Mtumishi wa mchongo akamatwa Kanisa Katoliki Arusha, ni baada ya kutapeli zaidi ya laki 6

Mtumishi wa mchongo akamatwa Kanisa Katoliki Arusha, ni baada ya kutapeli zaidi ya laki 6

Cute Wife

Platinum Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
3,054
Reaction score
8,449
Wakuu,

Jamaa huyu aliyetambulika kwa jina la Yusufu amedakwa huko Arusha baada ya kutambulika kuwa ni tapeli katika kanisa katoliki Kijenge, Arusha. Wananchi wanasema alikuja na akapewa nafasi hapo kanisani lakini kumbe alikuwa mtumishi wa mchongo.

Huyu mtumishi amekuwa akitoa elimu ya athari ya mionzi kwenye simu pamoja na TV na kuwauzia vifaa (vidude) ambavyo kwa maneno yake ni kuwa vinazuia mionzi hiyo na kuwafanya wabaki salama, na kwamba wasiponunua kifaa hicho karibuni serikali itakipandisha bei kifaa hicho na kufikia elf 20,000 :BearLaugh: :BearLaugh: :BearLaugh:

Mpaka anashtukiwa na kuja kukamatwa na polisi jamaa alikuwa ameshatapeli zaidi ya laki 6! Jamaa huyu amekuwa akienda kufanya utapeli katika makanisa na misikiti mkoani humo ambapo akifikia msikitini anajitambulisha kwa jina la Yusufu na kanisani kutambulika kama Dickson.

Mara kwanza akajitambulisha kama mtumishi na baada ya kudakwa akasema yeye ni mjasiriamali kama wengine wanaotembeza na kuuza bidha mbalimbali.

Ila TZ kuingiza watu mjini ni rahisi sana. Njoo na ujanja wako wa utaondoka na kijiji.


 
Nikiskia matapeli wameshikiliwa hua naumia sana 😭 hawa matapeli hua wanawachangamsha wapumbavu sasa kuwashikilia ni kuzidi kufanya watu waendelee kulala, imagine mtu anapambana na kazi ili apate pesa za kwenda kutoa sadaka kwa manabii afu maisha yake binafsi yanazidi kudidimia huku nabii akila bata 😂
 
Bora huyo kuna nabii anawauzia watu udogo na mafuta ya mizeituni na fruto kinyume na bei ya hizo bidhaa na bado hakamatwi🤔
 
Wakuu,

Jamaa huyu aliyetambulika kwa jina la Yusufu amedakwa huko Arusha baada ya kutambulika kuwa ni tapeli katika kanisa katoliki Kijenge, Arusha. Wananchi wanasema alikuja na akapewa nafasi hapo kanisani lakini kumbe alikuwa mtumishi wa mchongo.

Huyu mtumishi amekuwa akitoa elimu ya athari ya mionzi kwenye simu pamoja na TV na kuwauzia vifaa (vidude) ambavyo kwa maneno yake ni kuwa vinazuia mionzi hiyo na kuwafanya wabaki salama, na kwamba wasiponunua kifaa hicho karibuni serikali itakipandisha bei kifaa hicho na kufikia elf 20,000 :BearLaugh: :BearLaugh: :BearLaugh:

Mpaka anashtukiwa na kuja kukamatwa na polisi jamaa alikuwa ameshatapeli zaidi ya laki 6!

Ila TZ kuingiza watu mjini ni rahisi sana. Njoo na ujanja wako wa utaondoka na kijiji.

Ila watu wana courage, anadiriki kudanganya kwamba kuna mama alizima moto wa gas kwa fire extinguisher ya gari!!
 
Wafuasi wake ngoja waje wakupopoe,wazee wa kuua mijusi!!
Huwa humu hawaji wanajua kabisa hakuna vilaza humu ila ukiwakuta kwenye mitandao mingine ya Facebook na nk wanaweza kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom