Mtwara: Askari 7 wanaotuhumiwa kuua wafikishwa mahakamani

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Maofisa saba wa Polisi mkoani Mtwara wanaotuhumiwa kufanya mauaji ya mfanyabiashara wa madini, Mussa Hamis (25) anayedaiwa kufariki dunia Januari 5, 2022 akiwa mikononi mwa polisi, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mkoani Mtwara kwa ajili ya kesi yao kutajwa leo Jumanne Februari 22, 2022.

Washtakiwa hao ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Mtwara, Charles Onyango, Mrakibu wa polisi aliyekuwa Mkuu wa Intelijensia, Nicholaus Kisinza, Mkaguzi wa Polisi, John Msuya na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi.

Wengine ni Marco Mbuta, Mkaguzi wa Polisi Shirazi Ally Mkupa, Mrakibu wa Polisi aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi, Gilbert Kalanje, askari namba G5158 Kopro Salum Juma Mbalu. Watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani hapa saa 2:57 asubuhi wakiwa chini ya ulinzi mkali wa Polisi.

Watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Januari 25 na kusomewa shitaka la mauaji ya kukusudia. Kesi hiyo ilitajwa tena Februari 8, ambapo maofisa hao walifikishwa mahakamani hapo. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 8, 2022 itakapotajwa tena.

Tofauti na awali leo waandishi wameruhusiwa kuingia chumba cha mahakama kupiga picha kabla kesi haijaanza.

Kesi Mtwara.jpg
 
Mbona kama Wana subiri tusahau wawaachie
Maisha ya watanzania yanajengwa na matukio, muda husahaulisha watu mambo waliyopaswa kujua mwisho wake.

Hali itakwenda hivi kisha litaisha na maisha yataendelea .
 
Wameharibu maisha yao kwa kushawishiana kufanya uovu.Wako saba tena vyeo vikubwa hakuna hata mmoja angalau angekuwa na wazo tofauti!!
 
Hao watu ni katili sana,, yaan wako na Ajira/kazi Ila bado wanadhulumu na kuiba.. yaan wafungwe maisha tu
 
Sheria inafuata mkondo..Safi sana
 
Maofisa saba wa Polisi mkoani Mtwara wanaotuhumiwa kufanya mauaji ya mfanyabiashara wa madini, Mussa Hamis (25) anayedaiwa kufariki dunia Januari 5, 2022 akiwa mikononi mwa polisi, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mkoani Mtwara kwa ajili ya kesi yao kutajwa leo Jumanne Februari 22, 2022.

Washtakiwa hao ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Mtwara, Charles Onyango, Mrakibu wa polisi aliyekuwa Mkuu wa Intelijensia, Nicholaus Kisinza, Mkaguzi wa Polisi, John Msuya na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi.

Wengine ni Marco Mbuta, Mkaguzi wa Polisi Shirazi Ally Mkupa, Mrakibu wa Polisi aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi, Gilbert Kalanje, askari namba G5158 Kopro Salum Juma Mbalu. Watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani hapa saa 2:57 asubuhi wakiwa chini ya ulinzi mkali wa Polisi.

Watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Januari 25 na kusomewa shitaka la mauaji ya kukusudia. Kesi hiyo ilitajwa tena Februari 8, ambapo maofisa hao walifikishwa mahakamani hapo. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 8, 2022 itakapotajwa tena.

Tofauti na awali leo waandishi wameruhusiwa kuingia chumba cha mahakama kupiga picha kabla kesi haijaanza.

Sirro anatakiwa kuwajibishwa, anaongoza jeshi la wauaji
 
Back
Top Bottom