Mtwara: Askari Polisi mmoja kati watuhumiwa wa mauaji ya mfanyabiashara alikutwa mahabusu akiwa amejinyonga tarehe 22 Jan 2022

Mtwara: Askari Polisi mmoja kati watuhumiwa wa mauaji ya mfanyabiashara alikutwa mahabusu akiwa amejinyonga tarehe 22 Jan 2022

Mimi nilikaa MAHABUSU pale madale.ndani Kuna choo mnawekewa na maji .
Pia tambala lipo kwa ajili ya kufutia maji
Uenda hiyo MAHABUSU Ina choo Cha ndani.
Ila Mimi ninachojua polisi kafa.
Haya sawa maana mimi sijawahi ingia humo
 
Halaf jiulize..mahabusu anakuwaga peke yake au mnakua weng

Sent using Jamii Forums mobile app
Na kama IGP SIRRO alikuwa hajui sakata hili tangu tarehe 5jan basi hatuna jeshi la polisi mimi huwa najiuliza hivi sirro anapata wapi fedha kuwaeleza mapub karibu mikoa yote?! Jana nimeshinda kwenye pub yake kilimani pub pale chanika
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].kwani siku ya kuingia utaijua?
Unashangaa tu watu wanakuja wanajitambulisha sisi NI askari kutoka polisi kituo Fulani unahitajika kituoni.
Ushindwe na kulegea wewe!
 
kanyongwa huyo ili kuficha ushaidi………..
 
Afisa wa Jeshi la Polisi mkoani Mtwara, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Grayson Mahembe, ambaye ni miongoni mwa maafisa saba wa jeshi hilo waliofunguliwa mashtaka ya mauaji ya mfanyabiashara, amejinyonga.

Askari huyo alijinyonga Januari 22 mwaka huu kwa kutumia tambala la kudekia akiwa mahabusu ya kituo cha polisi wilaya ya Mtwara.

Katika taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mtwara ACP Mark Njera, alikiri kuwa askari wake saba wanaotuhumiwa kutekeleza mauaji ya kijana Mussa Hamisi (25), mkazi wa kijiji cha Ruponda wilaya ya Nachingwea mkoani humo aliyekuwa akiwadai askari hao zaidi ya shilingi milioni 33.7 wameshafikishwa mahakamani

Imeelezwa kuwa tukio la mauaji ya kijana huyo walilitekeleza Januari 5, 2022 na mwili wa marehemu waliutupa katika kitongoji cha Majengo, kijiji cha Hiari wilayani Mtwara.


Screenshot_20220126_104935.jpg
 
Mmhh mm naona mtu katolewa kafara apoo ili mzigo WA lawama wote abebeshwe yeye wengine waponee
 
Back
Top Bottom