eliakeem
JF-Expert Member
- May 29, 2009
- 17,214
- 15,853
Kwanza niwapongeze kwa shughuli za ujenzi wa Taifa. Nipende tu kuwakumbusha ya kuwa Nchi yetu sasa inaanza kukomaa na kuwa pevu. Nasema hivyo kwa sababu miaka yote tumekuwa tukishuhudia wastaafu ambao walikuwa wamezaliwa kipindi cha ukoloni. Yaani kabla ya uhuru wa Tanganyika.
Lakini sasa mwaka huu na kuendelea tutashuhudia wastaafu ambao wamezaliwa ndani ya kipindi cha uhuru. Heko baba wa Taifa na wengine wengi waliopigania na kuhangaikia uhuru mpaka kupatikana. Sasa matunda tumeyaona. Sasa wameanza kuwa watu wazima na hata wanazeeka.😀😀😀
Hivyo tunaanza kupata wahenga waliozaliwa kipindi cha uhuru. Tunaomba nao wawe na hekima na busara ili kuendelea kutupa misemo yenye kufundisha jamii, kama vile wahenga waliozaliwa kabla ya uhuru walivyotuachia hazina kubwa ya misemo. Mfano mimi binafsi napenda sana ule msemo "Asiye sikia la mkuu ..."
Mwisho niwatakie siku njema na pia kuendelea kupokea wahenga wapya. Yaani wastaafu waliozaliwa kipindi cha uhuru.
Uhuru hoyee!