Wakuu,
Jamaa huyu aliyetambulika kwa jina la Yusufu amedakwa huko Arusha baada ya kutambulika kuwa ni tapeli katika kanisa katoliki Kijenge, Arusha. Wananchi wanasema alikuja na akapewa nafasi hapo kanisani lakini kumbe alikuwa mtumishi wa mchongo.
Huyu mtumishi amekuwa akitoa elimu ya athari ya mionzi kwenye simu pamoja na TV na kuwauzia vifaa (vidude) ambavyo kwa maneno yake ni kuwa vinazuia mionzi hiyo na kuwafanya wabaki salama, na kwamba wasiponunua kifaa hicho karibuni serikali itakipandisha bei kifaa hicho na kufikia elf 20,000
Mpaka anashtukiwa na kuja kukamatwa na polisi jamaa alikuwa ameshatapeli zaidi ya laki 6!
Ila TZ kuingiza watu mjini ni rahisi sana. Njoo na ujanja wako wa utaondoka na kijiji.