Mtwara: Askari Polisi mmoja kati watuhumiwa wa mauaji ya mfanyabiashara alikutwa mahabusu akiwa amejinyonga tarehe 22 Jan 2022

Mtwara: Askari Polisi mmoja kati watuhumiwa wa mauaji ya mfanyabiashara alikutwa mahabusu akiwa amejinyonga tarehe 22 Jan 2022

Mambo ya kuuana na kutekana Tanzania yaliasisiwa awamu ya Tano chini ya Mwendazake...hizi ndizo gharama zake.

Mke anaua mume
Mume anaua mke
Mume anakodi mtu kuua mpz wake
Mtoto anaua baba kisa urithi
House girl anaua mtoto wa bosi
Kijana anaua girl friend wake
mchumba wa kike anamuua jamaa kisa kaachwa
Askari anaua raia
Raia anaua askari

Yaani sasa hivi ni mwendo wa kuliana timing tu...ukibugi tu umeingia cha kile dadadeq

Ni balaa tupu.
Kina zombe ilikuwa awamu ya ngapi vile?
 
Wameamua kumuondoa ili kupoteza ushahidi wakubwa wao wasitajwe
Ukisikia umafia ndo huu. Unakata mnyororo wa ushahidi kuhakikisha hakuna taarifa zitakazo kuhususha na hicho unachotuhumiwa. Lakini ya Mungu mengi, mahabusu kujinyongea chumba cha mahabusu!
 
Mhh,ila bongo[emoji119]anyway,kila aliyeshusika roho ya mauti imvae!mmoja baada ya mwingine hamtoboi shenz kabisa!
 
Mambo ya kuuana na kutekana Tanzania yaliasisiwa awamu ya Tano chini ya Mwendazake...hizi ndizo gharama zake.

Mke anaua mume
Mume anaua mke
Mume anakodi mtu kuua mpz wake
Mtoto anaua baba kisa urithi
Ndugu wanamuua bibi yao kizee kisa macho mekundu - mchawi
House girl anaua mtoto wa bosi
Kijana anaua girl friend wake
mchumba wa kike anamuua jamaa kisa kaachwa
Askari anaua raia
Askari anamuua askari mwenzake
Raia anaua askari
Raia anamuua raia mwenzake

Yaani sasa hivi ni mwendo wa kuliana timing tu...ukibugi tu umeingia cha kile dadadeq

Ni balaa tupu.
Mbona wewe hujamuua mkeo au raia mwingine?
 
Yani kweli damu ya mtu inakufuata popote uendapo.....yani wamepigwa ganzi,,akili zimechanganyikiwa....basi hata wangesema amejinyonga kwa suruali lake huku amekutwa na boksa tu....sasa dekio !!..yani MOPA !!!!

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Kikubwa Sasa tuelewe watu wanavosema mifumo imefeli wanamanisha na wanataarifa zakweli

Nadhani jeshi lapolisi walidhani wanaongea na wamakonde hawakujua taarifa hiyo inatufikia watanzania nakama tofauti na Hilo Basi jeshi jitakafarini wajitafakari haraka Zama zakutoa taarifa zikabakia Radio Tanzania daresalaaam sikuhizi hazipo
 
Inasikitisha sana nimemsikia mzee wake Leo anaomba uchunguzi ufanyike maana haelew tu kama mwanawe kajinyonga
 
Inasikitisha sana nimemsikia mzee wake Leo anaomba uchunguzi ufanyike maana haelew tu kama mwanawe kajinyonga
Kauli nilizosikia kutoka kwa mzee wake
~kajinyonga na kamba mara dekio
~yeye kasema wanamsumbua tu ila katumwa na wakubwa
~Shingoni kuna michubuko
~Hawajaonyesha mazingira aliyojinyongea
 
Kwani kila mmoja aliwekwa kwenye selo yake? Kuna kitu kinaendelea polisi huko, maana kila kitu ni wao
 
Mahabusu wa Mauaji huwezi waweka wote sehemu moja, watapangana namna gani ya kujitetea. Hao askari waliwekwa mahabusu tofauti, Mkuu wa Kituo akiwekwa LILUNGU, Aliyejiua akiwekwa Kituoni hapo polisi, OC CID alipelekwa Nachingwea nk nk. Ila kupata picha halisi ya kesi kama hizo watuhumiwa wanatenganishwa kwa umbali mkubwa tu na hakuna uwezekano wa wao kukutana mpaka mahakani. Ni possible kujiua. Kama ameawa basi kwa namna yoyote OCD, RPC na RCO watahusika tu.
Hilo dekio aliwekewa mahabusu ili awe anadeki?
 
Askari mmoja Kati waliokuwa wakituhumiwa kufanya mauaji ya mfanyabiashara kijana alijinyonga

====

Askari huyo alijinyonga Januari 22 mwaka huu 2022 kwa kutumia tambala la kudekia akiwa mahabusu ya kituo cha polisi wilaya ya Mtwara.

Katika taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mtwara ACP Mark Njera, alikiri kuwa askari wake saba wanaotuhumiwa kutekeleza mauaji ya kijana Mussa Hamisi (25), mkazi wa kijiji cha Ruponda wilaya ya Nachingwea mkoani humo aliyekuwa akiwadai askari hao zaidi ya shilingi milioni 33.7 wameshafikishwa mahakamani

Imeelezwa kuwa tukio la mauaji ya kijana huyo walilitekeleza Januari 5, 2022 na mwili wa marehemu waliutupa katika kitongoji cha Majengo, kijiji cha Hiari wilayani Mtwara.

Waliofikishwa Mahakamani Januari 25, 2022 ni:

1. Mrakibu wa Polisi Gilbert Kalanje -Mkuu wa Upelelezi wa wilaya ya Mtwara,

2. Mrakibu Msaidizi wa Polisi Charles Onyango - Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara,

3. Mrakibu wa Polisi Msaidizi Nicholaus Kisinza - Mkuu wa Kikosi cha Intelejensia ya Jinai mkoa wa Mtwara,

4. Mkaguzi wa Polisi John Msuya Mganga - Mkuu wa Zahanati ya Polisi Mtwara,

5. Mkaguzi wa Polisi Msaidizi Marco Mbuta,

6. Mkaguzi wa Polisi Shirazi Mkupa na

7. Koplo Salimu Juma Mbalu.

Kuhusu mauaji ya mfanyabiashara, soma Mtwara: Maafisa Saba(7) wa Polisi wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kijana aliyekuwa akiwadai zaidi ya Tsh milioni 33.7 (Januari 25, 2022)


View attachment 2095972
Kwa hiyo walikuwa jumla ya polisi nane(8) marehemu inclusive !!
 
Tambala la deki liue binadamu?? Happ tuanze kesi mpya tena,kuna watu watakutwa na sakata la mauaji ya watu wawili moja haijaisha ameua mwingine
 
Mauaji yametamalaki nchi nzima, kila taarifa ya habari siku hizi kuna mauaji... enzi za jpm watu walidai mauaji na watu 'kutupwa' baharini... sasa hivi naona wanaharakati kimyaaaa....
 
Polisi wetu wana akili ngapi ... ndo maana nasikiaga wengi division Ooooo "" hawakuona drsa.....ivi kweli tambala la deki? Jamani? Liue kamanda mkurya au?? Tena muuaji???? ....jipya au la nguo nzee!

Nyie chezeni tu...nikikamata nchi napiga wote wote chini...na hamnifanyi kitu....km rais.
 
Back
Top Bottom