MTV waandaa collabo ya Ne-Yo na Diamond Platnumz, this is epic!

mbaruck;13<script id="gpt-impl-0.7006173295437439" src="http://partner.googleadservices.com/gpt/pubads_impl_69r.js"></script>725409 said:
Huwa sipendi ligi yaishe!!Utakuja kuniambia mwenyewe yani kushirikisha wasanii wa nje c o la kupinga hilo

ukweli ni huu...Dimond alichomzidi Kiba ni pesa tu na siyo uwezo wa kuimba....mfuate mtu yyte anayejua muzik then muulize hii kitu...na ndo maana hata sauti za busara akaitwa Kiba coz ni tamasha la kimataifa na kujitingisha tingisha pale jukwaa siyo credit,credit n kucheza na sauti la pili SAUTI SOUUUUL....unadhan hawakumuona Dimond had wamshirikishe Kiba?...kingine Dunia sasa ndo inaenda kujua kwamba waLimuona Mrisho Ngasa(dimond) wakajua ndo bonge la player kumbe kuna MBWANA SAMATA(kiba) alikuwa mapumzikoni hahahaaaaa kiba hapana aysee,anakuja pia na fally ipupa,lakin pia davido kaomba na wote mliona lakin hiyo na Christian Bella je?...acheni nynyiiii atauza machungwa Dimond yuleee haya tu
 


Nakusikitikia sana na pia nakushangaa kwa kujitoa ufahamu ndugu yangu,ukirudia kuisoma post yako uku ukiitafakari kwa kufanya deep comparative analysis between the two utaelewa nnachomaanisha!
 

kumbe upo kishabiki zaidi!! hizo pesa mond kazipataje ka c o huo mziki!!kipaji na kujua kuimba bila ubunifu na kujituma ni sawa na zero tu!! yan me naona tangu kiba kuja mond ndo kazidi kukaza!!alikosa ktma akapata mtv!!watu wanasubiri sana mond ashuke ila kila cku jamaa anazidi kupanda chart!!kiba namkubal lakin mond me namkubal zaid coz anajituma zaid na kuzitumia fursa anazozipata, anajua mashabiki wanataka nin japo unasema hajui kuimba
 
Nakusikitikia sana na pia nakushangaa kwa kujitoa ufahamu ndugu yangu,ukirudia kuisoma post yako uku ukiitafakari kwa kufanya deep comparative analysis between the two utaelewa nnachomaanisha!

unalia nini?..toa hoja dadangu tuongee kwa fact binti yangu.
 
[QUO

kwa hiyo hiko ndo kigezo chako cha kutaka kutuaminisha neyo hajaimba na kiba?...na je ikitoka ngoma ambayo wapo wote TUKUFANYE NINI?
 
Akasikilize na tiffa uko hatutaki ndio mambo gani nyimbo zinakua hit alaf anakuja kuzifanyia remix zinakua za chama
 
Wapo watayarishaji wengi na wazuri wa muziki nchini Tanzania, lakini Sheddy Clever wa Burn Records ndiye aliyebahatika kuchaguliwa na Diamond Platnumz kwenda Nairobi kusimamia zoezi zima la kurekodi collabo ya kimataifa ya Diamond na Ne-Yo kutoka Marekani.

Bongo5 imemtafuta mtayarishaji huyo wa &#8216;Number One' na &#8216;Ntampata Wapi' zote za Diamond, ambaye ametueleza jinsi alivyojikuta akitimiza ndoto ambayo hakuwahi hata kuiota, ya sio tu kukutana bali kumrekodi mshindi wa tuzo za Grammy Ne-Yo kwenye beat aliyoitengeneza.

"Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwasababu yeye ndiye muweza wa yote, pili naushukuru uongozi wa WCB kwasababu wao ndio wamefanikisha haya yote. Kwakweli nimejisikia furaha sana kwasababu sikutegemea kama nitakuja kufanya kazi hii." Alisema Sheddy.

Sheddy alianza kwa kuelezea jinsi ilivyokuwa mara ya kwanza anapigiwa simu na Diamond kupewa dili hiyo;

"Mi nimepigiwa tu simu na Diamond akaniambia kuna kazi inatakiwa ifanyike kwahiyo tunatakiwa kusafiri, nikamwambia poa nashukuru, na akaniambia kila kitu tiketi yako ipo jiandae kwa safari&#8230; basi tukasafiri tukaenda tukafanya hiyo kazi&#8230;nashukuru Mwenyezi Mungu. Ni kazi nzuri na naimani itafika mbali."

Katika wimbo huo wa Diamond aliomshirikisha Ne-Yo, yeye Sheddy Clever amehusika kwa kiasi gani?

"Nimetengeneza beat, na vocal za Diamond kila kitu yaani nimeutengeneza wimbo kwa ujumla, Ne-Yo yeye tulimfata kule kwaajili ya kuweka vocal zake, Beat tulitengeneza pale studio (Nairobi), studio ile Diamond alilipia kwahiyo nilikabidhiwa studio kila kitu, ila kulikuwa na producer wake na Ne-Yo ni mzungu pia ndiye ambaye tulikua tunashauriana naye kubadilishana mawazo na nikajifunza vitu vingi zaidi."

Tupe uzoefu wako wa wakati unamrekodi Ne-Yo akiwa booth, ni msanii wa namna gani?

"Ne-Yo kwanza ni mtu mmoja amabye yuko peace sana tofauti na nilivyokuwa namfikiria, japokuwa nilikuwa na uwoga pia nikasema hivi ntamwambia nini hivi akikosea ntaweza kumrekebisha kweli? Lakini Ne-Yo anapenda pia kurekebishwa anapokosea, na anapenda pia ushauri sana kila anachokifanya anauliza niko poa? Vitu kama hivyo."

Ilimchukua muda gani Ne-Yo kurekodi sauti?

"Kwa upande wake hatukusumbuana sana nafikiri tulipiga kama take mbili tu akamaliza kurekodi kwasababu ana uzoefu wa siku nyingi."

Ne-Yo anazifahamu kazi ambazo umetengeneza zikiwemo za Diamond?
"Yeah Diamond alimwonesha kazi zote ambazo nimefanya na anapenda sana wimbo wa Number One."

Sheddy ambaye pia anawania tuzo ya Producer wa Muziki Wa Mwaka kwenye tuzo za AFRIMMA 2015,amemshukuru Diamond kwa heshima ambayo amempa kwa kufanya naye kazi na kumkutanisha na wasanii wengi wakubwa.

"Diamond amenipa heshima sana , kufanya nae kazi na kunikutanisha na wasanii wengi tofauti kwahiyo hii ni heshima kwangu, najiona nimekuwa tofauti na nimekuwa mkubwa&#8230;" alimaliza Sheddy.


Chanzo: Bongo5
 
DIAMOND anajua kuwekeza na anaijua biashara ya muziki haishii tu kuwa na sauti nzuri bali kujua soko la muziki linataka nini SAFI SANA DIAMOND.
 
nimeipenda hii, inaonekana Diamond anamuaminia sana dogo ndo maana anamuhusisha kwenye project zake kubwa zaidi ya mara 2
 
Pigeni hela vijana, achaneni na UKAWA.
 
Hadi raha kuisoma

msiompenda na mkae huko na muache kulalamika mabaya mumeyataka wenyewe na ndio muelewe hana muda nanyi...bahati yenu ya kusaidiwa mliipoteza wenyewe kwa upuuzi wenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…