JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mfululizo wa matukio ya mauaji ya kikatili hasa kwa Wasichana yaliyotokea hivi karibuni Wilayani Masasi Mkoani Mtwara kumetajwa kusababisha taharuki na hofu kwa wenyeji.
Kwa mujibu wa taarifa za vifo hivyo tangu Januari hadi Agosti mwaka huu wasichana watano na mvulana mmoja wamekutwa wameuawa na kutupwa.
Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Claudia Kitta amesema kupitia Kamati ya Ulinzi na Usalama wanaendelea na vikao kupata utafiti.
Upande wa Mbunge wa Viti Maalum, Agnes Hokororo amesema mauaji hayo yanaacha maswali mengi na kuviasa vyombo vya usalama kuhakikisha sheria inachukuliwa kwa yeyote atakayehusika.
Source: Azam TV