Askari mmoja Kati waliokuwa wakituhumiwa kufanya mauaji ya mfanyabiashara kijana alijinyonga
====
Askari huyo alijinyonga Januari 22 mwaka huu 2022 kwa kutumia tambala la kudekia akiwa mahabusu ya kituo cha polisi wilaya ya Mtwara.
Katika taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mtwara ACP Mark Njera, alikiri kuwa askari wake saba wanaotuhumiwa kutekeleza mauaji ya kijana Mussa Hamisi (25), mkazi wa kijiji cha Ruponda wilaya ya Nachingwea mkoani humo aliyekuwa akiwadai askari hao zaidi ya shilingi milioni 33.7 wameshafikishwa mahakamani
Imeelezwa kuwa tukio la mauaji ya kijana huyo walilitekeleza Januari 5, 2022 na mwili wa marehemu waliutupa katika kitongoji cha Majengo, kijiji cha Hiari wilayani Mtwara.
Waliofikishwa Mahakamani Januari 25, 2022 ni:
1. Mrakibu wa Polisi Gilbert Kalanje -Mkuu wa Upelelezi wa wilaya ya Mtwara,
2. Mrakibu Msaidizi wa Polisi Charles Onyango - Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara,
3. Mrakibu wa Polisi Msaidizi Nicholaus Kisinza - Mkuu wa Kikosi cha Intelejensia ya Jinai mkoa wa Mtwara,
4. Mkaguzi wa Polisi John Msuya Mganga - Mkuu wa Zahanati ya Polisi Mtwara,
5. Mkaguzi wa Polisi Msaidizi Marco Mbuta,
6. Mkaguzi wa Polisi Shirazi Mkupa na
7. Koplo Salimu Juma Mbalu.
Kuhusu mauaji ya mfanyabiashara, soma Mtwara: Maafisa Saba(7) wa Polisi wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kijana aliyekuwa akiwadai zaidi ya Tsh milioni 33.7 (Januari 25, 2022)