Responded MTUWASA: Mahitaji ya maji Manispaa ya Mtwara Mikindani ni makubwa kuliko uzalishaji ambao ni 63%

Responded MTUWASA: Mahitaji ya maji Manispaa ya Mtwara Mikindani ni makubwa kuliko uzalishaji ambao ni 63%

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mtwara (MTUWASA) inapenda kutoa ufafanuzi juu ya taarifa iliyochapishwa kupitia ukurasa wa Jamii Forums tarehe 09/01/2026 kuhusu hali ya upatakanaji wa maji katika maeneo ya Cocobeach, Ligula na Shangani.

Pia soma ~ Mamlaka ya Maji Mtwara hukata maji mchana na kuyafungulia usiku wa manane

Mahitaji ya maji eneo la Manispaa ya Mtwara Mikindani yamekuwa makubwa ukilinganisha uzalishaji halisi ambao ni asilimia 63% ya mahitaji. Hii hupelekea uwepo wa mgao wa maji baadhi ya maeneo ya ikiwemo Cocobeach, Ligula na Shangani. Wakati wa utekelezaji wa ratiba ya mgao wa maji yapo baadhi ya maeneo ambayo huchelewa kupata maji kutokana na uchakavu wa miundombinu, hivyo kusababisha kuchelewa kufika kwa maji katika maeneo husika.

Kutokana na changamoto hiyo, Serikali kupitia Wizara ya Maji imeipatia Mamlaka Mradi wa Maboresho ya Miundombinu ya maji Mtwara mjini wenye thamani ya shilingi bilioni 29 ukiwa na lengo la kuhakikisha hali ya upatikanaji wa maji Mtwara mjini unatengemaa.

MTUWASA inawahakikishia wananchi wa Mtwara Mjini wanaofaidika na huduma ya Majisafi na Salama, kuwa inaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ili kuhakikisha hali ya upatikanaji wa majisafi na salma inaimarika ,pia Mamlaka imejizatiti katika usimamizi wa Miradi hiyo ili ikamilike na kunufaisha jamii kama ilivyokusudiwa.
 
Mahitaji ni kiasi gani (L/day) na wanzalisha kiasi gani?
 
Maji yenyewe yanatoka machafu na chumvi nyingi.
 
Amani ni muhimu zaidi kunyweni na muoge amani
 
Back
Top Bottom