudi wana Wa kwao. Waarabu wana Mohammad, wachina wana Budha wao, wahindi wana Gurus nk. Wakristo wanaye Yesu wao. Waafrika sisi ni Watumwa(Property) wa Waarabu.


Quran 14: 4 says,
And WE have not sent any Messenger except with *revelation in the language* of his people in order that he might make things clear to them.

Quran 26: 198-199

And if WE had sent it down to one of the NON-Arabs, and he had read it to them, they would never have believed in it

[emoji115] [emoji115]
Hizo ayah hapo zinaeleza bila kumung'unya kua Hilo Taifa Ni lazima Lugha iwe yao. Yaani kila mesenja ni Lazima awe wa lugha ya wazawa na sio Lugha Ngeni. Waarabu-kiarabu na Wayahudi-kihebrania. Nk. Allah knows best.


Abu Hurayrah (RadiyAllahu Anhu) relates that Rasulullah (Sallallahu Alayhi Wasallam) said: _‘The Jews were divided into 71 or 72 sects as were the Christians. *MY UMMAH will be divided into 73 sects.”*_ (Al-Mustadrak).

[emoji115] [emoji115]
Hii hapa inaonyesha kutambua kua Wakristo na wayahudi watabaki kua sehemu ya unabii wake wakati akiwagawa na waislamu katika madhehebu 73 na kuchagua dhehebu moja la kwenda kukaa paradiso. Mengine yatakua kampani ya moto.


Quran 2:85 says
Do you, then, believe in some parts of the divine writ and deny the truth of other parts? What, then, could be the reward of those among you who do such things but ignominy in the life of this world and, on the Day of Resurrection, they will be consigned to most grievous suffering? For God is not unmindful of what you do.”_
[emoji115] [emoji115]
Hapa kurani inawataka waarabu wanaozunguka eneo la Mecca waamini kila kitu wasiache chochote kwenye huu wahyi walioshushiwa. Na watakao chagua cha kuamini katika kurani atawatesa vibaya sana duniani na siku ya kiama.
 
Makabila hayo 12 yalisha disolve Wakati ule wa utawala wa Roman empire. Kukawa na wasamaria walioitwa Mbwa na Wayahudi. Hata dini ya Uyahudi ilitokana na jina la kabila moja la Yuda.
 
Tatizo la Mtume Mohammad ni kwamba alikuwa mtu wa matukio ya kishetani sana, simuamini kama nisivyo waamini kina Gwajima na TB Joshua na the likes. Wote wasanii wanaoficha maovu yao kupitia jina la Mungu.
Pole ndugu yangu mbishi, TB Joshua ni mtumishi wa Mungu Niko Ambaye Niko.
Ila ni mwanadamu kama mimi na wewe na sio mkamilifu, na ana madhaifu yake kama mwanadamu.
Mkamilifu ni Mungu peke yake aliyekuja kwetu kwa jina la Yesu Kristo.
Naomba angalia Emmanuel TV kwa upendo wote utaamini ninachokisema.
TB Joshua anafanya kazi nyingi tulizo agizwa na Mchungaji wetu Yesu Kristo.
Naomba usimfananishe na binadamu mwingine yeyote. Gwajima ni Gwajima na Mbishi ni Mbishi.
Mbishi hawezi kuwa Gwajima, Wakristo ni lazima tutiane moyo na kulindana tunapofanya kazi ya Mungu.
Kazi ya Mungu ni ngumu na ni rahisi kama sote tutakuwa pamoja katika kuikamilisha. Pole sana ndugu yangu mbishi kwa kukukwaza.
 
Shida yenu ni pale mkiona stories za alliens zinakubaliana na maelezo ya Quran. Mnakubaliana nao.
unatusemea au unatulazimisha? mambo ya alliens ni porojo tupu hakuna kitu kama hicho wala hakuna mwanasayansi anaeweza kuthibitisha
 
Makabila hayo 12 yalisha disolve Wakati ule wa utawala wa Roman empire. Kukawa na wasamaria walioitwa Mbwa na Wayahudi. Hata dini ya Uyahudi ilitokana na jina la kabila moja la Yuda.
Ebu acha uhuni basi kwenye maandiko ya Mungu , waisrael wapo mda wote mpaka kiama
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…