John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Wimbi la mauaji limeendelea kuzitesa familia za baadhi ya Watanzania baada ya Polisi mkoani Mtwara kuthibitisha mauaji ya madereva bodaboda wawili ambao miili yao imepatikana pamoja na baadhi ya viungo vya mtu mwingine katika pori la Kijiji cha Hiari wilayani Mtwara
Akizungumzia matukio hayo baada ya jitihada za madereva bodaboda kufanya msako mkali ndani ya pori hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo amesema mauaji ya madereva watatu wa bodaboda yametokea ndani ya siku saba na upelelezi unaendelea.
Hamis Mohamed ambaye ni dereva bodaboda ameelezea kuhusu tukio hilo kwa kusema:
“Mwanzo tulikuja kumtafuta kijana mwenzetu ambaye alipotea tukakuta na mwili mwingine wa mtu ambaye hakuwa lengo letu, tukatoa taarifa Polisi wakaja kumchukua, ilikuwa Jumamosi iliyopita.
“Katika tukio hili lingine tuliomba sapoti ya Polisi lakini hawakutupa ushirikiano, tukajipanga sisi wenyewe kwa kuwa aliyepotea ni mwenzetu, tukaja, tukakuta mwili wake una hali mbaya, ulifungwa kamba na inaonekana aliteseka sana.”
Naye baba mzazi wa bodaboda ambaye amwili wake ndiyo uliokutwa mara ya mwisho, mzee Juma Mohamedi amesema: “Nilisikia kuwa alipakia watu wawili akaondoka nao, tangu siku hiyo hakurudi tena.
“Tukakutana ndugu, tukaenda Polisi ambako tulipewa RB, msako ukaendelea, siku ya kwanza ukapatikana mwili wa mtu mwingine, leo (Februari 15) ndipo umepatikana mwili wa mwanangu.”
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo upande wake amesema:
“Tukio la kwanza la Februari 6, 2022 kuliokotwa viungo vinavyodhaniwa kuwa ni vya binadamu ambavyo ni ugoko, utumbo mdogo na mbavu.
“Februari 12, 2022 mwili wa anayedhaniwa kuwa ni Mohamed Juma uliokotwa katika eneo hilo ukiwa umechomwa na kitu chenye ncha kali eneo la sikio upande wa kulia, pia alikuwa amefungwa Kamba.
“Februari 15, 2022 pia tumepata taarifa za kupatikana kwa mwili wa mtu ambaye anatambulika kwa jina la Mohamed Juma Mohamed ambaye pia ni mwendesha pikipiki.”
Pori la Hiyari lipo ndani ya Wilaya ya Mtwara nje kidogo ya Mji wa Mikindani.
Pia soma > Mauaji ya bodaboda Mtwara, Polisi mmeshindwa kazi?